Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 25.



"Wewe ni mtu muhimu sana kwangu Mtatiro na umekuwa sehemu ya furaha katika maisha yangu,ulinipokea na kunisaidia wakati mzee aliponitimua nyumbani,hukuniacha katika matatizo bali ulinishika mkono kama kijana mwenzio hivyo na mimi sitokuacha rafiki yangu" ni maneno niliyokuwa nikimwambia rafiki yangu wa damu Mtatiro ili aendelee kuwa na amani kabisa.

USHAURI

Kuishi na Virusi vya Ukimwi si mwisho wa maisha na uhai,kama kuna kitu nakichukia katika maisha yangu ni ubaguzi unaofanywa kwa hawa ndugu zangu,haya ni maisha tu na tunapaswa kupendana,unaweza ukawa muaminifu na bado mumeo/mkeo akakuletea ugonjwa,hivyo hatupaswi kuwanyooshea wengine vidole kana kwamba ni wadhambi kuliko sisi,tuache dharau za kijuaji na kebehi zisizo na msingi.

Ndugu zangu pia niwaombe mzingatie dawa kwa wakati ili ziweze kuwafubaza virusi angalau unapokutana na mwenzako usimuambikize ili muendelee kufurahia maisha,jambo la msingi ni wewe mwenyewe kuacha kujibagua,jikubali na songa mbele.Acha starehe za kijinga,panga mipango yako na timiza ndoto zako,usiwe mlevi kupita kiasi na hakuna sababu ya kuwaambukiza wengine kwa makusudi,wapende watu wote.Pia achana na imani za mitume na manabii kwamba wakupatie maji au mafuta utumie kisha uache dawa,achana kabisa na hizo imani mfu,wewe muombe Mungu atakusikia,kama akipenda anaweza kuuondoa huo ugonjwa na kama akiona inafaa wewe kuendelea nao basi Mshukuru na endelea kuishi,hata kama ukimuomba Mungu na ugonjwa usitoke lakini Mungu bado atabaki kuwa mwema hivyo usikate tamaa.

NAWAPENDA SANA



Basi baada ya afya ya rafiki yangu kipenzi Mtatiro kuimalika tuliendelea na kazi yetu ya kuuza mitumba sehemu na vijiji mbalimbali vya kanda ya ziwa.Nakumbuka siku moja Gabi alimpigia simu Mtatiro akawa amemuambia inapaswa tuonane ili tupange mikakati ya kuelekea maeneo kama kawa.Kweli,tuliondoka siku iliyofuata kuelekea kule yalipokuwa makazi ya muda ilipokuwa inasukwa mipango kabla.Tulipofika pale ndani tulimkuta Gabi kama kawaida akiwepo Jipe na jamaa yule dereva tuliyeenda nae kwenye tukio kahama.

Jipe "Wanangu mko poa"

Mtatiro "Tuko fiti kaka"

Jipe "Sasa Kesho safari ni Kagera"

Aliendelea "Si mko vizuri?"

Mtatiro "Sisi tuko tayari hata leo kaka ni nyinyi tu!"

Jipe "Sawa,Gabriel atatangulia leo halafu sisi kesho jioni tutaondoka"

Basi baada ya yale mazungumzo Jipe akatutaka tujitayarishe kwa ajili ya safari kesho yake.Mimi na Mtatiro tuliamua kurudi nyumbani huku Mtatiro akiapa na kusema safari hii wakijidai kutudhurumu basi ama zake ama zao!.

Siku iliyofuata mida ya saa 7 mchana tulikuwa tushafika eneo la tukio na ndipo tukakamata Noah na kuianza safari ya kuelekea mkoa wa Kagera,kwenye gari nilikuwa mimi na Mtatiro wakati huo jipe akiwa amekaa kwa mbele pamoja na yule jamaa dereva!.Tuliingia Kagera mida ya saa 12 asubuhi siku iliyofuata,njia tuliyotumia ni ileile ya kupitia Kahama huku tukiwa makini kupita maelekezo,Jipe alikuwa ametoa maelekezo ya kwamba,yeyote atakaye jiingiza mkenge basi ingekuwa ni halali yetu!.Baada ya kufika Kagera,Jipe aliwasiliana na Gabi ambaye alimuelekeza maeneo ambayo tungemkuta,nakumbuka tuliikamata njia na uelekeo wa Bukoba mjini,nje kidogo ya mji tukamkuta Gabi.

