Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Hahaha me pia nimesoma Kibumaye shule ya msingi pale mwl tata bhokano [emoji23][emoji23][emoji23]
Tuliishi opposite na kwa Juhudi
Daaa! basi wewe utakuwa tunajuana sema tu mlikuwa bado wadogo wadogo sana nyie! hapo kwa juhudi nilikuwa napita kila siku kwenda kirigiri Chekechea zamani zile, kindergarten ilikuwa palee RC, Opposite na kwa chacha Masero!

Vijana wa juhudi wale wadogo nimesoma nao, lkn kuna mwingine hapo hapo!Mwita Matinyi pst huyu ndo jilani na juhudi bial maarifa ! then karibu na kwa juhudi pia kuna Mwalimu Ghikaro!

daa! jamaa big up sana yule! alitupigisha chipukizi huyu bwana hatare nilisoma na mwanae mmoja hivi ni Daktari palee Kampala Univ.!

Kibumaye shule yangu bana nsito isahau ile! daa! niwe na hela nisiwe nazo Lazima nikatoe Donation one day nitafanya ukarabati si wa kawaida na madawati mapyaa mazuri, vitabu nk, km waalimu wangu wako hai napiga donee mwana!

Hasa kuna, Mwl mmoja alikuwa anaitwa Shadrack Gimakwi, Rebecca Marwa, daa mwanangu km hawa hawajafa lazima nitoe ng'ombe kumi! kumi! bila hawa nisingekuwepo hapa!..asa fanya! fanya one day twende Mkuu!

Rafiki zangu wengi sana kule nikifikaga palee Tarime mjini wala siaptagi taabu! wakiniona tu....haoooo! tata nyarusare! yeke muraaa! agha taisalama muyoo?..lkn sipandishagi bana ajili ya muda!
 
Mnafanya biashara za haramu halafu hamna codes za mawasiliano??!! Criminal gang lazima iwe na code hata kama ameshikwa na polisi akianza kuongea tu kwenye simu mwenzake lazima ajue kuwa hali sio hali au unatoa muda feki wa kufika eneo la tukio then unafika mapema sana kucheki mazingira ukiona hali haieleweki unapotea tu.
Wewe unashangaà hilo tu, je hilo la kuweka maburungutu ya hela feki chumbani unapolala..!
Hamna mhalifu professional anafanya huu ujinga
 
Wewe unashangaà hilo tu, je hilo la kuweka maburungutu ya hela feki chumbani unapolala..!
Hamna mhalifu professional anafanya huu ujinga
Ila kibongo bongo sishangai maaana huku wengi wamekimbia umande so wanafanya uhalifu kiholela mwisho wa siku wanafanikiwa mission ila baada ya siku moja wote wanakuwa wamekamatwa na polisi
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 16.



Shemeji yangu kiukweli alikuwa na pesa isiyokuwa ya kawaida,hakuwa tajiri sana kiasi ambacho kingemuingiza miongoni mwa matajiri wa pale Mwanza, lakini alikuwa na uwezo na utajiri wa size ya kati!,nyumba aliyokuwa anakaa yeye na mkewe(dada Sarah)ilikuwa ya kwake ambayo aliijenga kwa fedha yake mwenyewe,pia alikuwa akimiliki gari aina ya Nissan Patrol Nyeusi.

Pia alikuwa ni mtu fulani aliyekuwa na viprinsipo vyake ambavyo kama ulikuwa hujamuelewa ungeona kama ni mateso kuishi nae,pesa yake mpaka ifikie hatua umeila basi ilikupasa umenyeke sana na jasho likutoke ki kweli kweli!.Hivyo hata wakati ananipeleka pale mwaloni na kumwambia yule bwana kwamba ningekuwa miongoni mwa wavuvi,nilikuja kumuelewa baadae maana mwanzo nilidhani kama alikuwa akinishushia heshima na kunidharau!.

Kwakuwa tulifika hapo Ijinga mida ya saa 10 jioni,yeye bwana shemeji baada ya kuwapa maelekezo wale jamaa na kuwaachia alicho waachia,aliondoka akatuacha.Sasa nilipouliza jamaa ameenda wapi yule jamaa aliyenipokea akadai anaelekea kwenye miradi yake mingine ambayo hata sikuifahamu!.

