Mbute na chai
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 564
- 593
Tukio lililonitokea nikiwa darasa la tatu.
Ikiwa muda wa masomo umemalizika, nikiwa na wanafunzi wenzangu, tunapita jirani na mti wa mzambarao. Mti ule ulikuwa umesheheni zambarao zilizoiva na nono zaidi, wale waliyopitia maisha haya nadhani wananielewa vizuri. Mti huo ulikuwa mrefu mithili ya futi 60 hivi za urefu basi, kwakuwa nilikuwa mtundu nikasema ngoja nikwee nikajiangulie yaliyo mazuri zaidi. Nilimkabidhi rafiki yangu mfuko wangu wa madaftari uliyojulikana kama sport enzi hizo, nikamwambia nikidondosha zambarao unanihifadhia. Nilipofika mtini nikasema ngoja nile kwanza halafu nitashusha zingine. Baada ya kutosheka kula nikaanza kuangua na kumdondoshea rafiki yangu ahifadhi.
Nilipokuwa nadondosha zile zambarao nilisikia huko chini wakibishana na yule rafiki yangu akiwaambia ‘mimi ndiye ninayemkusanyia.’ Juu ya mti zambarao zile nono huwa zinatabia ya kuwa kwenye matawi membamba ya pembezoni nikajisemea isiwe tabu, basi nikashika tawi nene mkono wa kushoto huku mkono mwingine nikijinyoosha kufikia hizo zambarao na kumbe lile tawi nene lilikuwa na wadudu ambao tulikuwa tunawaita nyugi (wasp) jamii kama ya nyuki. Kumbe nilivyokuwa najinyoosha ndivyo nilivyokuwa natingisha kile kijumba chao na nilipokaribia kukamata kitawi chenye zile zambarao nikasikia kama mtu kanidunga sindano ya sikio, kwa wenge nikaachia lile tawi nene, mama yangu!!!! Nilisikia pwaaaaaach, parapataaaaa, kurukunguuu…… nikiwa katika hali ya taharuki nasikia huko chini zinakuja nyingi naomba na sisi tukuokotee bila kujua kuwa nilikuwa mimi mwenyewe ndiye naporomoka kama jackie chan kwenye movie ya who am I. Mungu saidia nikanasa kwenye matawi ya katikati huku jasho uchafu ule unaotoka kwa kujificha vyote vimenienea. Ile kama napata hafueni lile tawi lililonikwamisha pale likavunjika bahati nzuri nikawa nimekanyaga mti wenyewe. USIOMBE YAKUKUTE.