Gabi "wazee kwa huku itabidi tuzunguke kidogo muda uende kwasababu hatuna makazi,na ikifika mida tutaitana tufanye kilichotuleta".

Kwakuwa mimi na Mtatiro ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kufika Kagera ilibidi tukae kwenye ile gari maana hatukutaka kucheza mbali tukajichanganya na ukizangatia hatukuwa na simu!.Dereva alitafuta maeneo ambayo hayakuwa na shughuli nyingi za watu akapaki gari hapo.

Ilipofika mida ya saa 10 jioni mvua ikaanza kunyesha kama masikhara lakini muda ulipozidi ndipo hali ilizidi kuwa mbaya,tangu nizaliwe sijawahi kuona radi zikipiga kama siku hiyo,ile mvua ilikuwa na radi si mchezo hadi uoga ukawa unaniingia!.Kadiri muda ulivyozidi ndivyo mvua nayo ilizidi kuongeza spidi na nilikuwa naona Jipe anaomba iendelee kunyesha vilevile isikatike.Sasa ikafika mida ya saa 12 ikapungua ikawa inanyesha kidogo sana,tulikuwa ndani ya gari wakati huo tukiendelea kuvuta muda.Ilipofika mida ya saa 3 usiku mvua ikaanza tena kunyesha kama mwanzo.

Jipe "Huu ni muda sasa"

Aliendelea "Aisee wewe utaenda kutusubiri mahali nitakapokuelekeza"

Jipe "Wengine wote tutaongozana na mtafanya kila nitakachowaambia"

Basi ile gari ikaanza kuondoka kuelekea uelekeo wa Bukoba Mjini,kuna mahali tulifika ambapo kwa umbali kama wa mita 500 kulikuwa na sheli(sitoitaja),dereva alitakiwa kuzima taa na kugeuza gari atusubiri hapo!.Kila mmoja alikuwa tayari kwa ajili ya makabiliano.Muda huo ilikuwa ni saa 4 usiku lakini kulikuwa na mvua kubwa sana,tulipofika kwenye ile sheli baada ya Jipe kuchomoa SMG kuna mlinzi alimuona akaanza kukimbia kama mwehu huku akiwa na gobole,Jipe hakutaka kumpotezea muda,alipiga risasi ya mgongoni yule mlinzi akawa amedondoka chini.

Jipe "Mtatiro kusanya hao wauza mafuta wote"

Jipe aliingia ndani kwenye vyumba vilivyokuwa kando ya ile sheli huku akiniambia niongozane nae.Pale nje Mtatiro na Gabi waliendelea kuwadhibiti wale wauza mafuta na kuchukua hela huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Jipe "Toa pesa wewe la sivyo nitakuua"

Jipe alikuwa akimwambia dada mmoja kibonge ambaye tulimkuta mle ndani wakati huo akimnyooshea mtutu wa bunduki.Yule dada alifungua boksi moja lilikuwa la mbao na kulikuwa na noti za kutosha,sasa kulibeba lile boksi mwenyewe kidogo likawa zito,Jipe akamuamuru yule demu atupatie mfuko,yule demu alitoa mfuko mmoja ambao ulikuwa kama shuka ambao ulikuwa umechakazwa na rangi ya maoili!,niliukamata ule mfuko haraka nikaanza kuchukua zile hela haraka sana,sikutaka kabisa kuhangaika na silva maana jipe alisema nitemane nazo,baada kumaliza zile hela,Jipe alimuamuru yule demu alale chini na asijaribu kuinua kichwa kwani atamuua,tuliondoka chap mle ndani kuelekea nje ambapo tuliwakuta Gabi na Mtatiro wakiwa wanatusubiri!.

Tulikimbilia gari na tulipofika dereva aliondoka kwa spidi kali sana lile eneo,wakati huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha sana.Wakati tupo njiani,Jipe alimpigia simu yule demu Kamange na kumtaka achukue ile gari Mark 2 atukute Geita.Ile Noah ilitembea vibaya mno usiku huo na tulifanikiwa kufika Geita mida ya saa 8 Usiku,Jipe akawa amemwambia Gabriel na dereva ya kwamba wao watangulie Mwanza halafu sisi tungeisubiri ile Mark 2.

