SoC02 Nilivyoweza kuongeza kipato kutoka milioni 1 hadi milioni 14 kwa mwezi

Stories of Change - 2022 Competition

TheCrocodile

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2021
Posts
1,199
Reaction score
3,307
Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Mimi ni mhitimu wa degree ya masuala ya Sayansi.Miaka 6 iliyopita, nilikua nimeajiriwa sehemu ambapo nilikua nalipwa kiasi cha shilingi milioni 1 tu kwa mwezi. Sikuridhika kabisa na kipato hiki, na nilikua na njaa sana kali sana ya mafanikio.

Hivyo pale kazini nilikua mtu wa kujifunza vitu vingi sana na kwa haraka mno, ndani ya miezi 6 tu, nilikua najua vitu vingi sana na nikawa kati ya mihimili pale kazini, ilikua ni kawaida kabisa mimi kuingia saa moja kamili asubuhi na kutoka saa kumi na moja na nilikua napiga mzigo hasa.

Baada kama ya miezi 7 tangu nianze kazi, nikaanza kuomba kazi sehemu mbalimbali, ilinichukua kama miezi 5 hivi, nikapata shavu lingine, ambapo kazi mpya nilipanda mshahara mara mbili na nusu, na kuanza kulipwa milioni 2.5. Siku nimeandika e mail ya ku resign ilikua ni balaa na nusu.

Nilipigiwa simu na maboss waliokua juu yangu zaidi ya watatu kila mmoja akitaka kujua kwa nini naondoka na nini wafanye ili nisiondoke.

Jibu langu ambalo nilishaliandaa maana nilijua haya yatatokea, lilikua tu ni kwa sababu tu ya kukua kikazi na hakuna ubaya wowote, na sio kwa ajili ya ubaya wowote. Na niliwaeleza kuwa huko niendako nimepata cheo zaidi na nimekua zaidi pia kiuchumi.

Baada ya majadiliano mengi sana na marefu, hatimaye waliniachia, ila walisikitika sana na wakanitakia kila la kheri.

Baada ya kuanza kazi kampuni namba 2, mwendo ulikua ni ule ule, nilikua nachapa sana kazi na kujifunza mambo mengi sana, na hii kampuni pia ilikua na wigo mpana zaidi wa kujifunza mambo mengi kama ukiwa ni mtu mwenye hamu ya kujifunza.

Niliendelea na uchapa kazi, baada ya kuona sasa nimekusanya uzoefu na ujuzi wa kunitosha kusonga mbele, baada ya kama miaka miwili hivi nilianza kuomba kazi sehemu zingine kama kawaida yangu, ilinichukua kama miezi 7 hivi tangu nianze ku apply nikawa nimepata kazi sehemu nyingine tena. Kama kawaida, nikaandika barua ya kuacha kazi, habari ikawa ile ile ya kuitwa na kuulizwa imekuaje tena, nami jibu langu likawa lile lile kama ile kampuni ya mwanzo kuwa ni kukua tu kikazi, nikachapa zangu lapa, nikaanza kazi kampuni namba 3. Hii kampuni ya 3 niliyoingia niliingia kwa mshahara wa milioni 4.5.

Nikaingia mzigoni kama kawa. Hapa nilifanya kazi kama mwaka mmoja na miezi mitano hivi, nikawa nimepata nafasi sehemu nyingine tena kwa nafasi kubwa zaidi, na hii kampuni namba 4 niliingia kwa dau la mshahara wa shilingi milioni 7.6.

Hii kampuni namba 4 nilikua pia napiga mzigo kweli kweli.... Yaani sio mzigo wa kitoto aisee, mimi ni aina ya watu ambao wakiipenda kazi wanaifanya kutoka moyoni kweli kweli, na kama mnavyojua Watanzania wengi ni wavivu, kwa hiyo akitokea "jembe" mmoja kwenye nafasi fulani akawa anapiga mzigo, basi kazi nyingi anakua anasukumiwa huyo ambae sio mzinguaji.

Basi ndivyo ilivyokua kwangu, wenzangu ambao nilikua nao level moja ikawa kazi nyingi wanazisukumia tu kwangu, na ambae tulikua tunaripoti kwake na yeye kwa sababu pia alikua anaona akinipa kazi naifanya vizuri na kwa wakati kuliko wengine, kazi nyingi pia akawa ananitupia mimi, ikiwa pia na baadhi ya kazi zake yeye, akibanwa basi ananitupia tu mimi. Hii ilinipa faida moja kubwa sana, nilijikuta najifunza vitu vingi na vikubwa sana ndani ya muda mfupi mno, japokua ilinifanya kuwa na kazi nyingi sana.

