SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

SoC02 Nilivyotengeneza helkopta

Stories of Change - 2022 Competition

Theorist Mosses

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2022
Posts
345
Reaction score
253
Habari, ndugu jamaa na marafiki kwa jina naitwa Moris, nilizaliwa mkoa wa mara nilisoma na kumaliza masomo ya sekondari na kufaulu vizuri mkoani mara.

Baada ya kumaliza masomo ya sekondari nili jiusisha na kazi ya ufundi umeme wa majumbani, ambapo kazi hii hapo awali alikuwa akifanya baba yangu.

Ndoto yangu ilikuwa nikuja kuwa rubani wa ndege na nilipenda sana maswala ya utafiti na uchunguzi. lakini pia nilipenda kushirikiana na watu wadogo kwa wakubwa, pamoja na kujifunza "kinaganaga" vitu vingi sana.

Kama vile usomaji wa vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya dini na bidii katika kazi ya ufundi umeme ilinisaidia sana. lakini pia nilifanya bidii katika ibada, ambapo nilikuwa nikifanya bidii ili nije kutimiza ndoto yangu ambayo ni kuja kufanya kazi ya urubani wa ndege.

Katika chunguzi na tafiti zangu Kwa mara ya kwanza nilifanikiwa kutengeneza mashine ya kuzarisha umeme, ambayo ilifanya kazi vizuri lakini nakumbuka mashine hii ilinipa "wigo" msukumo mzuri wa kuiboresha mashine iwe bora zaidi. sikuishia hapo lakini nilijiendeleza kwa kujifunza kupitia vitabu vya kisayansi, ambapo baadae nilipata "shauku" iliyo nipelekea kufanikiwa kwa wazo la kutengeneza helikopta.

Nadhani nilitengeneza kitu bora na cha tofauti kuliko ninavyokielezea hapa. lakini kwa sababu sikuwa na vibali maalum kutoka vitengo husika vya kiserikali pamoja na mamlaka ya anga ilinipelekea kufungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo sababu nyengine sikuwa na reseni.

Pengine wapo vijana wenzangu wengi sana mitaani, ambao hawaja fahamika "kinagaubaga" Kutokana na kazi zao. Ingawa pamoja na mapinduzi makubwa ya teknolojia walio yafanya ndani na nje ya Tanzania, wenye ndoto sawa na zangu lakini wame fukiwa kwenye shimo "kindakindaki" hata wasiweze kupewa nafasi ya kuonesha maarifa walio nayo na vipaji vyao.

Matokeo yake wanatokea watu wenye jicho la "husuda" ambao wasiokuwa na maslahi bora kwa vijana pamoja na taifa kwa ujumla. ambao wanafanya kazi ya kuzima vipaji kupitia madaraka na siyo kwamba nchi yetu hatuwezi kuendelea kwenye maswala ya kisayansi na kiteknolojia "la hasha" kumbe tunajiangamiza wenyewe na kujiteketeza "kimasomaso" bila kujua.

Kupitia kwa vijana wanao zaniwa kuwa wao siyo kitu na kufungiwa kazi zao kwasababu zisizo za msingi, matokeo yake wanaendeleza watu wasio na ujuzi wowote kwenye hizo fani ambapo inapelekea taifa kuzidi kushuka kimaendeleo na kiuchumi.

Nina imani kwamba kitaka kila kizazi kipya ndani ya kila miaka mitano, lazima kuna vijana wenzangu wanao chipuka kwenye fani mbalimbali kwenye nyanja zote ambao naweza kusema ni vijana hodari sana ambao hawaja somea kwenye hizo fani walizopo.

Taifa zuri hujengwa na vijana, watu wengi wamekuwa wakishuhudia vijana ambao tunaishi nao tu mitaani. wengine ni ndugu zetu tumeona vipaji vyao walivyo vionesha kwa njia mbalimbali lakini kwa sababu ya kutoendelezwa imewapelekea kualibikiwa kisaikolojia matokeo yake kuanguka kwenye "ngada" na madawa ya kulevya.

Najua wapo vijana wenzangu miongoni mwetu walio fanikiwa kutengeneza vitu vingi vikubwa zaidi yangu, lakini wameshindwa kujiendeleza katika nyanja zote ikiwemo katika sayansi na teknolojia. pamoja na kwamba vitu walivyo vitengeneza vimeonekana lakini kwa sababu ya kuto kizi vigezo vya kiserikali wamefungiwa.

Hivyo naungana pamoja na vijana wenzangu kutoa "lai" kwa serikali, iangalie kwa ukaribu namna bora ya kutuendeleza sisi vijana kwenye nyanja zote. kwamba vijana wapewe kipaumbele itapelekea vijana wengi kupata "hulka" ya ajira na kujiamini pamoja na kuimarika kisaikolojia.

Hakika"penye nia pana njia"Itasaidia sana pia kuwavuta vijana wengine wa mitaani kupata fursa kuacha tabia ambazo ni mbovu mara moja. kama vile "panya road" tabia ambazo zinaweza kuyumbisha au kuangusha kabisa uchumi wa taifa, jambo ili nalitazama kwa mapana zaidi kwa sababu vijana ni "mbegu" ambazo zina paswa kuangaliwa ili ziweze kustawi vizuri zitazamwe Kama kitovu cha taifa la kesho.

Serikali ihakikishe vijana wanapata haki zao za msingi, iwapo kama ikitokea kuna kijana amegundua kitu flani ndani ya sayansi na kwamba kipaji chake kimeonekana na kuthibitishwa tayari.

