SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
Habari, ndugu jamaa na marafiki kwa jina naitwa Moris, nilizaliwa mkoa wa mara nilisoma na kumaliza masomo ya sekondari na kufaulu vizuri mkoani mara.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari nili jiusisha na kazi ya ufundi umeme wa majumbani, ambapo kazi hii hapo awali alikuwa akifanya baba yangu.

Ndoto yangu ilikuwa nikuja kuwa rubani wa ndege na nilipenda sana maswala ya utafiti na uchunguzi. lakini pia nilipenda kushirikiana na watu wadogo kwa wakubwa, pamoja na kujifunza "kinaganaga" vitu vingi sana.

Kama vile usomaji wa vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya dini na bidii katika kazi ya ufundi umeme ilinisaidia sana. lakini pia nilifanya bidii katika ibada, ambapo nilikuwa nikifanya bidii ili nije kutimiza ndoto yangu ambayo ni kuja kufanya kazi ya urubani wa ndege.

Katika chunguzi na tafiti zangu Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kutengeneza mashine ya kuzarisha umeme, ambayo ilifanya kazi vizuri lakini nakumbuka mashine hii ilinipa "wigo" msukumo mzuri wa kuiboresha mashine iwe bora zaidi. sikuishia hapo lakini nilijiendeleza kwa kujifunza kupitia vitabu vya kisayansi, ambapo baadae nilipata "shauku" iliyo nipelekea kufanikiwa kwa wazo la kutengeneza helikopta.

Nadhani nilitengeneza kitu bora na cha tofauti kuliko ninavyokielezea hapa. lakini kwa sababu sikuwa na vibali maalum kutoka vitengo husika vya kiserikali pamoja na mamlaka ya anga ilinipelekea kufungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo sababu nyengine sikuwa na reseni.

Pengine wapo vijana wenzangu wengi sana mitaani, ambao hawaja fahamika "kinagaubaga" Kutokana na kazi zao. Ingawa pamoja na mapinduzi makubwa ya teknolojia walio yafanya ndani na nje ya Tanzania, wenye ndoto sawa na zangu lakini wame fukiwa kwenye shimo "kindakindaki" hata wasiweze kupewa nafasi ya kuonesha maarifa walio nayo na vipaji vyao.

Matokeo yake wanatokea watu wenye jicho la "husuda" ambao wasiokuwa na maslahi bora kwa vijana pamoja na taifa kwa ujumla. ambao wanafanya kazi ya kuzima vipaji kupitia madaraka na siyo kwamba nchi yetu hatuwezi kuendelea kwenye maswala ya kisayansi na kiteknolojia "la hasha" kumbe tunajiangamiza wenyewe na kujiteketeza "kimasomaso" bila kujua.

Kupitia kwa vijana wanao zaniwa kuwa wao siyo kitu na kufungiwa kazi zao kwasababu zisizo za msingi, matokeo yake wanaendeleza watu wasio na ujuzi wowote kwenye hizo fani ambapo inapelekea taifa kuzidi kushuka kimaendeleo na kiuchumi.

Nina imani kwamba kitaka kila kizazi kipya ndani ya kila miaka mitano, lazima kuna vijana wenzangu wanao chipuka kwenye fani mbalimbali kwenye nyanja zote ambao naweza kusema ni vijana hodari sana ambao hawaja somea kwenye hizo fani walizopo.

Taifa zuri hujengwa na vijana, watu wengi wamekuwa wakishuhudia vijana ambao tunaishi nao tu mitaani. wengine ni ndugu zetu tumeona vipaji vyao walivyo vionesha kwa njia mbalimbali lakini kwa sababu ya kutoendelezwa imewapelekea kualibikiwa kisaikolojia matokeo yake kuanguka kwenye "ngada" na madawa ya kulevya.

Najua wapo vijana wenzangu miongoni mwetu walio fanikiwa kutengeneza vitu vingi vikubwa zaidi yangu, lakini wameshindwa kujiendeleza katika nyanja zote ikiwemo katika sayansi na teknolojia. pamoja na kwamba vitu walivyo vitengeneza vimeonekana lakini kwa sababu ya kuto kizi vigezo vya kiserikali wamefungiwa.

