Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Mura amang'ana me pia nimezaliwa Mogabir basae tukahamia tarime town then tukahamia dar mura weito napajua kewilanga mtoni/ napajua kedeli/napajua mtingiro [emoji23][emoji23][emoji23] na kukirighiri center pale [emoji23][emoji23]
Nimeishia hapa
 
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane!.

Kwenye haya maisha kuna wakati huwa ninakaa chini na kusema "Kama sikufa kipindi kile,basi siwezi kufa mpaka Mungu atakaporuhusu".

Nadhani wengi mtakumbuka ni siku chache tu zimepita nimeandika kisa cha maisha ambayo nilikutana nayo wakati nikiwa nimekwenda kumsalimia baba yangu mdogo akiwa ni Headmaster, maisha yale yalikuwa ya kawaida ila washirikina walifanya tukakosa amani.

Sasa baada ya hapo nilifaulu vizuri tu kuelekea shule ya upili(advance)na nikapangiwa huko Tanga kwa mchepuo wa Sayansi wenye combination PCB. Hali yangu ya maisha ya shule kiukweli ilikuwa mbaya sana mpaka nikajuta kwanini nilichukua hiyo combination, siyo kwamba sikuwa na akili, la hasha!,akili ilikuwepo ya kutosha kwasababu nilifaulu kwenda advance kwa divisheni 2,ni combination iliyohitaji kupiga msuli kana kwamba umetumwa na kijiji, haikutaka mchezo wala kujisahau hata kidogo,sasa mimi nilipofika huko nikajikuta naungana na makundi na kujanjaruka kuwashinda hata niliyowakuta!.

Mkurya mimi kutoka wilayani Tarime kijiji cha Mogabiri nikajikuta nazamia kwenye dimbwi la mapenzi ya mtoto wa kitanga ambaye alifanya hata kusoma nikaacha nikawa namuwaza yeye na utamu wa papuchi yake!.

(Shamima popote ulipo ulaaniwe mbwa wewe kwa kuniharibia maisha[emoji23][emoji23]). All in all ni kwamba napambana na maisha yanasonga japo ni kibishi!. Sasa haya ya kwanini nilifeli nadhani kwa leo si mahala pake,nitawaeleza tu kilichofuata baada ya mimi kufeli shule!.

Kiasili mimi ni mkurya kutokea wilaya ya Tarime huko kijijini Mogabiri,ingawa hatukuishi sana hapo kijijini lakini ndipo chimbuko letu lilipo hapo, kwa pale Tarime mjini nyumbani kwetu ni Rebu.Pia tunao ndugu wengi tu waliotapakaa karibu kila kona ya hii nchi!, hapa Dar es salaam wamejaa ila wanajifanya kama hawanioni vile!(Maisha ya sikuhizi yamekuwa yakipumbavu sana).Kwakuwa wanajifanya kukausha na mimi pia napiga mikausho ya hatari!,sitaki kumgasi mtu!.

Basi bana, nakumbuka ile nimemaliza skonga nikawa nashangaa shangaa pale nyumbani kusubiri tokeo la kuelekea chuo, sasa nilifahamu kabisa siwezi kufaulu kwa kile nilichokifanya kule skonga, Mzee yeye aliamini toto lake limemaliza shule na anajivunia kwasababu nilikuwa nina akili,hakuelewa kabisa kwamba baada ya kufika shule nilijanjaruka kuwazidi hata niliowakuta!. Baada ya matokeo kutoka na ikaonekana nimepata divesheni zero, mimi kwa upande wangu sikushituka ila Mzee alihamaki sana na kushangaa nilipatwa na nini hadi nifeli!.

Tangu nimeanza darasa la kwanza hadi darasa la saba, sikuwahi kuvuka namba 5,ingawaje sikuwahi kuwa namba 1 lakini nilikuwa nacheza kwenye namba 2-4. Nilipofika form 1 hadi form 4 wembe ukawa uleule!,nashika namba 3 -5,sasa hadi nafaulu kuingia advance Mzee wangu hakushangaa maana alifahamu kabisa toto lake nilikuwa nina akili!.Mzee wangu kiukweli alikuwa mkali mno na ilikuwa ikitokea nimefanya kosa akanikamata,kiukweli nilikuwaga naimba Haleluya!.Yeye alikuwaga achapi kwa fimbo za miti ya kawaida,bali alikuwa anachapa kwa nyaya ya umeme!,Aisee usiombe kukutwa!.Kuna muda nilikuwa nikifahamu nimefanya kosa siku hiyo najiwahisha kuoga na kuingia kulala na kujifanya naumwa!,sasa akija akikushika shingoni kama anakupima joto akakuta huna joto,aisee utaomba ardhi ipasuke ikumeze ili ikuepushe na kipigo kisichokuua ila chenye kukufanya ukajuta kwanini ulizaliwa!.