Serikali isimfungie kwa sababu kwa kufanya hivyo itamuharibu kijana kisaikolojia, kama ikatokea ajakizi vigezo asifungiwe lakini iangaliwe namna bora ambapo kijana aweze kupata kibali pamoja na elimu zaidi. kwasababu kwakufanya hivyo taifa litakuwa linapanda "mbegu" iliyo bora na imara zaidi kwa ajiri ya maendeleo bora na kupata vijana wenye ujuzi.

Kama ikitokea kijana hana elimu ya kutosha kwamba ameshindwa kupata kibali kwa sababu ya elimu ndogo aliyo kuwa nayo. Lakini tukirudi kwenye uwezo wake na ujuzi kwamba kipaji chake tayari kime onekana pamoja na kuthibitishwa na wataalam mbalimbali wa serikali basi kijana asomeshwe.

Serikali na vyombo husika vichukulie kwa mitazamo mipana sana na kwaajiri ya sayansi na teknolojia ya taifa la kesho. ili kijana anapo maliza masomo afanye kazi ya ndoto zake kwasababu kipaji ni "kimwasu" naamini kwa namna moja ama nyengine kwa njia hii nchi yetu itaendelea kiuchumi katika nyanja zote ikiwemo kwenye ajira, sanaa, elimu, michezo, sayansi na teknolojia.

Lakini pia wazazi na walezi muhakikishe mnakuwa mstari wa mbele kuhakikisha vijana wanapata malezi na ushauri mzuri ulio bora wenye tija ndani yake. ambayo ni njia itakayo wafanya vijana kujisikia kuwa wao ni watu wa muhimu sana wanaohitajika na wenye mchango mkubwa ndani ya jamii inayo wazunguka. Ili waimarike vizuri kisaikolojia pamoja na kuwakumbusha vijana kwenda na kuhudhulia kwenye nyumba za ibada ili kukomesha tabia chafu za vijana Kama vile. kushinda kijiweni mda wote, kujiunga na makundi ya kijambazi, kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya.
 
Upvote 53
Hivi upo online tuendelee na mjadara

line
Ungeweka tu maoni ntayakutaga nikija, ni meseji na sio simu.

Vipi? ulilipa muda kulifikiria wazo la kugawanya sifuri?....... au ni ishu nyingine tu!, tell me
 
Mkuu kuna jamaa pale karibu na kidatu MUSOMA (alitengeneza ndege Fulani ivi miaka ilee ) Ile ndege ilikuwa inatembea lakini haikuruka juu yule na wewe ni tofauti .???
 
Kuna baadhi ya vitu ukiona ndugu yako anajifanya anatengeneza au kugundua kaa naye mbali, zinavyatuka muda wowote na hatoweza kufanukiwa chochote cha maana

♦️ Anayechukua maspika na vifaa vya resio na kusema amegundua kituo cha redio

♦️Anayeunga machuma chuma na kuunda kitu mfano wa katapila na kusema amegundua katapula

♦️ Anayetengeneza body kama la helicopter na kuweka injini ya bajaji na kusema kuwa kagundua helcopter, hapo hakuna kitu yote, yote ni matoyi yanayofanywa na watoto kama michezo na ukiona mtu mzima anakomaa nazo weka hii alama?
 
Unajua helikopta ni nini ?
 
Kabla sijatengeneza mjadara na wewe nataka utuambie helikopta ni nini ?
 
Mkuu Mimi nataka nigundue vitu muhimu katika ubongo wa binadamu ...!
 
Mkuu kuna jamaa pale karibu na kidatu MUSOMA (alitengeneza ndege Fulani ivi miaka ilee ) Ile ndege ilikuwa inatembea lakini haikuruka juu yule na wewe ni tofauti .???
Huyo jamaa nilimsikia lakini unajua kutengeneza injini itakayo badirisha nishati kuwa mwendo na kusababisha kitu kitembee ni swala Dogo ilo ?

Unajua jamaa alitengeneza ndege inayo pitisha hewa sasa chanzo cha ndege kupaa ni nguvu kubwa itakayo zalishwa na injini ambapo ndege itaanza kutembea kwa speed hapo zile mbawa zake zitakusanya hewa nyingi na kufanya ndege inyanyuke.

sasa jamaa alishindwa kwenye shepu ya ndege alitengeneza inayo vuja hewa kwamba alitakiwa kutengeneza mbawa za ndege ngumu zisizo pitisha hewa ambapo zitakusanya hewa uvunguni mwa ndege hapo ndege itaruka.

Jamaa alishindwa zile gharama za kutengeneza shepu ya ndege ambayo ni ngumu nazani ni kwasababu ya kukosa pesa za kutosha kwa sababu injini tayari anayo na ndege imetembea basi hapo angemalizia kwenye mbawa za ndege serikali ingemchukua ikamuendeleza jamaa angefika mbali sana.
 
Tafadhali ndugu mpendwa naomba unipigie kura yako hili niweze kuibuka mshindi.

Kwa wageni mnaweza kunipigia kura kwa kugusa kimshale chini kabisa ya chapisho chenye arama hii "^" kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Hebu tuwekee video ya majaribio ya kuirusha hyo helcopter yako kabla hujaomba hivyo vibali kwanza
 
Ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura niweze kuibuka mshindi kwa kugisa kimshale chini ya makala HiI "^" niweze kuibuka mshindi.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura kwa kubonyeza arama ya kimshale "^" chini kabisa ya post hii kura yako itaniwezesha kuibuka mshindi.
 
Tafadhali, ndugu mpendwa baada ya kumaliza kusoma chapisho hili naomba unipigie kura yako kwa kubonyeza arama ya kimshare "^" chini kabisa ya post hii kuniwezesha kuibuka mshindi.
 
Nimekupa kura zote mkuu, karibu ujifunze na kwangu ruksa kunikosoa SoC 2022 - Jinsi lugha ya Kiswahili itakavyoondoa umasikini Afrika

Back
Top Bottom