Kwa sababu bosi wangu alikua kwenye nafasi za juu, ile kunipa baadhi ya majukumu yake ikanipa ujuzi na uzoefu adimu sana wa kiuongozi.

Fitna za hapa na pale kama mnavyojua tena sehemu za riziki hazikosekani, yakaanza maneno kuwa jamaa anapendelewa sana, hivi na vile. Ila yule bosi wangu aliniambia, usijishughulishe na majungu, wewe piga kazi utafika mbali sana.

Basi, imepita kama mwaka na miezi 5 hivi, sina hili wala lile, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni moja hivi kanicheki LinkedIn paaap...!! Akaniuliza tu utakua interested kwa nafasi fulani hapa kwetu, kuna mtu ameku recommend kwangu kwa hii nafasi, na nimeangalia profile yako nimeona utatufaa, kama uko tayari nikuunganishe na HR apange siku ya usaili tukusikilize. Na hiyo nafasi aliyoisema ni nafasi kubwa, sio ndogo.

Moyo ukashtuka sana, ila nikasema sawa, niko tayari ku explore hiyo nafasi. Akasema sawa haina shida, baadae HR wao akanicheki, akanipangia usaili wiki inayofuatia.

Nikapiga raundi 5 za usaili ndani ya miezi miwili, na bila kutarajia nikawa nimefaulu usaili na kupata hiyo nafasi, ambayo ndio naitumikia hadi sasa, ambayo mshahara wake ni Shilingi za Kitanzania milioni 14, na marupurupu kibao (posho ya nyumba laki 5, posho ya mafuta laki 5, posho ya mawasiliano laki 2). Kumbuka kuwa nina degree moja tu hadi sasa (Bachelor), na classmates wangu hakuna hata mmoja ambae amefikia level ya nafasi niliyonayo pamoja na kwamba wengi tayari wana Masters.

Kufanya kazi kwa bidii kubwa na kuipenda kazi unayoifanya kunalipa sana. Vijana mlioajiriwa msijibweteke, pigeni kazi na kujifunza mambo kwenye kazi zenu kila siku, ila usikae sana sehemu moja muda mrefu, kwani kuna uwezekano wa kuzoea kazi na hivyo kutojifunza lolote jipya.Unakuta kijana kakaa kampuni moja ya binafsi miaka 5 sijui 8 au wengine 10+. Unatafuta nini? Hapo unakua huna jipya tena, unaenda kazini kupasha moto siti tu wala huna jipya lolote.

Pia, msiogope kuwa risk takers hata ukiwa umeajiriwa, usiache kuomba kazi sehemu zingine kila mara kwani kila unapohudhuria usaili ni nafasi ya kujinoa zaidi makali yako sokoni na kujiuza zaidi. Msishau pia "kuji-brand", mimi ukiona profile yangu ya LinkedIn ni hatari namna ilivyo, mtu akiingalia tu anajua huyu yupo serious na anaipenda kazi yake.

Mwisho, hakikisha unaondoka kwenye kampuni huku kila mtu akiwa anatamani kuwa ungeendelea kubaki, na si kinyume chake.
 
Upvote 102

Degree ya nini?
 
Hongera sana mtoa mada mimi nipo upande wako kwa 100% kila kitu ulicho andika hapo ni ukweli mtupu.

mimi nipo katika ulimwengu huo ambao upo kwenye uo uzi na nimeshukuru sana kuusoma huu uzi maana kuna maboss zangu nawajua wanapewa more than 20m+ per month.

Mimi nipo level ya chini sana yaani kiufupi safari yangu ndio inaanza na mwanga nauona maana saivi nipo kwenye kampuni ya pili.

Ninacho kitaka ni story yangu iendane na yako ili namimi nije kutoa ushubuda mbele za watu kwanzia muda huu saa 03:04 usiku kuna kitu kimebadirika ndani ya maisha yangu kupitia ili andiko lako na kwa kuonyesha kuguswa na hili andiko ntalishapisha ili liwe linanipa moyo na nguvu ya kuchapa kazi.

Asante sana [emoji1666] kwa kunionyesha mwanga hakika nitakuja kusimulia namimi siku nikilipwa 20m+ , God Bless you [emoji120]
 
😳Huu ni uzi kwa ajili ya wale ambao wameajiriwa hasa katika sekta binafsi kwa ajili ya kuwatia moyo wa kukuza uchumi wao.

Ya kwel haya???
 
Asante kwa mtazamo wako. Uzuri sina control na mtazamo wako, huo ni utashi wako binafsi. Natamani ningeweka screenshot za mikataba yote hapa. Endelea tu kutoamini.

