SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
Habari, ndugu jamaa na marafiki kwa jina naitwa Moris, nilizaliwa mkoa wa mara nilisoma na kumaliza masomo ya sekondari na kufaulu vizuri mkoani mara.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari nili jiusisha na kazi ya ufundi umeme wa majumbani, ambapo kazi hii hapo awali alikuwa akifanya baba yangu.

Ndoto yangu ilikuwa nikuja kuwa rubani wa ndege na nilipenda sana maswala ya utafiti na uchunguzi. lakini pia nilipenda kushirikiana na watu wadogo kwa wakubwa, pamoja na kujifunza "kinaganaga" vitu vingi sana.

Kama vile usomaji wa vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya dini na bidii katika kazi ya ufundi umeme ilinisaidia sana. lakini pia nilifanya bidii katika ibada, ambapo nilikuwa nikifanya bidii ili nije kutimiza ndoto yangu ambayo ni kuja kufanya kazi ya urubani wa ndege.

Katika chunguzi na tafiti zangu Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kutengeneza mashine ya kuzarisha umeme, ambayo ilifanya kazi vizuri lakini nakumbuka mashine hii ilinipa "wigo" msukumo mzuri wa kuiboresha mashine iwe bora zaidi. sikuishia hapo lakini nilijiendeleza kwa kujifunza kupitia vitabu vya kisayansi, ambapo baadae nilipata "shauku" iliyo nipelekea kufanikiwa kwa wazo la kutengeneza helikopta.

Nadhani nilitengeneza kitu bora na cha tofauti kuliko ninavyokielezea hapa. lakini kwa sababu sikuwa na vibali maalum kutoka vitengo husika vya kiserikali pamoja na mamlaka ya anga ilinipelekea kufungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo sababu nyengine sikuwa na reseni.

Pengine wapo vijana wenzangu wengi sana mitaani, ambao hawaja fahamika "kinagaubaga" Kutokana na kazi zao. Ingawa pamoja na mapinduzi makubwa ya teknolojia walio yafanya ndani na nje ya Tanzania, wenye ndoto sawa na zangu lakini wame fukiwa kwenye shimo "kindakindaki" hata wasiweze kupewa nafasi ya kuonesha maarifa walio nayo na vipaji vyao.

Matokeo yake wanatokea watu wenye jicho la "husuda" ambao wasiokuwa na maslahi bora kwa vijana pamoja na taifa kwa ujumla. ambao wanafanya kazi ya kuzima vipaji kupitia madaraka na siyo kwamba nchi yetu hatuwezi kuendelea kwenye maswala ya kisayansi na kiteknolojia "la hasha" kumbe tunajiangamiza wenyewe na kujiteketeza "kimasomaso" bila kujua.

Kupitia kwa vijana wanao zaniwa kuwa wao siyo kitu na kufungiwa kazi zao kwasababu zisizo za msingi, matokeo yake wanaendeleza watu wasio na ujuzi wowote kwenye hizo fani ambapo inapelekea taifa kuzidi kushuka kimaendeleo na kiuchumi.

Nina imani kwamba kitaka kila kizazi kipya ndani ya kila miaka mitano, lazima kuna vijana wenzangu wanao chipuka kwenye fani mbalimbali kwenye nyanja zote ambao naweza kusema ni vijana hodari sana ambao hawaja somea kwenye hizo fani walizopo.

Taifa zuri hujengwa na vijana, watu wengi wamekuwa wakishuhudia vijana ambao tunaishi nao tu mitaani. wengine ni ndugu zetu tumeona vipaji vyao walivyo vionesha kwa njia mbalimbali lakini kwa sababu ya kutoendelezwa imewapelekea kualibikiwa kisaikolojia matokeo yake kuanguka kwenye "ngada" na madawa ya kulevya.

Najua wapo vijana wenzangu miongoni mwetu walio fanikiwa kutengeneza vitu vingi vikubwa zaidi yangu, lakini wameshindwa kujiendeleza katika nyanja zote ikiwemo katika sayansi na teknolojia. pamoja na kwamba vitu walivyo vitengeneza vimeonekana lakini kwa sababu ya kuto kizi vigezo vya kiserikali wamefungiwa.