Kweli,Kesho yake mida ya saa 4 asubuhi yule demu akawa amefika pale Geita kutuchukua tukawa tumeondoka,Tuliingia Mwanza mida ya saa 11 jioni.Tuliwakuta kina Gabi wao wameshafika,sasa tulipofika Mtatiro alimwambia Jipe ya kwamba pesa tulizopora ziletwe zihesabiwe ili kila mtu afe na chake,nadhani wao walidhani Mtatiro anatania lakini jamaa alikuwa serious sana,sikuwahi kufahamu kama Mtatiro akikasirika anakuwa vile aisee,mara zote mimi nimekuwa nikimuona akiwa kawaida nikawa namchukulia poa,siku hiyo ndiyo niliiona rangi halisi ya yule mkurya.

Mtatiro "Haiwezekani tupore pesa halafu nyie muwe mnagawana nyingi na sisi mnatupa kidogo,mkitaka damu leo imwagike ficheni hizo hela muone!"

Jipe "Hakuna atakayedhurumiwa hata mmoja"

Mtatiro "Mbona juzi mmetunyenga?"

Jipe "Yale yalikuwa ni maelekezo ya bosi"

Mtatiro "Basi mwambieni leo kila mtu anapata pasu,sitaki ufara!"

Baada ya jamaa kuona Mtatiro yuko serious,Jipe alimwambia Gabi walete zile pesa ili kila mmoja apewe haki yake.Kweli,mimi na Mtatiro kila mmoja alipata mioni 6,na wao pia walipata kama sisi.Tuliamua kuondoka zetu baada ya kupokea mgao wetu.

Mtatiro "Mwanangu kama ni hela ya mtaji tushapata,tuachane na hizi habari wao kama wanaendelea ngoja waendelee"

Aliendelea "Cha kufanya tukafungue duka la jumla tuachane na mitumba"

Mtatiro "Au wewe unaonaje mwanangu?"

Mimi "Kwanini tusifungue duka la vipodozi?"

Mtatiro "Eti eeeh,sawa?"

Baada ya kupata ile hela kweli tuliachana na biashara ya mitumba na tukafungua duka la vipodozi yale yale maeneo ya Usagara tukaanza kupambana,nakumbuka Mtatiro alikuwaga anafuata vipodozi Uganda kwasababu huko ndiko vilikuwa vinapatikana kwa bei ya chini,kiukweli tulipiga sana hela na maisha yetu yalianza kubadilika mdogo mdogo,ilifika sehemu tukahama pale kwa braza ake Mtatiro kila mmoja akaenda kupanga geto lake mwenyewe.

Nakumbuka siku moja Mtatiro akaja kuniambia kwamba Gabi anampigia simi twende kuna mchongo wenye hela kubwa tukapige.

Mimi "Umemwambiaje!"

Mtatiro "Mi nimemwambia kwasasa tunashughuli zetu,wao kama wanaendelea waendelee!"

Aliendelea "Jamaa baada ya kumwambia ananiambia kwamba tunataka kuwachoma,hivyo tujiangalie tutaumia"

Mimi "Sasa itakuwaje?"

Mtatiro "wale hawawezi kututisha we tulia"

Basi baada ya jamaa kuona hatuwapi tena ushirikiano wakaamua kutokutushirikisha kwenye michongo yao tena lakini walikuwa wamechukia sana baada ya sisi kuachana nao.Baada ya miezi kadhaa kupita,kuna siku Mtatiro akaja kuniambia amesikia habari mahali kuna majambazi wamedakwa wengine wameuawa huko Mbeya na mmoja wapo wa waliodakwa ni Gabi,sasa baada ya kuifatilia ile habari ni kweli kabisa ilikuwa Jipe na majambazi kadhaa wenzie waliuawa palepale eneo la tukio.

Kumbe walienda kumpora mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya India ambaye ndani ya gari alikuwa na madini pamoja na pesa alizokuwa akizitoa huko Chunya kuelekea Mbeya,sasa wao hawakujua yule mfanyabiashara alikuwa na eskoti ya askari kadhaa,yawezekana walijua hilo ila wakajifanya wabishi kwakuwa walikuwa na silaha.Walikufa majambazi wawili na mmoja akiwa Jipe huku Gabi na mwingine mmoja wakisalimu amri.

Gabi alifungwa miaka the thelathini gerezani na mwaka juzi nimetoka kumuona pale gereza la Ruanda Mbeya.Jamaa amechoka sana na aliponiona mara ya kwanza alionyesha huzuni lakini hakuwa na namna ndo hivyo ishatokea.Aliniambia yule aliyekuwa bosi wake alikimbilia huko Kenya kuanzisha maisha huko.Huwa namtembelea jamaa nikipata nafasi,na siachi kumtia moyo na kumfariji,namwambia ashukuru akufa,maadam yuko hai basi atatoka tu gerezani na ataendelea na maisha yake ingawaje atakuwa amepoteza muda.

