Nilivyokuwa najiona mjanja, nikaishia kutapeliwa Milioni 42

Hata wakati Deci inaanza wabishi walikuwepo wakaishia kupigwa.
Kula na like yangu aisee watu wanakosoa sana
Yaani Wewe soma pita hivi hata kwenye hadithi za kutunga kuna cha kujifunza

Sasa kwa maelezo haya mafupi tu kwa upande wangu umemaliza
Na Sio DECI tu
Kuna kitu hapa Juzi juzi ya KALYINDA na ESCATEC watu wamenyooshwa hivihivi na hakuna majibu mpka leo
Shubaaamiti
 
Leta vitu mkuu tukaribishe pasaka vizuri....ila ni story flani hiv unakua kama unaangalia movie na imetukumbusha mengi ya shuleni
 
Mkuu unaamini hii ni uongo kwa sababu ya mazingira uliyosomea.
2010 una uhakika hupati wali wa 200!?
Kitu hawa watunga story hawajui ni kuwa unaweza kabisa kusema ni kisa cha kutunga na bado watu wengi wakavutiwa. Kusema ni kisa cha kweli wakati unatunga ni udanganyifu na hii ni sumu kweli kweli kwenye uandishi. Báhati mbaya kwao ni kuwa kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kusoma na kujua kuwa ni uongo. Kwa mpenda kusoma vitabu kama mimi hawa watunzi wa JF wako level ya chini sana kiasi cha kuweza kunidanganya. Ni kama matapeli tu, siku zote tapeli anakuwa na maneno meeeengi akidhani kuwa ndiyo ataaminika kwa urahisi. Kwenye tunzi kama hizi kuna vitu wanafanya makosa kuvisimulia ambavyo kwa hali ya kawaida visingepaswa kusimuliwa.
 
Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.

1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.

Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.
Mwaka 2003-2004 ubwabwa maharage na nyama hapa dar ulikuwa shilingi 200-250 ..sio kila kitu cha kubisha na jamaa ipad kaanza kuziuza yupo chuo ...probably ni 2010-2011-2012..

Na kweli pesa ya stationary chuoni ilikuwa ni shilingi 620,000..unaenda kuchukua dirishani kwa muhasibu soon after orientation period kuisha.

Sio kila kitu ni cha kubisha
 
Kitu hawa watunga story hawajui ni kuwa unaweza kabisa kusema ni kisa cha kutunga na bado watu wengi wakavutiwa. Kusema ni kisa cha kweli wakati unatunga ni udanganyifu na hii ni sumu kweli kweli kwenye uandishi. Báhati mbaya kwao ni kuwa kuna watu wenye uwezo mkubwa wa kusoma na kujua kuwa ni uongo. Kwa mpenda kusoma vitabu kama mimi hawa watunzi wa JF wako level ya chini sana kiasi cha kuweza kunidanganya. Ni kama matapeli tu, siku zote tapeli anakuwa na maneno meeeengi akidhani kuwa ndiyo ataaminika kwa urahisi. Kwenye tunzi kama hizi kuna vitu wanafanya makosa kuvisimulia ambavyo kwa hali ya kawaida visingepaswa kusimuliwa.
Labda uko sahihi, mimi kufikia naingia jf basi nina mda wa kupoteza so i don't look for perfection just kuburudika tu.
Pili kupangilia story ni kipaji yawezekana ni kweli lakini ukashindwa kupangilia matukio sawa sawa au ni uongo lakini ukapangilia vizuri
 
Tatizo watu huwa hawazingatii details ndogo ndogo...jamaa kasema wakati anaingia form 1 ...chai tu ilikuwa shilingi 200..!! Nakiri kwa nyakati za miaka ya mwanzoni mwa 2000-2004 ulikuwa unaweza kupata breakfast kwa pesa hiyo.
Chapati zilikuwa zinauzwa sh 50,andazi shilingi 10-20, vitumbua shilingi 10-20 ...chai ya rangi sh 10-20.

Mfumuko wa bei ulikuja utawala wa kikwete ila kipindi cha mkapa life was easy n cool.
 
mzee, mimi sio mwandishi wa story lakini nataka kuoa binti bikra. Nikaribishe nyumbani nipate kujesevia
Nitakutajia mahari nayo hutaiweza kijana wangu.Wewe endelea kuchukua haohao wenzio used kote kote.

Mm ni mpenzi na mtunzi wa hadithi hivyo nikiona kijana akiandika story nzuri huwa natamani kuwa naye karibu na kwa kuwa nina wakuuu wa kike napenda pia kutumia fursa hiyo.
 