Kutokana na kutokuridhika kwa mzee na yale matokeo, kuna siku kadhaa sikumuona pale nyumbani nikajua uenda atakuwa kwenye mambo yake, sasa kumbe mzee amesafiri hadi Tanga kwenda kuonana na Headmaster kufahamu mwanae ni kwanini nimefeli kiasi kile na wenzangu kufaulu!, Alichoamini mzee ni kwamba sikustahili kufeli na nilipaswa nifaulu!. Ule mpango wa yeye kwenda Tanga kumbe hadi Maza nae alikuwa akifahamu ila aliamua kula buyu ili ukweli ufahamike!, Mama yangu alikuwa rafiki yangu mkubwa sana na yeye peke yake ndiye shida zangu zote nilikuwaga nikimwambia!.Ila safari hii na yeye aliukaza uso wake na hakutaka kabisa kucheka na kima!.

Mwanaume niliendelea kujinafasi na kujimwayamwaya kwa kipindi kile kifupi ambacho mzee hakuwepo nikiamini atakuwa ameenda kwenye shughuli zake, akili yangu iliamini kwasababu mzee wangu alikuwa akinimini basi angenipatia mtaji ili nianze biashara!.

Baada ya kama siku 5 mzee alirejea, sasa tukiwa tunapata chakula usiku alikuwa akiniangalia kwa jazba sana, sikuwa na tatizo nae kwasababu niliamini yeye kuwaga na hasira za karibu ndiyo ilikuwa kawaida yake!. Sasa ile naendelea kula sijui ili wala lile,nilishitukia amenipiga kofi ambalo lilifanya kuanza kuona maluweluwe!.

Mama "Tamtigha omwana araghere!"(Muache mtoto ale)

Mzee "Amos hebu niletee waya hapo chumbani"

Sasa mdogo wangu aitwaye Amos akaagizwa waya akachukue waya ili viboko vichukue nafasi!.

Mzee "Leo nakuua mbwa wewe"

Kiukweli siku hiyo nilijua kabisa nakufa maana mzee wangu alikuwaga hana masikhara kabisa na maneno yake!. Basi mama alikuwa akijaribu kumtuliza mzee lakini bado ikashindikana, kwa wakati huo sikuelewa kabisa ni kitu gani kilimsibu mzee wangu ambaye alikuwa amerejea kutoka huko alikokuwa ameenda!.

Mzee alinyanyuka akatoka akaenda ndani ambako sikufahamu alikwenda kufanya nini,wakati huo kiukweli hata chakula sikuwa na hamu nacho tena kwasababu mabanzi na makwenzi niliyokuwa nimechezea yaliniharibia mudi kabisa!.Baada ya mzee kutoka chumbani alikuja na kamba ya katani akanisogelea akanifunga na kunibana miguu kana kwamba anataka kuchinja kuku!,sasa akauchukua ule waya uliyoletwa na dogo nikaanza kuchezea stiki!,kiukweli nilipigika sana!. Baada ya kuona ameniadhibu vya kutosha alinilaza kifudi fudi wakati huo kanifunga mikono kwa nyuma kama vile jambazi au mwizi amepigwa pingu.

Mzee "Leo nakuua, sali sala yako ya mwisho!"

Aliendelea "Siwezi kuharibu pesa yangu halafu wewe uende shule kuwa mtoro!"

Baada ya kusikia ile kauli basi nikajiongeza kiakili na nikafahamu kabisa atakuwa alikwenda shuleni kuutafuta ukweli wa mimi kufeli!.Kiukweli nilikiona kifo kiko karibu yangu!.

Mzee "Yaani nakulipia karo wewe unaenda kuvuta bangi shule?"