Mimi na Mtatiro lile duka la vipodozi tuliuza na kila mmoja akaendelea na biashara zake,Mtatiro aliondoka kwenda Uganda kwa anko wake hadi leo anaishi huko.Mimi niliamua kurudi Tarime Sirari nikafungua duka nikaanza kukimbiza,kuna mtoto wa dingi mkubwa anaishi Dar es salaam alikuwa anafanya biashara ya vyombo akaniambia nije tuungane tufanye biashara kwa kua inalipa sana,hivyo nikaondoka Tarime kuja Dar,kufika nikampatia jamaa zaidi ya milioni 9 akanidhurumu hadi leo,niliamua kumuachia Mungu nikaanza kupambana upya kutafuta mtaji,nilipopata mtaji nikanunua bodaboda yangu ambayo ndiyo inaniingizia kipato kwa hapa mjini.


Nawapenda sana.


MWISHO.
Mkuu mlikuwa mnapata taarifa kupitia vyanzo gani kujua kama sehemu fulani kuna pesa na nyie kwenda kuvamia au mlikuwa mna bahatisha?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
My MCE (man crush everyday ) ni UMUGHAKA
Tena wewe ni JF man of the year kwa maoni yangu. Wanaume wengi wanaposimulia simulizi kama hizi mara nyingi huwa wanasusa kutokana na kelele na kukatishwa tamaa na wana JF wenye mdomo ila wewe umekaza hasa hadi umemaliza.

Wewe ni kidume na nusu.
Shukrani sana UMUGHAKA
 
My MCE (man crush everyday ) ni UMUGHAKA
Tena wewe ni JF man of the year kwa maoni yangu. Wanaume wengi wanaposimulia simulizi kama hizi mara nyingi huwa wanasusa kutokana na kelele na kukatishwa tamaa na wana JF wenye mdomo ila wewe umekaza hasa hadi umemaliza. Wewe ni kidume na nusu.
Shukrani sana UMUGHAKA
Nakadori kama Nakadori
 
My MCE (man crush everyday ) ni UMUGHAKA
Tena wewe ni JF man of the year kwa maoni yangu. Wanaume wengi wanaposimulia simulizi kama hizi mara nyingi huwa wanasusa kutokana na kelele na kukatishwa tamaa na wana JF wenye mdomo ila wewe umekaza hasa hadi umemaliza. Wewe ni kidume na nusu.
Shukrani sana UMUGHAKA
Usiku anapandisha ya mabinti wa kitanga walivyosababisha apate zero form 6.
Papuchi zilivyomnogea.
Angalizo:iwe Ni usiku kwa usiku kwa above 18 tu.
 
My MCE (man crush everyday ) ni UMUGHAKA
Tena wewe ni JF man of the year kwa maoni yangu. Wanaume wengi wanaposimulia simulizi kama hizi mara nyingi huwa wanasusa kutokana na kelele na kukatishwa tamaa na wana JF wenye mdomo ila wewe umekaza hasa hadi umemaliza. Wewe ni kidume na nusu.
Shukrani sana UMUGHAKA
Mwaga sifa Mama ..

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Yani imenibidi nirudie kuisoma story toka episode ya mwanzo kubaini ni wapi Mwamba Mtatiro alipiga mbususu yenye viwatirifu aiseeeee nimegundua ni pale alipo kula mbususu mbele ya Umughaka!


Sasa nafikiri kile kitendo cha Mtatiro kula Mbususu mbele ya Umughaka kili mkasirisha Mungu hivyo Matatiro akauvagaa....aiseee ile siku kuna namna mateso ya Umughaka aliyoyapata wakati Mtatiro anaichakata Papuchi yalizaa laana(jokes....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23])

Daaa mwamba Mtatiro ni jasiri sana hadi alikataa kutumia dawa akijua ata survive tuu hatari sana sasa sijui ataendelea kupambana au Umughaka atabaki mwenyewe?


Aiseee Umughaka umetisha sana sana,,,,, sikuwai kutekwa na stori namna hiii
Mbususu yenye viwatilifu.

Aisee.

Hii ya leo mpya.😁😁😁🤣🤣
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 13.