Hivyo naungana pamoja na vijana wenzangu kutoa "lai" kwa serikali, iangalie kwa ukaribu namna bora ya kutuendeleza sisi vijana kwenye nyanja zote. kwamba vijana wapewe kipaumbele itapelekea vijana wengi kupata "hulka" ya ajira na kujiamini pamoja na kuimarika kisaikolojia.

Hakika"penye nia pana njia"Itasaidia sana pia kuwavuta vijana wengine wa mitaani kupata fursa kuacha tabia ambazo ni mbovu mara moja. kama vile "panya road" tabia ambazo zinaweza kuyumbisha au kuangusha kabisa uchumi wa taifa, jambo ili nalitazama kwa mapana zaidi kwa sababu vijana ni "mbegu" ambazo zina paswa kuangaliwa ili ziweze kustawi vizuri zitazamwe Kama kitovu cha taifa la kesho.

Serikali ihakikishe vijana wanapata haki zao za msingi, iwapo kama ikitokea kuna kijana amegundua kitu flani ndani ya sayansi na kwamba kipaji chake kimeonekana na kuthibitishwa tayari.

Serikali isimfungie kwa sababu kwa kufanya hivyo itamuharibu kijana kisaikolojia, kama ikatokea ajakizi vigezo asifungiwe lakini iangaliwe namna bora ambapo kijana aweze kupata kibali pamoja na elimu zaidi. kwasababu kwakufanya hivyo taifa litakuwa linapanda "mbegu" iliyo bora na imara zaidi kwa ajiri ya maendeleo bora na kupata vijana wenye ujuzi.

Kama ikitokea kijana hana elimu ya kutosha kwamba ameshindwa kupata kibali kwa sababu ya elimu ndogo aliyo kuwa nayo. Lakini tukirudi kwenye uwezo wake na ujuzi kwamba kipaji chake tayari kime onekana pamoja na kuthibitishwa na wataalam mbalimbali wa serikali basi kijana asomeshwe.

Serikali na vyombo husika vichukulie kwa mitazamo mipana sana na kwaajiri ya sayansi na teknolojia ya taifa la kesho. ili kijana anapo maliza masomo afanye kazi ya ndoto zake kwasababu kipaji ni "kimwasu" naamini kwa namna moja ama nyengine kwa njia hii nchi yetu itaendelea kiuchumi katika nyanja zote ikiwemo kwenye ajira, sanaa, elimu, michezo, sayansi na teknolojia.

Lakini pia wazazi na walezi muhakikishe mnakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wanapata malezi na ushauri mzuri ulio bora wenye tija ndani yake. ambayo ni njia itakayo wafanya vijana kujisikia kuwa wao ni watu wa muhimu sana wanaohitajika na wenye mchango mkubwa ndani ya jamii inayo wazunguka. Ili waimarike vizuri kisaikolojia pamoja na kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhulia kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni mda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
 
Upvote 53
Baada ya kumaliza kusoma bandiko hili gusa kimshare chini ya post chenye aram hii "^" kunipigia kura nipate nafasi ya kuibuka mshindi.
 
Kura yangu unayo brooo
Vijana tuache ujinga
 
Kura yangu unayo brooo
Vijana tuache ujinga
Lakini pia serikali inachangia pakubwa Kuwa haribu vijana kisaikolojia hali ya "kutojiamini".

Siwezi kuwalaumu vijana wenzangu wa mitaani wengi wao wamesoma na wana vyeti vyao, unakuta mtu ana degree yake alafu anafanya kazi ya bodaboda linapo tokea swala la kujiajiri wenyewe kwenye nyanja flani, vijana wananyimwa haki zao awapewi vibali.

Najiuliza inamaana hii inchi inazingatia haki za binadamu kwenye swala la kujiajiri au kuna kipengere kwenye sheria kinacho zuia vijana kujiajiri kwenye nyanja za sayansi na teknolojia na kuruhusu kwenye kilimo na bodaboda.?

Vijana wengi wamekuwa wakiishi nje ya ndoto zao kwasababu ya kukosa haki zao za msingi hili ni pengo kubwa sana litakalo chelewesha maendeleo.
 
