Nilivyosave Milioni 10 kwa miezi 6 na kujenga nyumba mbili na kununua gari zuri

Hongera sana. Mie nimekuelewa kua ukiwa na malengo flani ni vizuri kujibana na kuongeza njia zingine za kipato ili uyafikie.

Halafu nyie mnaoshangaa kusave 10 millions kwa miezi sita angalieni maisha aliyokua anaishi kwa hesabu za haraka hakua anatumia zaidi ya laki 3. So kwenye mshahara pekee aliweza kupata million 6.

Na hizo side hustle kumletea million 4 kwa miezi sita ni sawa mbona sio kitu cha ajabu. 4 millions kwenye biashara/deals nzuri kwa miezi sita? Inawezekana.
 
Asante sana, yale maisha yainifunza mambo mengi sana kwa muda mchache, jambo ambalo ningelifanya kwa miaka 15 nililifanya kwa miaka pungufu ya sita.

Ninausoma upepo wa nini cha kubana hapa kwangu nilipohamia hasa nauli za kufika kazini na matumizi ya familia pamoja na kuongeza njia zaidi za kupata kipato nje ya ajira ili nifikie lengo lingine kubwa. Inawezekana!
 
Kumbe wewe una vyanzo vingine vya mapato ila inatutajia tu mshahara wa 1.3M.

nyie inspirational speakers mna matatizo gani.
Mnafaidika nini kqa kusema uongo?

1.3M - 35000 kila mwezi - 15000 za mtoto
 
Mmh casino manager, kazi za casino zinakuaga za shift sana na weekend kupata off casino ni ndoto za alinacha maana ndo siku za kazi,sasa ulikua una manage vipi huo mda? maana kuna mda unaingia night inabid upumzike mchana em nieleweshe mkuu na kigogo kulivo mida ya night pia ulikua unatembea wajuba wanakuacha salama [emoji44]
 
SUV ni ya kununua kwa mtu kwa milioni 6 hivi pamoja na ufundi kidogo kuirekebisha, siyo miaka 3, ni zaidi ya sita sasa mkuu
So, ni 6M… sio “approximate 20M”?

But story yako inajenga. La msingi mtu ni kuwa na GOALS zenye timeframe then kustrategize the HOW to reach malengo hayo

Kupendapenda starehe na kula bata kwa sana hakuwezi kumfikisha mtu kwenye malengo yake
 
Kumbe wewe una vyanzo vingine vya mapato ila inatutajia tu mshahara wa 1.3M.

nyie inspirational speakers mna matatizo gani.
Mnafaidika nini kqa kusema uongo?

1.3M - 35000 kila mwezi - 15000 za mtoto
Sijaelewa kwanini umefocus kwenye mshahara. Lengo halikuwa kuelezea mshahara. Nimeelezea namna nilivyofikia ndoto yangu ya kusevu milioni kumi. Rudia kusoma
Kigogo Sambusa unaijua? Ipo Ilala Msimbazi. Siyo Kigogo unakosema wewe.

Off yangu ni Jumapili na Jumatano. Siku nyingine zote ni night shifts.
 
So, ni 6M… sio “approximate 20M”?

But story yako inajenga. La msingi mtu ni kuwa na GOALS zenye timeframe then kustrateguze the HOW to reach malengo hayo

Starehecna kula bata kwa sana hakuwezi kumfikisha mtu kwenye malengo yake
Hakika mkuu. Malengo yanafikiwa kwa kuzipa talaka starehe na bata. Sikuwa na uwezo wa kuwaza kununua gari ya m20.
 
Mkuu unaelewa maana ya kuserve? Total minus consuption, Kinacho baki ndio kusevu. Sasa wewe unachukua A+ B unasema umeserve??😅😅
 
Mkuu nipigie shavu la kazi kazini yoyote ata kama ni usafi ntashukulu sana nipo dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…