Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,610
Kipindi fulani nilikuwa ni mwajiriwa wa kampuni moja kama mlinzi wa mali wa zile kampuni hakika nilifanya kadi nzuri na mwisho nikawa mfanyakazi bora wa kampuni kwa namna ambavyo wengi hawakutegemea.
Nilikuwa naingia lindo saa 11 jioni na kutoka saa 12 asubuhi kila siku, ofisini kulikuwa na mali ambazo zilikuwa ndani ya ofisi na nyingine nje ya ofisi. Nje ya ofisi kuliko na jenereta kubwa mbili na ndogo 3, magari ya ofisi nayo yalikuwa yanalala pale pamoja na magari ya wafanyakazi ambao muda mwingine walilazimika kuyaacha pale.
Nilivyokuwa nalinda; nilinunua redio 5 ndogo aina na Kchibo ambazo nilikuwa naziweka maeneo muhimu (yenye mali muhimu) kisha redio zote nilikuwa nazi-tune stesheni moja ya radio, wakati ule nilikuwa napenda sana kusikiliza radio free. Basi nilikuwa naingia saa 11 jioni na ikifika saa 3 usiku naondoka kurudi nyumbani nikiacha redio zinalinda hadi saa 11 asubuhi narudi kuzima redio zangu na kurudi nyumbani.
Nilifanya hivyo kwa zaidi ya miaka 2 hadi siku boss ameniuliza mbona wewe uko tofauti na walinzi wenzako maana zamani kampuni ilikuwa inakumbana na changamoto ya wizi na haijulikani nani alikuwa anafanya vile.
Boss alinipenda sana kwa namna nilivyokuwa nafanya kazi kwa uaminifu na siku moja nilipigiwa simu niende ofisini na kukuta bodi nzima ya kampuni ikaniambia nimekuwa mfanyakazi bora wa mwaka. Hakika sikuamini nilitoka machozi ya furaha mbele yao, jitihada zangu zilipata matunda sikuweza kujua lini kazi yangu itanilipa.