Wakati nimefika hapo sikufahamu kumbe kuna eneo jamaa walikuwa wakiendelea na mapishi bhana,sasa jamaa niliyekabidhiwa kwake alinichukua akanitaka tusogee pembeni kidogo ambako kulikuwa na kibanda cha mabanzi na nyasi,nilipofika hapo nikakuta kundi la watu 7 wakiwa na miili iliyokuwa imejengeka vizuri kimisuli!,jamaa walikuwa wamevaa bukta tu huku vifua vikiwa wazi.Mimi pamoja na kakitambi kangu kalikokuwa kameanza kuchomoza kwa ajili ya beer na fedha haramu,nilijiona kwa wale jamaa siyo kitu kabisa kwa namna walivyokuwa wamejazia misuli!.Jamaa mmoja wapo kwenye wale watu nilisikia anamwambia yule jamaa niliyekuwa nae ya kwamba "Waukae angalia usije ukalala njaa!".Kumbe yule jamaa niliyekuwa nae hilo ndilo lilikuwa jina lake,sasa sikuelewa kama ndilo alilopewa na wazazi wake au lilikuwa jina tu alilopewa na wale jamaa!.

Waukae "Aisee kazi mpya hii!"

Jamaa 1 "Ooh karibu mwanangu,huku ndiko nyumbani kwetu!"

Jamaa 2 "Town tulishakusahau,makazi yetu ni pamoja na samaki mwanangu!"

Wakati huo walikuwa wamekaa wamezunguka sufuria kubwa lililokuwa limefunikwa kwenye sinia kichwa chini miguu juu!,kuna jamaa mmoja alinyanyuka akaelekea ndani kwenye kile kinyumba akatoka na samaki 3 wakubwa ambao walikuwa kambale,samaki wale walikuwa wa kuchoma!,kumbe wao walishindwa kula muda ule walikuwa wakipiga stori wakimsubiri huyo Waukae.Jumla yetu pale ikafanya tukawa watu 9.

Tukauzunguka ule ugali na ndipo lile sufuria likafunuliwa,aisee sikuwahi kushuhudia ugali wenye ukubwa ule toka nizaliwe,hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kuona ugali uliokuwa mkubwa kwa kiwango kile,wale samaki wakawekwa chini kwenye mfuko na kazi ya kuanza kufukuzana na matonge ikaanza rasmi!,mimi nilikula sana samaki kwakuwa nilikuwa nina hamu nao sana maana wakati nikiwa Sirari chakula changu kikubwa ilikuwa nyama na kichuri!.

Baada ya kushiba nilijisogeza kando nikawaacha jamaa wakiendeleza libeneke!.

Jamaa 1 "Mwanangu mbona unakimbia"

Mimi "Mwanangu niko fiti!"

Jamaa 2 "Huyu hana njaa muda bado!"

Ile kauli ya yule jamaa wa pili sikuielewa kwa wakati ule lakini kwa baadae ilikuwa na maana kubwa sana kwangu!.Niliondoka zangu nikaelekea ziwani kwenda kunawa mikono!..

Walipomaliza kula ugali ambao haukubaki hata punje,ndipo kila mtu alinyanyuka na kuendelea na mambo yake,mimi niliendelea kushangaa kwa kuwa ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ziwani kabisa na kusogelea maji ya ziwani,mara zote nimekuwa nikiliangalia lile Ziwa Victoria kwa mbali tu na sikuwahi kabisa kulisogelea kwa karibu hadi kuyagusa maji yake!.

Ilipofika mida ya saa 12 jioni niliona wale jamaa wakianza kubeba nyavu pamoja na makarabai na kupelekea kwenye ile mitumbwi,zoezi lile lilifanyika kwa haraka na ndipo wengine wakawa wanavaa masweta na nguo za kazi,kuna jamaa wengine wao walibaki kama walivyokuwa tu hapo awali!. Baada ya muda giza nalo likaanza kutanda,ndipo Waukae akawa ameniambia nivue suruali nibaki na bukta pamoja na tisheti kisha nizame kwenye mtumbwi!. Sasa kumbe ile mitumbwi mingine niliyoiona ilikuwa ya watu wengine,wale jamaa tuliokuwa tunakula nao pale,waliokuwa wafanyakazi wa shemeji walikuwa 4,hivyo ukiniweka mimi pamoja na Waukae tulikuwa jumla 6,wale wengine walikuwa wa mitumbwi mingine!.

