Nilivyoumbuka kwenye swimming pool

Nilivyoumbuka kwenye swimming pool

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Amani iwe nanyi waungwana...

Haya maswala ya kuigaiga na kujifanya over confidence kisa Umeona kuna watu wa aina fulani, niwaonye yatakuja kumtoa mtu uhai!.

Kiberenge wa watu nilikuwa nimeenda kutembea hotel fulani hivi ina bonge la swimming pool,kuogelea sijui hilo nalijua mpaka katikati ya ubongo wangu!.

Lakini yale maji yalikuwa yanatamanisha si haba kwanza unaona mpaka chini,halafu yanapumua uhai uhai tu!.

Isitoshe kulikuwa na hali ya hewa amaizing kajua fulani hivi ka saa nne kale ambako malaika bado hawajaanza kuchochea jua kwaajili ya kubandika maharage ya mbinguni!.

Pembeni yangu kulikuwa na wazungu kama wanne hivi wapo juu ya swimming pool,wanapigazao stori wakicheka na ndio hao walioniponza!.

Upuuzi ni kujua kuwa wazungu wote wanajua kuogelea kumbe wengine balaa tupu wanaishi kwenye mabalafu tu huko!.

Ujasiri wangu nilijua wataniokoa tu hata nikizama!, baada ya kuwapa "Hi" kiberenge cha watu nikajisaula nakubaki na mpensi wangu!, taratibu nikajivuta kwenye swimming pool hadi kwenye maji ya kina kifupu nikatumbukia nikawa nasogea kwenye kina kirefu hapo najiona mimi ndo kambale sasa kama sio mumi!.

Baada ya kuyazoea kidogo nikasogea ya kina cha tumboni,baadae ya shingoni! Sasa bilinge bayoyo ndo ikaanzia hapo miguu huku chini nikaanza kuhisi kama inabebwa! Nikajiachia kikambare hapohapo ndio usaliti na maji ukanianza!.

Steps za mikono na miguu zikaanza kushindana kumbe wakati nafanya hivyo ndo nikazidi kwenda kwenye kina zaidi!. Nikajitia u super star ati nizamie!,mzamo ukakubali kuibuka kukakataa!.

Abadani mzamiaji nikashindwa kuwa muibukaji,nilishuka mpaka chini nikakanyaga tiles za swimming nikajisukuma kuelekea juu,hapo miguu na mikono yote inakazi ya kupiga maji hadi nikasahau upi mkono upi mguu ilimradi tu nijitoe kwenye yale maji!.
Msukumo ulikuwa hafifu hata sikufika juu! Hapo pumzi za kiberenge kwishneh!.

Nikarudi tena chini nakukanyaga tena tiles mara hii sikufanya mchezo nilisukuma haswa!,ile nakaribia kufika juu nikaachama mdomo walahi kile sio kikombe ni jagi!.. niliyanywa ya maana japo nilipata kaupenyo ka kuvuta hewa kiduchu!.

Ndo wale wazungu wakataharuki hapo maji yananirudisha chini kwa raundi nyengine yaniue nije kuwa mzimu wa ukoo sijui.

Mikono narusha hovyohovyo miguu naruka ndomboro sio mateke tena!,kufika chini nikajipush tena Sasa mara hii ile naibuka tu nilivuta hewa Kama propera maji niliyomeza sijui ilikuwa lita ngapi!.

Hapo wakati nazama tena nilishuhudia miguu ya watu ikitaabika kulizunguka pool na vichwavichwa vya watu vikihangaika huku na kule!.

Sasa hiyo tafrani ndo nikajua kwisha habari!.. nikazama kwa mara ya tatu nikaibuka tena ile naibuka nakuta natazamana na lifimbo linamashikio nikataka likamata nikalikosakosa!!.

Walikuwa wamelishika watu wawili ili nikilishika wanivute bahati mbaya ikawa upande wangu!.

Nikarudi tena chini hapo kila tundu la mwili linataka kuvuta na kutoa hewa sasa!
At this time wakati narudi ile nafika katikati akili ndo ikanikaa sawasawa nikalipimishia lile limti nikalidaba na kulikumbatia, kwa haraka sana nikavutwa nakuibuka haloo nilivuta hewa nafikiri waliombele yangu waliona mpk kidaka tonge cha mdomoni nacho kikishiriki kwa dhati kuvuta hewa!.