Na ili watu wawe na moyo na hali ya kuendeleza kufanya Tafiti bunifu ni lazima kuwe na ruzuku serikali lazima iwezeshe jitihada za kila ambae ana buni kitu chake hata kama iwe kitu hiko kinafanana na kingine sokoni

mfano magari Mgunduzi wa injini wa kwanza ndio alieleta mapinduzi ya magari lakini siku hizi kuna magari mengi yamebuniwa ya aina tofauti tofauti ya umeme, gas, na Mafuta
lakini mifumo ya injini, piston na Valves huo ni ubunifu pia tusikae kusema tu hiko sio kipya kilifanywa hujui ni kitu gani mtu kaongezea humo
 
Ni miongoni mwa ndoto zangu kwa sasa nimejifunza concept Kama za kurusha rocket, pia nime jifunza theory kama vile za kina Einstein ( general relative, quantum physics, newton theory of gravity" lakini katika kujifunza huku nimefanikiwa kutengeneza theory yangu mwenyewe inayo husu "big bang" namuomba sana mungu nitimize ndoto yangu ya kuja kufungua kampuni binafsi ya anga hapa nchini. nadhani kila kitu kinawezekana kwa vijana itabidi tuwaombe Sana vijana wa ki-Tanzania wabadirike wawe "chanya" Lakini pia tusisahau kuwaombea vijana wale waliopo mahututi hospitalini.
Wewe umetengeneza formula ya big bang Wacha masihara

Naomba nione kama hutojali
 
General relativity sio relative
 
Kaka unajua serikali inaweza kufanya kitu hapa Ila kuna watu flani wana kinyongo pale kijana utakapo onekana unaujuzi kuliko wao basi lazima wakufungie na reseni upati.

Hatuwezi kuendelea ikiwa sisi kwa sisi hatupendani hatupeani sapoti Ila kinachofanyika nikuzima kipaji kwa sababu zisizo za msingi kwenye nyanja za sayansi na teknolojia.

Ukiangalia mwenye upande wa kilimo na michezo unaona vijana wanavyo pata sapoti hadi kwenye hatua za kimataifa. Lakini kwenye sayansi na teknolojia imekuwa "mwiba" kijana akijiusisha na kipaji chake kwenye ugunduzi na chunguzi za kisayansi unafungiwa Mara moja.

Serikali iangalie hili swala siyo la kufumbia macho linadumaza uchumi na maendeleo ya taifa letu.
 
Wewe umetengeneza formula ya big bang Wacha masihara

Naomba nione kama hutojali
Big bang siyo formula,!!!!

Tafuta kwenye fizikia na kihisabati Kama utaona kuna formula ya big bang aipo hakuna, Unajua maana ya "big bang" kwenye sayansi na teknolojia.

"Big bang" ni nini ?
Tunajua vitu vyote ulimwenguni kabla avijawepo lazima kuna chanzo chake kilicho fanya kiwepo na kwamba kila kitu kina chanzo chake na lazima kianzie kwenye hatua ya udogo.
MFANO

Miti kabla ijazaliwa ilianzia kwenye udogo sindiyo, mfano binadamu Kabla ajazaliwa alianzia kwenye udogo sindiyo nk.

Tuna jifunza sayansi huwa inaenda na uthibitisho sasa nita kuthibitishia ili unielewe. Naomba tuweke maswala ya ustarabu Wa kidini pembeni haya twende sasa.

Tunajua wewe kabla ujazaliwa hapo awali kulikuwa amna kitu yani empty, namaanisha wewe huyu wa leo hii kuna hatua ulipitia yani ulianzia kwenye udogo mpaka kufikia kuwa mtu mzima. Sasa tukija kwenye sayansi swala hili tunalichukulia Kama jambo ambalo lina uthibitisho kwamba wewe kabla ujazaliwa kunakitendo kilicho anzia udogo Wa "atom" mpaka kutengeneza kiumbe alafu ukazaliwa.