Hivyo naungana pamoja na vijana wenzangu kutoa "lai" kwa serikali, iangalie kwa ukaribu namna bora ya kutuendeleza sisi vijana kwenye nyanja zote. kwamba vijana wapewe kipaumbele itapelekea vijana wengi kupata "hulka" ya ajira na kujiamini pamoja na kuimarika kisaikolojia.

Hakika"penye nia pana njia"Itasaidia sana pia kuwavuta vijana wengine wa mitaani kupata fursa kuacha tabia ambazo ni mbovu mara moja. kama vile "panya road" tabia ambazo zinaweza kuyumbisha au kuangusha kabisa uchumi wa taifa, jambo ili nalitazama kwa mapana zaidi kwa sababu vijana ni "mbegu" ambazo zina paswa kuangaliwa ili ziweze kustawi vizuri zitazamwe Kama kitovu cha taifa la kesho.

Serikali ihakikishe vijana wanapata haki zao za msingi, iwapo kama ikitokea kuna kijana amegundua kitu flani ndani ya sayansi na kwamba kipaji chake kimeonekana na kuthibitishwa tayari.

Serikali isimfungie kwa sababu kwa kufanya hivyo itamuharibu kijana kisaikolojia, kama ikatokea ajakizi vigezo asifungiwe lakini iangaliwe namna bora ambapo kijana aweze kupata kibali pamoja na elimu zaidi. kwasababu kwakufanya hivyo taifa litakuwa linapanda "mbegu" iliyo bora na imara zaidi kwa ajiri ya maendeleo bora na kupata vijana wenye ujuzi.

Kama ikitokea kijana hana elimu ya kutosha kwamba ameshindwa kupata kibali kwa sababu ya elimu ndogo aliyo kuwa nayo. Lakini tukirudi kwenye uwezo wake na ujuzi kwamba kipaji chake tayari kime onekana pamoja na kuthibitishwa na wataalam mbalimbali wa serikali basi kijana asomeshwe.

Serikali na vyombo husika vichukulie kwa mitazamo mipana sana na kwaajiri ya sayansi na teknolojia ya taifa la kesho. ili kijana anapo maliza masomo afanye kazi ya ndoto zake kwasababu kipaji ni "kimwasu" naamini kwa namna moja ama nyengine kwa njia hii nchi yetu itaendelea kiuchumi katika nyanja zote ikiwemo kwenye ajira, sanaa, elimu, michezo, sayansi na teknolojia.

Lakini pia wazazi na walezi muhakikishe mnakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wanapata malezi na ushauri mzuri ulio bora wenye tija ndani yake. ambayo ni njia itakayo wafanya vijana kujisikia kuwa wao ni watu wa muhimu sana wanaohitajika na wenye mchango mkubwa ndani ya jamii inayo wazunguka. Ili waimarike vizuri kisaikolojia pamoja na kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhulia kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni mda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
 
Upvote 53
Baada ya kumaliza kusoma bandiko hili gusa kimshare chini ya post chenye aram hii "^" kunipigia kura nipate nafasi ya kuibuka mshindi.
Nimekupigia ila inaitwa kimshale sio kimshare jaribu kujifunza matumizi ya R na L najua watu kanda ya ziwa ni tatizo sana lakini jitahidi
 
Nimekupigia ila inaitwa kimshale sio kimshare jaribu kujifunza matumizi ya R na L najua watu kanda ya ziwa ni tatizo sana lakini jitahidi
Asante sana, kaka nimekosea hapo naomba kunywa soda.
 
Tafathali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Unajua maana ya general relativity ?