Tuligawana watu watatu kwa kila mtumbwi na kisha ikawashwa tukaondoka!.Hakuna siku ambayo sitokuja kuisahau kama hiyo maana ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kupanda mtumbwi pia ilikuwa siku ya kwanza kusafiri ziwani,muda huo kiukweli ziwa lilikuwa limetulia sana na hakukuwa na mawimbi.Baada ya mwendo mrefu kuelekea katikati ya ziwa Victoria,nilikuwa nikigeuka nyuma naziona taa za pale kijijini mwaloni kwa mbali sana,pia kwa umbali ule ilifanya tukawa tunaona mianga ya taa kutoka vijiji vingine vilivyokuwa kando ya ziwa!.Baada ya kufika walipoona panafaa kushusha nyavu,zile boti zilizimwa injini,kulikuwa na utulivu wa hali ya juu sana wakati huo,mawazo yangu yalikuwa yanakwenda mbali zaidi na kujikuta nawaza endapo tukizama itakuwaje,lakini kwa upande wa wale jamaa wao hawakuwa na hofu kabisa!.

Zile nyavu zikaanza kushushwa taratibu kutoka kwenye ile boti yetu,nyavu zilipokwisha kushushwa zote,ndipo nilimuona Waukae anachukua kopo moja kubwa la Toss(ambalo lilikwisha sabuni) lilikuwa na maji ndani yake akalifungua kisha akawa anachota yale maji kwa mkono kisha anayatupa ziwani huku akinuia jambo fulani!,sasa kwakuwa nilikuwa mtu mzima niligundua ya kwamba ile ilikuwa ni dawa na alichokuwa kuwa anafanya ni kama vile walipewa masharti na mganga,lile jambo lilikuwa likifanyika siku zote ambazo nilikuwa hapo Mwaloni na ilikuwa ni lazima lifanyike!.Na hata ule mtumbwi mwingine pia lilifanyika jambo hilo!.

Baada ya hapo tulitulia humo ndani ya mitumbwi hadi mida ya saa 10 usiku,sasa mimi nilifahamu ya kwamba tukishatupa zile nyavu tungerudi mwaloni hadi kesho yake ndipo kazi ifanyike kumbe haikuwa hivyo!.Ilipofika mida saa 10 usiku ndipo tukaanza kuvuta zile nyavu!,nilichokuja kugundua ni kwamba,wale jamaa hawakujazia ile miili yao misuli kwasababu ya kunyanyua nondo(vyuma vya Gym)bali walijaza kwasababu ya kuvuta zile nyavu!,aisee asikwambie mtu,ingawa kulikuwa kuna baridi na hali ya hewa isiyokuwa ya joto lakini mimi nilichuruzika jasho kama nilikuwa nakimbizwa!.

Mahala popote ukiwa unawaona wavuvi nakuomba wapigie saluti,ile kazi haikuwa ya kitoto kama watu wazaniavyo!.

Basi baada ya kuvuta zile nyavu kwa muda,ndipo na samaki nao waliokuwa wamenaswa na zile nyavu wakaanza kujitikisa na kurukaruka!,kwa upande wangu niliendelea kushangaa sana kwasababu ilikuwa ni kitu kipya!.Hiyo siku tulipata samaki wengi sana na kitu ambacho niliendelea kukishangaa sana ni kitendo cha kumvua samaki aina ya Sangara mwenye ukubwa na kimo kama cha mtoto wa miaka 6.Niliuliza nikaambiwa huyo ni cha mtoto,kuna siku huvuliwa Sangara mwenye kimo cha mtu mzima ingawaje huwa ni mara chache lakini hutokeaga!.

Ilipofika mida ya saa 12 asubuhi baada ya kuifanya ile kazi kwa muda mrefu,mashine ziliwashwa na kurudi mwaloni huku tukiwa na rundo la samaki wakubwa na wadogo!.Tulipofika Mwaloni tulikuta kulikuwa na gari kubwa ambalo lilikuwa rasmi kwa ajili ya kubeba na kuhifadhi samaki!.Haukupita muda nikawa nimemuona na shemeji pia!.