Baada ya kutolewa kwenye swimming nahema sio mchezo hata kujitambua Kama Kuna kuja na kupotea naona miguu ya watu tu iko pekupeku imenizunguka!.

Nikasikia mtu tu akisema mkamueni tumbo huyo!.

Hapo ndo nikageuza shingo kipembepembe nikajiona nakitambi cha lita kadhaa za maji!,kumbe haikuwa kitambi tu na mpesi wangu ulibaki kwenye maji hivyo nyara za taifa za kiberenge zilikuwa mubashara mbele ya hadhira iliyoniokoa!.. kwa hapo sikuona aibu maana hali ilikuwa tafrani tupu hakuna haya mbele ya janga!.

Sasa baada ya kukamuliwa tumbo na kutemeshwa maji ya swimming pool niliyoyanywa pasipo kupenda ndo akili ikanikaa sawa nakuanza kuona watu wote walionizunguka walivyokuwa wakinishangaa mimi badala ya kuyashangaa maji yaliyotaka kuniua!.

Pole zilikuwa nyingi si haba,wale wazungu waliokuwa confidence yangu nao walikuwepo wanaongea lugha gani sijui hata!.. hapo ndo nikapewa na pensi yangu nikasitiri nyara ya taifa ambayo ilikuwa imeshaonekana na jumuhia mbalimbali!.

Mpaka naondoka pale nilikuwa gumzo na kituko pia! Ule mwendo wa kijanja niliokujanao sio nilioondokanao!.

Niwahase tu ndugu zanguni ujuaji uwe na kiasi litakuja kufa jitu sikumoja.
 
FB_IMG_16598668966813387.jpg
 
Nimecheka mno nikakumbuka yangu ya Jangwani Sea breeze. Nimebaki nayatazama maji tu hivi ila yalinitoa nishai. Ilibaki kidogo nizame.

Mwalimu niliyekua nae alikua bize na demu wake. Nimemuita hata haitiki mara ya kwanza, ya pili, ya tatu nikajikaza nikamrukia ndo akajua hapa nitapoteza ndugu kisa mapenzi.

Akanikwepa ila akanifuata akanitoa. Nilibaki naogelea kule kwa watoto. Maji nayapenda ila ndo hivyo yananichenga aisee. Ila wanangu watajua kuogelea mapema kabisa. Labda wakatae wenyewe tu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka vibaya japo inasikitisha lakini uandishi wako unachochea mtu kucheka.

Pole sana ndugu yangu Kenzy.
Mimi ni muoga wa maji, nilinusurika kupelekwa maji kwani nilivuka mto kwa kushikana mikono tukiwa kikosi lakini maji yalitaka kutuzidi nguvu na yaligika juu ya kifua.

Kuna wakati nilikuta mto umefurika kiasi nilikatisha safari kwa kuhofia maji ikabidi nizunguke na gari zaidi ya kilomita 70 kuyakwepa.

Baharini kwenyewe sitaki mazoea nachezea maji yanayoishia magotini.
 
Baada ya kuyazoea kidogo nikasogea ya kina cha tumboni,baadae ya shingoni! Sasa bilinge bayoyo ndo ikaanzia hapo miguu huku chini nikaanza kuhisi kama inabebwa! Nikajiachia kikambare hapohapo ndio usaliti na maji ukanianza!.

Steps za mikono na miguu zikaanza kushindana kumbe wakati nafanya hivyo ndo nikazidi kwenda kwenye kina zaidi!.

Nikajitia u super star ati nizamie!, mzamo ukakubali kuibuka kukakataa!.

Ahahaaaaaaaa....! Pole sana. Nimechekaa sana.
 
Nimecheka mno nikakumbuka yangu ya Jangwani Sea breeze. Nimebaki nayatazama maji tu hivi ila yalinitoa nishai. Ilibaki kidogo nizame...
Muhimu kujua kuogelea ndugu hivihivi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka vibaya japo inasikitisha lakini uandishi wako unachochea mtu kucheka...
😂😂 Ahsante ndugu maji sio mkate
 
Baada ya kuyazoea kidogo nikasogea ya kina cha tumboni,baadae ya shingoni! Sasa bilinge bayoyo ndo ikaanzia hapo miguu huku chini nikaanza kuhisi kama inabebwa...
Ahsante ndugu..
 
Back
Top Bottom