Aliendelea "Hizo bangi ulianza kuvuta lini?"

Sasa nikaanza kushangaa ni nani alimwambia nilikuwa navuta bangi? Kiukweli kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwenye maisha yangu ni huo uvutaji wa bangi alionieleza!.

Mimi "Hapana baba sivuti bangi!"

Mzee "Leo utanitambua mshenzi wewe"

Kiukweli kujitetea ilikuwa ngumu sana maana kila nilipojaribu kujitetea nilionekana muongo na kuishia kukandamizwa viboko visivyokuwa na idadi!. Sasa kumbe alipokwenda kule shuleni, walimu walimwambia ya kwamba mimi nilijiingiza kwenye kundi la waliokuwa wameshindikana na kuanza kujihusisha na uvutaji wa bangi!,walimu pia hawakufahamu hicho hakikuwa chanzo cha mimi kufeli bali ilibidi wamwambie mzee kwasababu ya kuniona mimi kukaa na watu ambao pale shuleni walikuwa wameshindikana!.Na kwa kipindi kile walimu walikuwaga hawaangaiki na mtoto wa mtu,wao walikuwa wakituambia mwisho wa mambo yote ni pepa(mtihani)ndiyo utakaochuja nafaka halisi na magugu!.

Basi bana, baada ya kupigika sana na mzee kunishikia panga, ilibidi maza aingilie kati kwa kujifunga kibwebwe na kumkoromea mzee!.

Mama "Hivi baba Sarah unataka kumuua mtoto kisa kufeli shule!"

Aliendelea "Kama humtaki mtoto muache akatange tange huko!"

Basi baada ya mama kuingilia kati, mzee aliniacha na akanitaka nipotee pale nyumbani na nisije kumtambua kama baba yangu. Mama alinisogelea na kunifungua zile kamba mkononi na miguuni!. Kiukweli nilipigika sana.

Nilitoweka pale sebuleni nikaelekea chumbani kulala huku nikiendelea kulia kwa kwikwi, mwili wangu wakati huo ulikuwa umejaa alama ya nyaya za umeme zilizosababishwa na kile kipigo!.

Usiku huo kiukweli sikupata usingizi kabisa kutokana na maumivu ya viboko!.
Ina muendelezo au
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 5.




Nilibaki kushangaa zile hela namna zilivyokuwa uimejaa kwenye lile begi!,kiukweli mate ya tamaa yalianza kunitoka ndani ya moyo!.Nilikuwa nipo tayari kusikia maelekezo atakayonipa ndugu Gabi ili niweze kuyafuata ilimradi tu niweze kujipatia zile hela!.Mawazo yangu kiukweli yalihama na kunichukua kuanza kufikiria vitu vya kijinga,nilitaka baada ya kuzipata hizo hela nikanunue mkoko(Gari) ili niende nikamdolishie dingi ajute kunikataa na kuniona sifai!.Kiukweli niliwaza ujinga sana.


Gabi "Sa sikia jamaa yangu"

Aliendelea "Hii ni pesa ya Tanzania lakini si halali"

Mimi "Si halali!,kivipi tena isiwe halali?"

Gabi "Yes!,swali zuri,ndiyo maana nimekutafuta wewe nikiamini unataka hela"

Mimi "Hakuna mtu asiyetaka hela kaka,we niambie nini nifanye"

Gabi "sawa,sasa humu ndani tupo watu watatu,yaani mimi,wewe pamoja na wife".

Aliendelea "Tulipoingia ndani nilimwambia wife afunge mlango ili isije mtu akaingia ghafla kama anaingia chooni"

Gabi "Sidhani kama wewe ni mtoto baada ya hapa ukaanza kupayuka payuka kama mwendawazimu"

Aliendelea "Hizi ni hela bandia na ndiyo maana nimesema si halali"

Gabi "Mimi kukuleta hapa ni kwasababu nina muamini sana Mtatiro na tumeshapiga sana hizi mishe,sasa naomba mwanangu tukubaliane kwanza"

Baada ya jamaa kuniambia zile hela niza bandia,kiukweli nilibaki kushangaa kwasababu ulikuwa ukiziangalia zilikuwa zinaonekana kabisa ni pesa halali kwa matumizi na ilikuwa ni vigumu sana kuzitambua labda mpaka uwe mtaalamu wa hali ya juu.

