Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Mkuu hata mimi Nov 2019 niligongewa three months japo nilikaa 2 weeks nilienda kikazi nikiwa na full documents zinazoonesha mwaliko wangu na siku ninazopaswa kuattend zilikuwa saba nikaongeza zangu saba ili nizurure kidogo ... immagration walinigongea three months....nilikuwa na documents zote hadi confirmation ya hotel niliyofanya booking....invitation letter nk.
.tofauti na matarajio yangu Tanzania ndo waliangalia hizo nyaraka zote ila upande wa SA aliniuliza tu nikamwambia bila kukagua nyaraka akapiga muhuri wa miezi mitatu passport yangu...

Nilirudi nikiwa na miezi miwili na wiki kama mbili mbele....ingekuwa sio kazi ningekaa kaa kidogo sababu by that time nilikuwa nishapata marafiki tena wanaojielewa

SADC countries inaruhusiwa miezi 3 japo sijajua kiundani kwa nini wengine wanangewa mwezi au chini ya mwezi naendelea kujifunza kwenye uzi wa huyu jamaa
 
Vipi story yako IMEISHA AU ??
 
Ni kias ganii boss mfano unatakaa kuongezaa miezii miwiliii
Kwenye kuongeza inategemea unataka kuendelea kuishi huko kwa shughuli gani? Maana unapotaka kuongeza inabidi utoe sababu maana kuna visa za aina tofauti tofauti kama ya kusoma, kufanya kazi, volunteer etc na zote zina gharama yake.
 
Ngoja mimi niendelee wakati tunamsubiri Keagan Paul

Wakati tumemaliza ibada kwenye muda wa saa 3 usiku, ikabidi wanakwaya tuanze safari ya kurudi kwenye hotel soo wakati tunapanda kwenye usafari bahati nzuri Tshespo akaja kukaa pembeni yangu .

Niseme ukweli Tshesipo alikuwa kachangamka sana na kuonesha ukaribu sana na mimi wakati bado tuko kwenye gari akaniomba Camera akawa anaangalia zile picha tulizopiga asubuhi kule mlimani na kuniuliza hii umeipenda?? Hii imetoka vizuri huku akitabasamu

Wakati tumekaribia kufika kwenye zile hotel pembeni kidogo kulikuwa na kama hoteli ambayo njee kulikuwa na restaurant ambayo watu walikuwa wakipata chakula vinywaji na mziki kidogo mara tshespo akasema sehemu nzuri sana kwa kupata chakula imetulia na mimi pia nikadakia nzuri sana akasema basi akasema tukifika kwenye hoteli tugeuze hapo kupata chakula.

Basi tuipofika pale hotelini nilienda room kwangu nikajiandaa fasta nikawa namsubiria Tshesipo huku nikiendelea kuscroll camera mdogo mdogo kuangalia picha za Tshespo. Baada ya dakika chache nikaona sms keagan toto la konda, toka njee
shuka chini hapa parking.

Daa kotoka njee nilivyomuona sikujua kama ndio Tshespo tulietoka nae kanisani maana alikuwa kabadiika haswa, hapa ndio niiona urembo aliokuwa kabarikiwa Tshesipo maana alikuwa kavaa skerti fubi inaishia magotini,,mahips na tako yalivyokuwa yamejaa ndani ya hile sketi plus ule mpasuo ungedhani sketi ile inachanika ndani ya dkk mbili

Nywele zlikuwa zimeangukia mgongoni, chuchu saa sita oclock, guu sasa ndio nilichoka asee, guu nilidhani ni paja la mange kimambi, nikasema hapa keagan lazima leo nimueleze hisia zangu, baada ya kufika pale akesema mbona unaniangalia sana, nikamwambia hapana umependeza sana akacheeka huku tukiongozana kwenda restaurant .
 
Mkuu shusa uzi wa hii nondo.

Kama ikikupendeza tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kuongeza inategemea unataka kuendelea kuishi huko kwa shughuli gani? Maana unapotaka kuongeza inabidi utoe sababu maana kuna visa za aina tofauti tofauti kama ya kusoma, kufanya kazi, volunteer etc na zote zina gharama yake.
Gharama kubwaa mfano ya utaliii
 
Puuuzi kweli were.ahah
 
Gharama kubwaa mfano ya utaliii
Kwa kweli gharama za visa tofauti na nilizokuwa natumia sizijui. Volunteering niliyokuwa natumia ilikuwa rand 420. Ila mtiti upo kwenye kuiongeza masharti yake ni kama unaomba kuwa rais wa nchi.
 
Mkuu imalizie mwenyew, deputy author wa bashite tuhamia kwa riki boy tukanywe chai na kashata za wavulana huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…