Nimeona username yako unaitwa "baba swalehe" Mimi nikikuita "baba sele" nitakuwa nakosea ?
Nmekuuliza because nlkua fast na nlkua na operation mchana ya kufanya

You think I don't know general relativity seriously?
Yaani nisijue description ya gravity in modern world
Curving space and time na bla bla zingine

I wanted to teach you or help you( maybe help you get a good technical school here at minnesota) sio kuishia hapa kukupa votes so far nshakupa
 
Don't about to me i know them.... I have referred from your publication

Wabongo mpoje mbona hampendi kupingwa or kuelekezwa

I know
about Big bang don't explain to me umeandika hapo una law yako and I was curious to know

You have a very odious complex behaviour my friend ukiulizwa swali jibu kirahisi and simple don't show off

I have written an article about
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
Usitusumbue mura..kimshare kiko wapi sasa!! halafu wewe unajua hiyo helikopita unge fanyanyia ya kumwagilia dawa ungepata support hata weye mwenyewe unge mwagilia matoke huko kenyamanyori
 
Hivi wewe una nini? akilini humo? ukiweka mbele hayo ya vinyongo hutafika mbali hayo ni ya Dunia yooote. hata uzunguni wako ivo !......uelewa huna Helikopita ilisha gunduliwa zamani sana wewe ume copy na ku paste!!

wkt hujui kuna hati milki ya wahusika hilo ni ttizo la akili yako!! wewe njoo na wazo jingine jipyaaaa tofauti na hilo siyo unaiga iga tu!! wkt hela ya kulipia fine za kimataifa huna
 
Ni vyema ukawa unasoma kwenye page maalum Kama za NASA utaelewa maana hizi page zengine unakuta mtu anajiandikia tu anacho jisikia ndiyo Kama hivi unachanganya mambo sasa dark energy inawezaje wezaje kuwa "udongo" unakosea.
Hahahahaah! mfano mzuri ni hiyo page. Ni mimi nimejiandikia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£

Concept ya kugawanya ziro ndiyo 'upya' wenyewe ambao sijaweza kuupata huko NASA.

Kihesabu haikatai jombaa nikisema 0/2 = +1 + -1 si ni sawa tu maana hata ukizijumlisha unapata sifuri ileile ya mwanzo bro!

Uzuri wake haiishii moja tu unaweza kupata hadi positive infinity mradi tu ujumlishe na negative infinity, see?
 
Tukisema kuwa kabla ya kuwepo chochote hata hilo giza halikuwepo.

Giza limeanza kuwepo baada ya kugawanya sifuri fulani kuwa pande mbili za giza na mwanga.

Mwanzoni ilikuwa ni hamna/nothingness/utupu yaani ziiiip
 
Kwaiyo ndiyo ume solve ukapata "energy za udongo" ambazo zimetokana na "0" unajua hakuna sayansi ngumu Kama sayansi ya anga za mbali.
 
Unajua sayansi ya anga inaelezewa na uhalisia wa vitu vilivyo duniani sasa wewe tangu lini ukaona sifuri inagawanyika ?
Tukisema kuwa kabla ya kuwepo chochote hata hilo giza halikuwepo.

Giza limeanza kuwepo baada ya kugawanya sifuri fulani kuwa pande mbili za giza na mwanga.

Mwanzoni ilikuwa ni hamna/nothingness/utupu yaani ziiiip
 
Kwaiyo ndiyo ume solve ukapata "energy za udongo" ambazo zimetokana na "0" unajua hakuna sayansi ngumu Kama sayansi ya anga za mbali.
Tushauriane tu hapa, mfano wewe unaweza kuniambia chanzo kingine cha hiyo dark energies?

Hiyo energy za udongo basi achana nalo, ntakuwa nilikukumisquote wewe. Sio wazo langu hata.
 
Unajua sayansi ya anga inaelezewa na uhalisia wa vitu vilivyo duniani sasa wewe tangu lini ukaona sifuri inagawanyika ?
Inabidi iwe hivyo au una mbadala mwingine wa kuwepo kwa chochote badala ya hamna?
 
Huwenda siku soma vizuri maoni yako kaka umeandika hivi " formula za big bang" au nimesoma vibaya nikaona kabla sijaingia deep kwenye theory yangu lazima kwanza nikuelezee "big bang" ni nini.!!!

Ngoja naandika "nondo ya theory yangu hapa sasa hivi naipandisha jukwaani.
 
Ndug
Ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili nakuomba unipigie kura ili niweze kuibuka mshindi.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜† Kumbe mnywa soda una akili hivi ukinywa bia si itakuwa balaa
Bia inaharibu "ubongo" inashauliwa mtu anywe maziwa, soda na maji kwa wingi pamoja na kufanya mazoezi hapo utakuwa fiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…