Gabi "Sababu ya mimi kukwambia ni pesa bandia ni kukulinda wewe na sisi pia"

Aliendelea "Ningeweza kukwambia tu shika mzigo nenda kafanye moja mbili tatu halafu kila mtu akafa na chake,lakini nimeona wewe bado mgeni wa haya mambo na pengine ungedakwa ungewaleta hapa mapongo"

Mimi "Kaka siwezi kabisa kufanya huo upuuzi"

Gabi "Sa sikia Umughaka,kwenye kila elfu 10,wewe yako tano na sisi yetu ni tano"

Aliendelea "Sasa ni juu yako kuhakikisha kila mzigo nitakao kuwa nakupatia unamaliza ili uchukue chako na chetu tukipate!"

Mimi "Sawa kaka,kwahiyo niambie sasa nafanyaje"

Gabi "Mimi kila siku nitakuwa nakupatia shilingi laki moja,wewe ndiyo utahakikisha hiyo laki unaichenji unabaki na yako fyu(50) na sisi ya kwetu fyu".

Basi baada ya jamaa kuniambia vile ikabidi sasa akili ianze kukimbia fasta!,Jamaa alitaka kwenye ile laki moja atakayonipatia kila siku,nihakikishe naingia mtaani kuwashikisha wadau ili pesa yao iwe ni elfu hamsini na yangu pia iwe elfu hamsini,kwakifupi tuwe tunakula pasu kwa pasu!.Baada ya yale mazungumzo jamaa akanitia laki moja nikatia mfukoni akanipatia na nauli ya kunirudisha mpaka Sirari!.

Gabi "Ukiwa unamaliza mzigo utakuwa unanicheki kwenye simu,kama sipo nitakuwa nakujulisha ili ukija utamkuta shemeji yako utamuachia cha kwetu atakupatia mzigo mwingine"

Mimi "Haina noma kaka"

Basi nikaondoka zangu kurudi Sirari!,nikiwa njiani nikamtafuta Mtatiro kwenye simu kutaka kumfahamisha lile dili!.

Mtatiro "Mwanangu hilo dili lina hela kama ukituliza akili,cha muhimu ni kuwa na siri sana na pia jiamini usije kujishitukia shutikia"

Aliendelea "Mwanangu mi mbona nimefanya sana hiyo kazi na mshikaji,vitu vyangu vyote vya ndani ulivyoviona nimenunua kwa pesa ya mshikaji,ni dili tamu sana sema mshikaji kuna muda nae anapoteaga sana ndo maana nikaamua niingie kwenye hiace angalau niwe napata hela ya kula"

Aliendelea "Mimi nikirudi kama jamaa bado akiwepo tutaungana kaka"

Mimi "Kwahiyo Mtati wewe ulikuwa unafanyaje fanyaje mwanangu,nipe mbinu za kuzibadilisha"

Mtatiro "Jamaa amekwambia atakuwa anakugei kiasi gani?"

Mimi "Ameniambia kwenye kila elfu kumi,yangu tano na yake tano"

Mtatiro "Ni vile vile tu kama kwangu ilivyokuwa,sasa sikiliza wewe uwe unaingia madukani unanunua vocha ya buku,hiyo ni rahisi mno na kwa pale Sirari bado kuna wajinga wengi"

Mimi "Mbona kama buku ni nyingi sana kaka,au niwe nanunua tu ya jero!?"

Mtatiro "Vocha ya jero ni ngumu sana kupewa chenji na nirahisi kushituka ila ukinunua Vocha ya buku kwenye kila teni wewe utakuwa unachukua yako buku nne na jamaa unamlelekea buku tano yake"

Mimi "Sawa kaka nimekuelewa,ngoja niingie kitaa"

Mtatiro "Kwani uko wapi sasa hivi?"

Mimi "Ndiyo natoka kwa mshikaji"

Mtatiro "Sawa mwanangu kapambane,uwe unanikumbuka angalau ka vocha"

Mimi "Haina noma"


Basi niliucahapa mwendo kuelekea barabarani ambapo nilikamata Hiace za kunipeleka mpaka mjini ili nikadandie vimchomoko vya washikaji nirudi Sirari!.Kwa wakati huo baada ya kupata umaarufu na kuwa mwenyeji pale Sirari,nilikuwaga silipi nauli kama nikitaka kwenda Tarime au kurudi Sirari,nilikuwa nadandia tu gari yoyote iliyokuwa ikielekea sehemu husika kwasababu nilikuwa nafahamika!.