Mimi "Mama nyakuru Mwita"

Mama "Tata sabhoke"

Ilikuwa ni heshima na salamu ambayo nilimpatia mama yangu baada ya kuwa nimefika hapo sokoni kwenye meza aliyokuwa akifanyia biashara!.

Mama "Ulienda wapi baba?"

Mimi "Nilikuwepo tu mama!"

Mama "Mbona umenenepa hivyo,au umepata kibarua huko baba!?"

Mimi "Nabangaiza tu hivyo hivyo!"

Mama "Nilimpigia mama yako mkubwa lakini akaniambia uliondoka na akajua labda ulirudi nyumbani"

Mimi "Mama nilienda kupambana na maisha yangu!".

Mama "Sasa baba utaendelea kuhangaika hivi hadi lini,rudi nyumbani mimi niliongea na baba yako na akasema hayo yameisha"

Mimi "Mama kwa umri huu siwezi kukaa tena pale nyumbani"

Mimi "Nilipita tu kuwasalimia"

Mama "Ulipita nyumbani?"

Mimi "Nimeanzia huko ndiyo nikaja hapa"

Mama "Dada yako alikuja na amemaliza kuondoka wiki iliyopita!"

Aliendelea "Chukua namba yake utawasiliana nae alisema ukirudi nikwambie umtafute"

Basi baada ya mazungumzo na mama nilichukua ile namba ya dada yangu mkubwa(Sarah)kisha nikaondoka zangu!.Mama yangu mara zote alikuwaga rafiki yangu kipenzi,pamoja na lile seke seke la mzee lakini bado alitaka nirudi pale nyumbani kitu ambacho kisingewezekana kwa wakati huo!.Sasa wakati naondoka nilimpigia dada yangu simu ili kumjulia hali maana tangu nilivyokuwa nimemaliza shule sikuwahi kuongea nae kwasababu yeye alikuwa ameolewa huko Mwanza!.

Baada ya kuongea na dada kwa dakika kadhaa alishangaa sana kwa kile kitendo ambacho mzee alinifanyia na alilaumu sana kwanini nilishindwa kumshirikisha kwa muda wote huo nikawa kimya!.

Da'Sarah "Sasa sikuhizi unafanya kazi gani hapo Tarime?"

Sikutaka kabisa kumficha kitu dada nilimwambia niliamua kuwa mpiga debe angalau maisha yaendeleee,alinishangaa sana ya kwamba nawezaje kuwa na elimu halafu niende kupiga debe!.

Da'sarah "Nilimwambia baba ukweli na kama ni kuchukia ngoja achukie,haiwezekani pesa anamalizia kwa mama yake Robina halafu sisi tunahangaika!"

Aliendelea "Kwahiyo sasa ulikuwa unakaa wapi?"

Mimi "Niliamua kupanga hapo Sirari!"

Da'Sarah "Ngoja nimwambie shemeji yako aje akutumie nauli uje huku"

Aliendelea "Na huyo mzee wala usimwambie chochote,muacheni na hela zake,yeye si anaona mama yetu hana maana!"

Mimi "Mimi nishamsahau na wala sihitaji hata kumi yake!"

Mimi " Halafu dada kama huko kuna sehemu ya kufikia hilo suala la nauli kwangu alinisumbui,we hata usimsumbue shem we kama inawezekana hata leo nianze safari"

Da'Sarah " Sasa hivi kweli kuna gari za kutoka hapo kuja Mwanza?"

Mimi "Hilo suala wewe niachie mimi,mimi nikifika nitakwambia"

Da'Sarah " Sawa wewe panda gari uje kama una nauli na ngoja nimpigie shemeji yako simu muda huo!"

Ile kauli ya Dada kunitaka niende Mwanza nikama ilinisaidia maana mpaka wakati huo nilikuwa sielewi hatma yangu!.Basi nilielekea mpaka stendi ambako nilikuwa nikitembea kwa umakini na tahadhari kubwa ili nisije kujikuta naangukia mkoni mwa mapongo,wakati huo begi langu lilikuwa na hela lipo mgongoni sikutaka kabisa kuliachia!.Basi nilipofika pale stendi nilidandia Hiace za Musoma ambako nilipanga nikifika pale Zero zero( Makutano) nisubiri gari zinazoenda Mwanza kutokea Musoma mjini!.Nilifika pale Makutano mida ya saa 9 alasiri na nikatelemka kusubiri gari za Mwanza.