Sasa turudi kwenye "Big bang" kisayansi ni nadharia inayo elezea "uumbaji" wa ulimwengu wote huu unao uona kama tulivyo elezea huko juu kwamba kila kitu ulimwenguni lazima kilizaliwa na kilianzia kwenye udogo basi hata huu ulimwengu wetu ulizaliwa na ulianzia katika hali ya udogo.

tukijumisha mfumo mzima wa jua (solar system) pamoja na mfumo wa (galaxy) galaksi, kabla ujazaliwa kuna mchakato uliofanyika kuanzia udogo wa "atom" sijui kwa kiswahili chake tuite nini "atomi"

Sasa "big bang" inaelezea mchakato uliofanyika mpaka kuzaliwa kwa huu ulimwengu na nyota zote kwamba kabla ujazaliwa ulikuwa katika hali ya udogo ambapo ulianza kutanuka kuanzia udogo na kupelekea mlipuko ambao baadae ulipoa na kutengeneza "dark age" kipindi cha giza baadae zika zaliwa "nebulae" ambapo ni mjumuiko wa gas mbali mbali Kama hydrogen, oxygen, helium ndiyo maana unaona kuna gas duniani unajiuliza zimetokea wapi ?, sasa tuendele.

Sasa uwepo wa hizi gesi kwenye dark energy (energy fields) hizi gase zilianza kusumbua particles za dark age ambazo zilikuwa tuli. Naomba hapa Kama ujaelewa utaniuliza swali tuendele.

Sasa mchakato huo wa uwepo wa gas ambapo kwa jina lengine matter (maada) ulisababisha uzito ambao ulipelekea kuzaliwa kwa nyota na sayari pamoja na bahari na maji na miti.

Unashangaa kwanini nimetaja maji unajua maji ni nini maji ni muunganiko wa gesi mbili yani oxygen na hydrogen ambazo gas hizi zimeundwa na vipunje vidogo vidogo Sana visivyo onekana kwa macho ambavyo sisi tunaita "Maji"

Lakini pia zikazaliwa nyota unajua nyota "jua" ni nini ?

Jua letu hili ni muunganiko Wa gas mbili yani hydrogen na helium ambazo zimeundwa na vipunje pia ambazo gezi hizi zimesababisha muwako endapo ziki kusanishwa pamoja kwa walio soma "chemistry" wame nielewa.

Kwaiyo "big bang" siyo formula ni mlipuko ambao unaelezea uumbaji ulivyo fanyika hadi kufikia ulimwengu Wa sasa.
 
Ni miongoni mwa ndoto zangu kwa sasa nimejifunza concept Kama za kurusha rocket, pia nime jifunza theory kama vile za kina Einstein ( general relative, quantum physics, newton theory of gravity" lakini katika kujifunza huku nimefanikiwa kutengeneza theory yangu mwenyewe inayo husu "big bang" namuomba sana mungu nitimize ndoto yangu ya kuja kufungua kampuni binafsi ya anga hapa nchini. nadhani kila kitu kinawezekana kwa vijana itabidi tuwaombe Sana vijana wa ki-Tanzania wabadirike wawe "chanya" Lakini pia tusisahau kuwaombea vijana wale waliopo mahututi hospitalini.
Interesting!

Natamani sana niijue hiyo nadharia ya namna yako ya 'big bang' ipojepoje asee....
 
Anhaa oookay, nimeshaiona
 
Ni miongoni mwa ndoto zangu kwa sasa nimejifunza concept Kama za kurusha rocket, pia nime jifunza theory kama vile za kina Einstein ( general relative, quantum physics, newton theory of gravity" lakini katika kujifunza huku nimefanikiwa kutengeneza theory yangu mwenyewe inayo husu "big bang" namuomba sana mungu nitimize ndoto yangu ya kuja kufungua kampuni binafsi ya anga hapa nchini. nadhani kila kitu kinawezekana kwa vijana itabidi tuwaombe Sana vijana wa ki-Tanzania wabadirike wawe "chanya" Lakini pia tusisahau kuwaombea vijana wale waliopo mahututi hospitalini.
Theory yako mpya inayohusu Big Bang inasemaje mkuu, japo kwa ufupi?
 
Back
Top Bottom