Tuliwashusha wale samaki kwenye chombo kisha wakawa wanapimwa uzito,waliokuwa wakubwa wa size iliyotakiwa waliipakiwa kwenye ile gari,na waliobaki waliwekwa kwenye madumu kisha kuna land-rover lilikuja kuwachukua!.

Baada ya kuifanya ile kazi kwa muda wa mwezi mmoja nikaanza kuizoea,sasa kuna siku nikawa napiga mastori na Waukae ambaye tayari alishakuwa mtu wangu wa karibu sana!.Wao ilipofika mwisho wa Mwezi walikuwa wakilipwa kwa makubaliano walioyafahamu wao,lakini mimi sikulipwa chochote,sasa nikafahamu uenda shemeji atakuwa anampatia Dada pesa yangu anihifadhie,uenda alidhani angenipatia ningeitumia katika ulevi na uzinzi uliokuwa umekithiri pale kisiwani,kilichokuwa kinanisaidia ilikuwa ni ile hela yangu ambayo bado nilikuwa nayo.

Waukae "Unadhani bila vile utapata samaki!?"

Aliendelea "Utarudi na mitumbwi ikiwa inakukodolea macho!"

Mimi "Kwahiyo ni kila mtu mwenye mtumbwi anafanya?"

Waukae "Ni ujanja wako tu,wapo ambao wanamtegemea Mungu lakini huwa hawasaidii wanaishia kupata hasara na kuuza injini!"

Mimi "Kwani Injini inauzwaje!"

Waukae "Injini ipi sasa,maana kuna hiyo Yamaha na Honda!"

Mimi "Kwani zinatofautiana bei!?"

Waukae "Hiyo Yamaha ina bei yake na Honda pia ina bei yake"

Mimi "Nzuri ni ipi kaka?"

Waukae "Yamaha ina sipidi ila Honda ina nguvu na hata bei yake imesimama"

Ile mitumbwi ya shemeji yeye alikuwa amefunga injini za Honda,lakini mitumbwi karibia mingi ilikuwa na injini za Yamaha!.

Waukae "Yaani hapa bila dawa unadhani unatoboa!"

Aliendelea "Hivi Masangara ni shemeji yako kabisa eti!"

Mimi "Masangara ndiyo nani?"

Baada ya kuuliza Masangara ndiyo nani yule jamaa akaanza kucheka sana kana!.

Waukae "Sisi tunamjua kwa jina la Masangara"

Mimi "Ni shemeji yangu ila hilo jina sikuwahi kulifahamu"

Waukae "Huku watu wanamjua kwa jina hilo"

Waukae alikuwa ni msukuma bila hata kuuliza kwasababu ongea yake na rafudhi yake vilitosha kukuaminisha pasipo shaka!.

Baada tena ya kupiga kazi kwa mwezi mmoja uliofuata wenzangu wakalipwa hela nzuri tu lakini kwangu ikawa hola!.Sikuelewa sababu za shemeji kutokunilipa ilikuwa ni nini wakati nilikuwa nafanya kazi sawa na akina waukae!.

Niliamua kuweka vocha kwenye kiswanswadu changu na kumpigia Dada Sarah na kujifanya namsalimia ili nione uenda angeniambia shemeji huwa anamuachia hela yangu!,baada ya mazungumzo nikaona yuko kimya sikutaka kumuuliza maana niliona nikimuuliza na akajua kumbe mumewe anipatii chochote ingeleta shida katika mahusiano yao,ingeonekana nimekwenda pale kuwachonganisha,hivyo nikaamua kukaa kimya!.
Ndani ya mwezi huo nilipokuwa nimejifunza na kuielewa ile kazi na namna ilivyokuwa inapesa ndefu,niliamua kumpigia simu Mwanangu Mtatiro.
Ugali kama huu?
JamiiForums-1308624164.jpg
 
Wewe unashangaà hilo tu, je hilo la kuweka maburungutu ya hela feki chumbani unapolala..!
Hamna mhalifu professional anafanya huu ujinga

Wahalifu wa kiafrika anaua anatupa line ya voda, anasajili airtel kwa kitambulisho chake halisi, halafu anatumia simu ileile aliyofanyia uhalifu, au anafanya uhalifu sehemu anajulikana kama john anakimbia na kule alikokimbilia anajitambulisha kama john.