Sikutaka kupandia gari za Mwanza pale Tarime mjini maana kulikuwa na wajuaji wengi hivyo nikawa naogopa kukamatishwa!.Basi haukupita muda nikawa nimepanda gari za Mwanza na nikawasiliana na dada nikawa nimemjulisha nishapanda gari!.,Kiukweli akili yangu mpaka wakati huo ilikuwa inawaza mambo mengi sana,sikujali ya kwamba Sirari nimeacha vitu vyangu wala nini,mimi nilichojali ni usalama wangu na kama ni vitu niliona ningevifata hali ambapo ingetulia!.

Wakati nikiwa kwenye gari nilimtafuta mshikaji wangu Mtatiro ambaye niliamini yupo Mwanza na nilipanga nikifika Mwanza tuonane!.


Mimi "Mwanangu vipi?"

Mtatiro "Mwanangu umekuwa adimu sana kama mate ya nyoka!"

Mimi "Ahahahaa ahahaaa,nambie mwanangu"

Mtatiro "Nimekutafuta juzi kati ulikuwa hupatikani!"

Mimi "Kuna mahali nilikuwepo mtandao ulikuwa haushiki kaka"

Mimi "Nipo njiani mwanangu nakuja M-Z-A"

Mtatiro "Unakuja lini,leo!?"

Mimi "Yeah nipo njiani"

Mtatiro "Umefika wapi?"

Mimi "Tunakaribia Kiabakari"

Mtatiro "Mimi sipo Mwanza mwanangu"

Mimi "Ulirudi Tarime?"

Mtatiro "Hapana,nipo hapa Bunda kuna ki mgodi kimetema ndiyo tupo na brother"

Mimi "Duuu!"

Mtatiro "Mwanza unaenda kwa nani?"

Mimi "Naenda kwa sista Sarah!"

Mtatiro "Mwanangu achana na habari za Mwanza kwanza,we kama vipi telemkia hapo Bunda mimi nitakufata uje tuone kama tutapata chochote"


Mtatiro alinishawishi hadi nikajikuta tena safari ya Mwanza kama imetoweka moyoni mwangu,nilichokuwa namshukuru Mshikaji wangu Mtatiro alikuwaga kila fursa haachi kunishirikisha kama rafiki yake,iwe haramu au iwe halali,kiukweli kwenye hilo sitamsahau jamaa yangu(Kwasasa anaishi Uganda).

Mtatiro "We mwambie Konda akushushe kituo kinaitwa Nyasura"

Aliendelea "Akikushusha hapo Nyasura ndiyo itakuwa jirani na huku nilipo!"

Mimi "Sawa"

Basi safari ikawa inaishia Bunda ingawa nilishalipa nauli ya Mwanza moja kwa moja,sikuona taabu kwasababu bado fungu nilikuwa nalo la kutosha.Ingawaje pesa niliyokuwa nayo ilikuwa haramu lakini ilikuwa inanipa kujiamini kwingi sana!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika pale Bunda na mimi kushushwa hapo Nyasura kama Mtatiro alivyokuwa amenielekeza!.Basi nilimpigia simu Mtatiro nikamueleza ya kwamba nishafika hapo Nyasura,jamaa akawa amenitaka nipumzike sehemu aje kunifuata maana alipokuwepo yeye kulikuwa na umbali mrefu kidogo!.


Muendelezo soma >> Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani
𝐒𝐢𝐦𝐮𝐥𝐢𝐳𝐢 𝐭𝐚𝐦 𝐦𝐩𝐚𝐤𝐚 𝐧𝐚𝐤𝐮𝐭𝐚 𝐧𝐚𝐜𝐡𝐞𝐤𝐚 𝐩𝐞𝐤𝐞 𝐲𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐚𝐬𝐞𝐞!! 𝐡𝐨𝐧𝐠𝐞𝐫𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐮𝐭𝐮𝐧𝐳𝐢

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Booojooo kaziroooooo 🙆🙆🙆🙆🙆Kumbe na Bukoba mshavamia! Iiinnyweeeeee😁😁😁😁😁 in nshomiles voice 😎😎
 
Tupo.Ndugu yetu kawakilisha vyema kwa uvumilivu na unyenyekevu mkubwa kama ilivyo Asili yetu ya kikurya huwa hatutishwi na maneno ya watu Big up Mura Umughaka

Tafsiri ya neno Umughaka kwa kiswahili ni Mwanaume kwa wasio jua
Ahsante kwa taarifa mkuu
 
Back
Top Bottom