Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa nimekusikia mfilipino. .....😂 😂 😂
Watu huwa wanapitia mengi lakini kutokana na akili zenu wabongo huwa mnawaza chai tu.
Nimekusikia mvenezuela......Muvi za Kikorea ambazo ni fictions huwa mmaziamini kwa sababu ni za watu ambao sio wa Tanzania kama wewe mnaziamini.
Mambo ya kiroho ni mapana sana, mambo ya kulala na kila demu kwa kuwa umempata kirahisi unavuna mikosi, nuksi, laana ambazo zinaepukika, vijana muwe makini kulala na kila mwanamke ni maagano mnabaslishana uchafu wa nafsi
Pole sana mkuu,
Wasalaam wana jamvi,
Kama kichwa cha huu uzi kinavyosema na nimeamua kuanzisha huu mkasa ambao ni wa kweli kabisa ulishawahi kunitokea kipindi cha nyuma miaka kadhaa iliyopita. Na huu mkasa nimekukumbuka na nimeamua ku share na nyinyi hapa baada ya kuusoma mkasa wa @Stepanov.
Mkasa ulikuwa hivi, Ilikuwa siku ya jumamosi mida ya saa 12:30 jioni nilikuwa kwenye Bar fulani na washikaji, sasa ilipofika huo muda Muziki kwenye ile Bar ukazimwa ili kupisha muda wa adhana ya Maghrib. Baada ya kuzimwa muziki nikatoka nje kuzungumza na simu, nilipomaliza kuzungumza na simu na tayari nilikuwa na wenge kidogo la hangover nikawa narudi tena ndani nikashikwa mkono na dada mmoja.
We Kaka samahani kidogo kuna mdogo wangu alikuwa ana shida na wewe, nikasimama nikawa namsubiri kumuona huyo mwenye shida na Mimi. Aisee ilikuwa ni pisi ya maana tena kiwango cha SGR ya 🇨🇳 sio ya 🇹🇿. Na hapo tayari giza lilikuwa limeshaanza kuingia ilikuwa inaelekea saa 1 usiku. Yule Dada aliyenishika mkono akanivuta pembeni ili aniunganishe na yule demu aliyekuwa anataka kuongea na Mimi.
Baada ya hapo akaja yule demu alikuwa anaitwa Fatma akaanza kujie express mwenyewe, Samahani Bro ulikuwa umekaa na wenzako pale nilikuwa nashindwa hata namna ya kukuita au kukupata lakini Alhamdullilah ulipotoka nje kuongea na simu imekuwa ni self golden chance kwangu, akanitongoza yule demu na Mimi nilivyokuwa namuona aisee akili zote zikawa zimehamia kwenye kumla tu. Wakati anaongea hayo yote Mimi nilikuwa nipo kimya tu. Baada ya hapo akaniomba namba ya simu nikampa bila ubishi, nikamwambia basi poa haina noma, Pembeni alikuwa na gari Audi A4 rangi ya gold imepaki pale.
Kukatisha mada, baada ya masaa mawili tulienda kwenye hotel fulani tukakaa rooftop ukawa tunakula na kunywa vinono, sasa cha kushangaza muda wa kuondoka pale chini kuna gari nyingine ikawa inatusubiri pale ilikuwa ni IST sio Audi tena na ilikuwa na dereva wa kiume. Tukapanda ile gari nikarudishwa mpaka home nilikokuwa nimepanga bila hata kumwambia yule Dereva na yule Manzi naishi wapi. Tukiwa ndani ya gari nilikuwa nafanyiwa manjonjo na yule Manzi aisee 😂
Baada ya kurudi ghetto jumapili nikaamka mida ya saa 5 asubuhi, nikawa nawaza mambo mengi sana maana tumbo lilikuwa linauma as if nilikuwa nimepiga shoo ya nguvu sana usiku mpaka kiungo na mayai yake vilikuwa vinauma 😖
Ukapita muda kidogo nikaanza kuandaa msosi ghafla simu ikaita namba ngeni ikaingia kuipokea ni yule Manzi akaniambia yupo getini nilishangaa sana na akaniambia njoo nifungulie na alikuwa na msosi ule ule nilikokuwa nautamani siku hiyo, nilikula bila hata kuhoji baada ya hapo akaanza kuvua nguo zake maana alikuwa amevaa abaya akabaki na 👙 akazima na taa na chumba changu kilikuwa ghorofani ikawa ni giza tu.
Nikajikuta navunja tena amri ya sita katika mazingira nisiyoyaelewa lakini cha kushangaza akawa anataka kunipeleka buza hapo akili ikawa inanijia nikawa napinga sana kile kitendo ghafla nikapotelea usingizini kuja kushituka mida ya jioni sana na mwili hauna hata nguvu na yeye alikuwa ameshavaa akawa amekaa tu kwenye kiti na alikuwa amejiremba sana as if ndo kama ameingia.
Kukatisha, Jumatatu nimeingia kazini fresh muda wa kuondoka nikajikuta nimebeba vitu vya ofisini yaani kama naiba vile Boss akaniacha tu ile natembea barabarani akaniita na kuniambia We mwizi kwanini unaondoka na laptop tena ni mpya na begi lake?
Akaninyang'anya lile begi akaniambia maneno mabaya sana na Mimi nilikuwa sielewi chochote. Kesho yake nikaingia ofisini nikakutana na Mkurugenzi aisee ilikuwa noma kubwa na yule Mhindi akataka kunipeleka Polisi yaani nilifukuzwa kazi kama mbwa.
Baada ya hapo niliondoka nikarudi ghetto akili hata haiwazi chochote. Jioni nampigia yule demu aliniambia maneno ya hovyo sana na hata demu wangu ambaye alikuwa yupo mkoa mwingine nilipompigia simu alinitukana na kuniambia it is over sikutaki tena.
Haya ndio yaliyonikuta kushobokea Wanawake barabarani au njiani sio ishu kabisa.
Nawasilisha.
Ukiendelea hivi utakuwa mwandishi mzuri wa hadithi japo hii ipo kama ndoto vile japo sijasoma yote
1. Labda nikuulize tu; ni Baa gani hiyo ina zima mziki ili Waislam wapige adhana?
2. Kulikuwa na umuhimu gani wa kuhusisha kutongozwa kwako na Uislam?
3. Una maanisha mtu akiibiwa simu na mtu anayejiita John aseme ameibiwa na Mkatoliki?
Kutamani hakufai na siku zote ni kuomba Mungu akuepushe na mashambulizi ya Shetani
Sababu ya kuanzisha huu uzi ni kwa sababu nilikua na changia uzi wa Ivan Stepanov ana wakaniomba Wadau kama wawili au watatu ni sheee nao mkasa wanguView attachment 2990674
Mkuu mada yako imenikumbusha hili povu ulilonitolea. Noan umeamua kuiga upuuzi wangu. Vipi huna furaha?
Sina sababu ya kutafuta. Lakini ulichoweka hapo ni nini kama sio maisha binafsi kama mimi. Jambo la msingi ni kutokuchukulia sana seriously mambo ya social media. Sometimes tunachangamsha genge tuOKW BOBAN SUNZU tafuta thread ya Ivan Stepanov alioanzisha jana halafu soma post #231 mpaka #235
siku hizi yanatongoza walevi na kuliwa tigo?hebu nipe huo mtaa wa majiniMkuu pole sana. Niulize swali
Hilo lilikua jini live
- huKo Buza ulifika siku hiyo?
- je uliweza kurud kwenye hali yako ya kawaida tena? Ulifanyaje fanyaje na ilikuachukua muda gani?