Au anajua kabisa ana vitu haramu halafu anaviweka karibu yaani ndani anapolala au polisi wanatumia honeytape anapigiwa simu na mwanamke hadi anashawishiwa aende sehemu waonane nae anaenda kama kuku, au anajua ana majanga anatembea hovyo kama kuku wa kienyeji au anapigiwa simu anaulizwa uko wapi namba ngeni anataja sehemu halisi alipo kabisa au dili haramu anapangia kwenye simu wakati simu inatakiwa kutumika kuonana tu dili inapangwa face to face tena kwa codes maalumu.

Au mtu anafanya uhalifu eti anaenda kuvuka border kwa kutumia passport yake halali inayotambulika kabisa kuna vituko ambavyo ushahidi wahalifu wanauacha wanadakwa kizembe sana
 
Daaa! basi wewe utakuwa tunajuana sema tu mlikuwa bado wadogo wadogo sana nyie! hapo kwa juhudi nilikuwa napita kila siku kwenda kirigiri Chekechea zamani zile, kindergarten ilikuwa palee RC, Opposite na kwa chacha Masero!

Vijana wa juhudi wale wadogo nimesoma nao, lkn kuna mwingine hapo hapo!Mwita Matinyi pst huyu ndo jilani na juhudi bial maarifa ! then karibu na kwa juhudi pia kuna Mwalimu Ghikaro!

daa! jamaa big up sana yule! alitupigisha chipukizi huyu bwana hatare nilisoma na mwanae mmoja hivi ni Daktari palee Kampala Univ.!

Kibumaye shule yangu bana nsito isahau ile! daa! niwe na hela nisiwe nazo Lazima nikatoe Donation one day nitafanya ukarabati si wa kawaida na madawati mapyaa mazuri, vitabu nk, km waalimu wangu wako hai napiga donee mwana!

Hasa kuna, Mwl mmoja alikuwa anaitwa Shadrack Gimakwi, Rebecca Marwa, daa mwanangu km hawa hawajafa lazima nitoe ng'ombe kumi! kumi! bila hawa nisingekuwepo hapa!..asa fanya! fanya one day twende Mkuu!

Rafiki zangu wengi sana kule nikifikaga palee Tarime mjini wala siaptagi taabu! wakiniona tu....haoooo! tata nyarusare! yeke muraaa! agha taisalama muyoo?..lkn sipandishagi bana ajili ya muda!
Hilo jina la Nyarusare umelichukua kutoka kwa yule Mzee Nyarusare msanii alikuwa mwana-ccm kindakindaki na anapiga sana zeze? Nakumbuka kuna sikukuu moja ya May Mosi alipiga wimbo unaitwa kazi ni kazi. Pamoja na kwamba nilikuwa mdogo lakini mpaka sasa kumbukumbu ipo
 
Hilo jina la Nyarusare umelichukua kutoka kwa yule Mzee Nyarusare msanii alikuwa mwana-ccm kindakindaki na anapiga sana zeze? Nakumbuka kuna sikukuu moja ya May Mosi alipiga wimbo unaitwa kazi ni kazi. Pamoja na kwamba nilikuwa mdogo lakini mpaka sasa kumbukumbu ipo
Nadhani yule dingi alikuwa akiitwa Nyarusahi, alituburudisha sana enzi hizo hasa kukiwa na sikukuu za kitaifa pale ulipokuwa uwanja wa sabasaba

Hii nyarusare nahisi inasadifu kitu kingine ila ngoja ninyamaze
 
Duuh mkuu umughaka ubarikiwe, Kuna baadhi ya maneno yamekopwa kwenye kabila la kipogoro mfano neno waukaye ni neno la kipogoro likomaanisha mtu wa nyumbani au wa Kijiji au mji mmoJa, neno lingine ni longa mpaka kukuche maana ya longa ni ongea, mi mpogoro wa itete kishenzi na nimefurahi maneno ya kipogoro yanatumika japo kidogo
 
Back
Top Bottom