Baada ya kufika pale Sirari siku hiyo niliamua kuendelea na kazi yangu ya upiga debe huku nikiendelea kusoma mazingira na namna ya kuifanya hiyo kazi yangu mpya.
Sasa siku iliyofuata nilichukua noti ya elfu kumi kati ya zile hela bandia na kuitazama vizuri,kwakweli ilikuwa ni ngumu sana kuijua kwasababu ilikuwa na kila kitu ambacho kilipatikana kwenye noti halali,utofauti ambao nao ulikuwa kwa mbali labda ilikuwa harufu tu!,zile hela ulikuwa ukizinusa kwa ukaribu sana zilikuwa na hatufu fulani ya karatasi nyuepe(rim paper).

Nilichukua noti 3 ambazo zilikuwa elfu 30 nikaingia zangu pale stendi kupiga debe kama kawa!,sikutaka kabisa kuchenji zile hela kwa wadau wangu wa vimchomoko kwasababu niliona ningewaumiza wadau!.Sasa ilipofika mida ya saa 4 asubuhi nilielekea kwenye duka moja kubwa lilikuwa hapo jirani na mara nyingi tulikuwa tukinunua hapo bidhaa mbalimbali ikiwemo soda,nilipofika nilichomoa noti ya elfu 10 nikamwambia yule maza anipazie Coca baridi,bila tatizo yule Maza aliikamata ile hela akaitia kwenye droo kisha akafungua friji akanipatia soda niliyoiomba!.

Maza "Umughaka utafata chenji bhana sina chenji asubuhi hii"

Mimi "Haina tatizo"

Baada ya kuichukua ile hela nilifurahi kimoyo moyo huku nikijisemea siku zote jamaa alikuwa wapi!.Basi nilihakikisha siku ile zile noti mbili zilizokuwa mfukoni ninahakikisha nazimaliza na ndivyo ilivyokuwa!.

Ile kazi kiukweli niliifanya bila mtu yeyote kushitukia kabisa,sasa kuna muda nilikuwa namkamata mwana yeyote pale kijiweni nampiga liteni namwambia akanunue soda,moja yangu na moja yake,bila kujua unakuta muhuni anafurahi anaenda kununua huku akikimbia!.Uzuri wa pale kijiweni tulikuwa tukiishi kama ndugu,hivyo ukimpatia muhuni hela akanunue eidha soda au fegi anaona unamjali kinoma.

Kiukweli ndani ya mwezi mmoja baada ya kuifanya ile kazi maisha yangu nayo yalianza kubadilika,niliamua kuhama kwenye kile chumba nilichokuwa nina kaa mara ya kwanza ambacho nilikuwa nalipia elfu 15 kwa mwezi,nikaamua kwenda kupanga chumba na sebule,ambavyo nilikuwa nalipia elfu 50 kwa vyote viwili!.

Kazi ile ilikuwa tamu sana na nzuri na ule ukonda kiukweli nilikuwa nazugia tu!.

Ndani kwangu kulianza kubadilika baada ya kununua makochi ya kawaida,nilinunua kapeti nikatandika chini,baadae pia nikanunua subwoofer na TV,nilihakikisha najijenga na kujipanga kama kijana.

Baada ya pesa kunizidi nilianza kujichanganya na wanangu tukawa watu wa viwanja vya starehe pale Sirari,ule mji japo ulikuwa ni mdogo lakini ulikuwa na vistarehe uchwara vilivyokonga nyoyo!.Kipindi hicho ndipo sasa na mimi nikajifunza kunywa pombe huku bia yangu pendwa ikiwa ndovu lager!.Baada kupiga kazi ile ya magumashi kwa miezi 3,jamaa aliniambia mzigo umeisha na ataondoka kwenda Arusha na haitochukua mwezi atakuwa amerudi ili tuendeleze libeneke.
Mauti huanza na furaha!!!!
 
Back
Top Bottom