Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Hapa jamaa naona alishaanza kutulisha matango pori
 
Mnaomsubiri jamaa arudi jichangeni kabisa akirudi atakuja na post kama β€œtukutane kwenye group hili kwa muendelezo zaidi” akiambatanisha na kiji-link ka ku-join ukijipendekeza mtu tu jua umegeuka fursa atakutaka ulipe 5K au yoyote atakayoona inafaa ili kusoma zaidi na hivi kuna sehemu kasema alisambaza barua za maombi ya kazi na hajafafanua hizo kazi alipata au hakupata sasa wale wanaotamani kujilipua watataka kujua kweli alipata?ili nao wajaribu bahati yao.

Nawasikitikia maana hawa ndo hasa watakaokuwa wahanga wake but
mimi nasema akifikia hatua hii mods kuleni kichwa aoshwe BAN ambayo hajawahi kuiona ili akili imkae sawa.na hapa wamekuwepo watu wa hivi wengi sana ifikie mahali uzi kama huu ukishaanza kuwa na vi-episodes vinavyoonekana mwisho wake siyo leo basi mods wasiziachie hapa hadi hao wanaotaka kuhadithia mikasa yao watakapomaliza kuzipandisha kwenye server ya JF.

Inachosha sana mtu ku-scroll post #1370 hadi #2207 hujakutana na muendelezo,worst zaidi ni hao wataokutana kwenye group maana huko watakutana wote akili yao moja kufahamu jinsi ya kupata kazi South hakutakuwa na wigo mpana wa maswali ya msingi ya kufungua akili kama hapa so wakijichanganya wakaenda kwa kufuata yaliyosimuliwa hapa na msimuliaji ambaye sometimes naye alisimuliwa tu watapata tabu sana.
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA.

Na Keagan Paul
Ile Asubuhi kabla ya Safari kuanza, Kuna wadogo zetu kama 4 wa umri kama wa Miaka 16/17/18 walipanda ndani ya Bus. Waliomba kwa Konda kuongea na Abiria. Walituambia kuwa na wao wanaelekea South Afrika ila nauli zao ziliishia pale Tunduma. Waliomba tuwachangie Nauli.

Wametokea Dar ila wamekaa pale Tunduma kwa muda wa wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Kwa hiyo walikuwa wanaomba tuwachangie nauli ili waweze kuendelea na safari. Tulianza kuwachangia, Mmoja wao alikuwa na simu akaiuza mle ndani ya Bus. Madogo walikuwa wamechangamka sana. Mpaka wanakwenda South kwa nauli za kuunga unga. Wenyewe kutumia Mwezi mzima njiani ni kawaida tu.

Akiba waliyokuwa nayo, pamoja na Michango yetu waliweza kupata nauli ya kuwafikisha mpaka Harare. Walisema wakifika Harare watakaa tena wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Hivyo tuliendelea nao na safari kwenye bus letu. Kwa kifupi mbele ya safari katika kupiga piga nao story tulikuja kujua kwamba kati ya wale madogo, mmoja wao ndio kiongozi wao, yeye alishawai kuishi sana South Afrika. Ilionekana kila akirudi kwao Manzese Tanzania, wakati wa kuondoka huwa anachukua Vijana wengine anaenda nao South. Yani kwa zile story za Madogo nilijiona kumbe ni mim tu ndo sijafika South Africa, Kwa maelezo yao ni kama vile Vijana wengi wapo huko tayari.

Ni kweli kwa pilikapilika za Vijana niliowaona pale Tunduma niliona ni kama Vijana wengi sana wanaikimbia hii nchi, kila mmoja akilalamika kuwa Bongo Maisha magumu.

Staili ya hawa madogo kusafiri ni ya kuunga unga nauli, hawa madogo walivyofika Tunduma walikaa hapo, sidhani kama Kuna namna nyengine walifanya ili kupata nauli zaidi ya wizi. Na wapo madogo wengine wengi wa staili hii.

Pia pale Tunduma sio Waburundi wote walifanikiwa kupita, kuna baadhi walikosa pesa ya kulipia Visa ya kuingia Zambia. Sisi watanzania tunaingia Zambia bila kulipia Visa. Hivyo waburundi ndani ya Bus walipungua

Kila tulivyokuwa tukiendelea na Safari ndivyo Lugha yetu pendwa ya Kiswahili ilivyokuwa ikipotea. Tulifika Lusaka Mji Mkuu wa Zambia saa tatu usiku. Tulilala hapo. Wengine tulishuka kwenda kupata Huduma za Chooni, Wengine ndo ilikuwa mwisho wa safari yao. Asubuhi kulivyokucha tuliendelea na safari yetu ya kuelekea boda ya Zambia na Zimbabwe inaitwa CHIRUNDU









 
Wanasema trust no body in de world.....Kitu kimojaa ambacho nimejifunza nikiwa ugenini....urafiki ni affection....ni kitu ambacho hu tokea automatically.... accidentally
Maisha popote....maisha mpangaji mungu
 
Kama haudindi ni wewe Sisi ni malijari ......SASA kama kizazi kimesimama unataka niwaze kuoga akati nataka kut****mba
 
Uko serious kweli kuanika hbr hapa
 
h bora umeamua kutupoza na uzi huu
 
Aisee hii balaa tupu.....
 
Ningekuwa mod ningefuta huu Uzi..
Huu Uzi hauendelei Tena ndo umeishia hapo!!!
Hadi nyie mnaoponda hii stori bado munataka KP aendelee kutiririka ama kweli dunia ina mambo jogoo anaweza kutaga. Sasa kama mnajua kuliko mshikaji si mtiririke experience zenu za south au hamjui kuandika stori? πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Naona KP kaamua aipeleke telegram asante[emoji16][emoji16][emoji16]
 

Sefu tall wa mabibo!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…