Kwa mamlaka niliyojipa ninautangazia umma kuwa huu uzi ni chai... tuusome kwa kujifurahisha tu hakuna uhalisia wowote hapa.

1. Form one alienda akiwa hajui kama shule haina wanafunzi wa kike. Wasichana kutokuwa admitted ni badiliko kubwa sana ambalo huwa sio la siri. Chai no. 1
2. Chakula Tsh 200 canteen. Kama alisoma wakati wa iPad zinatoka ni kwamba sio miaka mingi iliyopita. Kukadiria ni kama 2010 kuendelea. Vyuoni misosi ilikua Tsh 1000 na zaidi. Hakukuwa na uwezekano upate kwa Tsh 200 wali maharage hata kwa shule za sekondari. Au ilikuwa ni Ihefu sec school? Chai no.2
3. Biashara ya mkopo kwenda smoothly bila mgogoro wowote ni Chai no.3 kwenye biashara ya mikopo lazima watokee wasumbufu. Labda kama wateja ni malaika.
4. Kumiliki simu 4 maalum kwa kutazama porn shuleni ni Chai no.4 hii isingeweza kuwa siri kwa vyovyote vile lazima lingemfikia mwalimu wa nidhamu. Katika wanafunzi kuna wenye maadili wasingelifumbia macho. Kuna wenye wivu na pesa unazopiga wasingekaa kimya. Kimsingi hustles za ndugu mwandishi wakati wa secondary zimetawaliwa na chai.

Kwa hustles za Chuo sina tatizo nazo maana angalau zinawezekana.

Mwaka 2005-2006/7 wakati naishi Buguruni maghettoni, chakula pale Chama/Sheli kwa mama nitilie tulikuwa tunalipa 300/=. Alafu huyu alikuwa anazungumzia canteen ya shule ya sekondari siyo UD.

Kwenye jonining instructions jamaa ametoa maelezo kuwa ishu ya shule kubadilisha sera haikuondolewa, hivyo yeye alienda akijua ni mchanganyiko kama kawa.

Kama unaona chai, lete stori yako isiyokuwa chai otherwise acha wivu na upunguze wenge.
 
Acha ujinga, hata mimi nimekula wali nyama kwa Shilling 300 nikiwa form 1
 
Labda uko sahihi, mimi kufikia naingia jf basi nina mda wa kupoteza so i don't look for perfection just kuburudika tu.
Pili kupangilia story ni kipaji yawezekana ni kweli lakini ukashindwa kupangilia matukio sawa sawa au ni uongo lakini ukapangilia vizuri
Sizungumzii kupangalia wala kipaji cha kuandika. Unaweza kuwa na kipaji cha kupangilia na kuandika ila usiwe na kipaji cha kudanganya au ''kuchota'' watu akili. Infact hawa watunga uongo kosa lao kubwa ni kujaribu kupangilia story zao kupita kiasi.
 
Mkuu twende kwa mifano hapo uongo uko wapi unaoweza kuuona bila shaka
 
Mwaka 2005-2006/7 wakati naishi Buguruni maghettoni, chakula pale Chama/Sheli kwa mama nitilie tulikuwa tunalipa 300/=. Alafu huyu alikuwa anazungumzia canteen ya shule ya sekondari siyo UD.

Kwenye jonining instructions jamaa ametoa maelezo kuwa ishu ya shule kubadilisha sera haikuondolewa, hivyo yeye alienda akijua ni mchanganyiko kama kawa.

Kama unaona chai, lete stori yako isiyokuwa chai otherwise acha wivu na upunguze wenge.
Canteen ya chuo nimeweka kama mfano. Kwanini mnang'ang'ania stori zenye harufu ya uongo zisikosolewe?
 
Kwanini watu mnapenda mambo ya uongo uongo? Ndo maana matapeli wanatupiga kila upande. Tunapuuzia sana mambo hata kama ni uongo wa wazi. Kwanini tulazimishane kuamini mambo yasiyo na uhalisia? Mwandishi angeweka Disclaimer kwamba hii ni stori ya kufikirika na haina uhalisia tusinge-criticise
Unateseka ukiwa wapi?
 
Mleta mada tuletee episode 2 ya kulia pasaka hata sisi wazee tunapenda hadithi zenu vijana.

Mleta mada hongera kwa kuleta uzi huu na umeandika vizuri na kwa urefu endapo kama bado hujaoa karibu nyumbani kwangu uchague nina wakuu wengi wa kike na wengi wao ni bikra.
Umejuaje kama ni bikra?
 
Back
Top Bottom