Uko field gani?Kwa maelezo yako nimehisi ni IT related...
 
Nadhani hii ni chai bab kubwa..kwa degree gan ya vyuo vya bongo ukalipwe hata mil7 tu labda ungekua kwenye nchi za western au USA..acha huo umotivation speaker watu wamevurugwa. Labda utuambie kwanza una profession ipi tuanzie hapo
 
Hongera sana mtoa mada mimi nipo upande wako kwa 100% kila kitu ulicho andika hapo ni ukweli mtupu.

mimi nipo katika ulimwengu huo ambao upo kwenye uo uzi na nimeshukuru sana kuusoma huu uzi maana kuna maboss zangu nawajua wanapewa more than 20m+ per month.

Mimi nipo level ya chini sana yaani kiufupi safari yangu ndio inaanza na mwanga nauona maana saivi nipo kwenye kampuni ya pili.

Ninacho kitaka ni story yangu iendane na yako ili namimi nije kutoa ushubuda mbele za watu kwanzia muda huu saa 03:04 usiku kuna kitu kimebadirika ndani ya maisha yangu kupitia ili andiko lako na kwa kuonyesha kuguswa na hili andiko ntalishapisha ili liwe linanipa moyo na nguvu ya kuchapa kazi.

Asante sana [emoji1666] kwa kunionyesha mwanga hakika nitakuja kusimulia namimi siku nikilipwa 20m+ , God Bless you [emoji120]
Karibu mkuu
 
Nadhani hii ni chai bab kubwa..kwa degree gan ya vyuo vya bongo ukalipwe hata mil7 tu labda ungekua kwenye nchi za western au USA..acha huo umotivation speaker watu wamevurugwa. Labda utuambie kwanza una profession ipi tuanzie hapo
Kuamini au kutoamini ni suala lako. Kama hauamini ni sawa.
Lakini huo ndio uhalisia. Thamani yako unaitengeneza wewe mwenyewe.
 
Duuuhh..!! Mkuu, ni vyema ungechukua muda wako kujifunza zaidi:
1.Kuna personalities za aina nyingi sana kwenye corporate world- Wapo wahamaji wazinguaji na wapo wahamaji ambao wanapiga kazi vizuri tu. Kwanza kitendo cha kuhama tu lazima uwe vizuri, usifikiri kuhama ni rahisi tu,kwamba unaamua tu na it happens, lazima uwe vizuri maana kuhama kuna involve competition kubwa kwenye interview process, so mtu anaehama sana most times anakua vizuri tu, fanya uchunguzi wako utaelewa.
2.Sasa nakwambia nalipwa that amount, ans I am not even among the top paid people kwenye corporate world. Kuna watu wanalipwa more than that amount, again, do your research utaelewa. You are very mis-informed on this mkuu.
3.Huo ni mtazamo wako, na siwezi kupinga perception ya mtu, ni haki yako ya kimsingi.
Ni sawa hatukatai kijana lakini mishahara inaendana na development ya nchi husika. Kwa tanzania mshahara juu ya 10 mil inahitajika uwe specialist au manager au CEO sasa wewe kwa MD yako ulipwe hivyo kwani umespecialize kwenye nn labda tuanzie hapo basi maana hiyo ni mishahara specialist?
 
Kuamini au kutoamini ni suala lako. Kama hauamini ni sawa.
Lakini huo ndio uhalisia. Thamani yako unaitengeneza wewe mwenyewe.
Wewe ni MD kama MD wengine bwana acha kutuletea motivation zisizo na uhalisia. Huna specification au ujuzi specific tena unadegree tu hakuna bosi chizi wa kukulipa hivyo taaluma yako hairuhusu
 
Hata enterview hauitwi wewe acha chai na ndoto za alinacha
 
Ni sawa hatukatai kijana lakini mishahara inaendana na development ya nchi husika. Kwa tanzania mshahara juu ya 10 mil inahitajika uwe specialist au manager au CEO sasa wewe kwa MD yako ulipwe hivyo kwani umespecialize kwenye nn labda tuanzie hapo basi maana hiyo ni mishahara specialist?
Sija specialize kwenye chochote, ni MD tu. Sina Masters yoyote.
Again, kuamini au kutokuamini ni juu yako, na kama huamini ni sawa pia. Mishahara haswa huku sekta binafsi haiko fixed, inategemea na value unayoleta, na namna ulivyoji brand hivyo ni kawaida kabisa kukuta mtu mnalingana kwa title, lakini anakuzunguka mshahara mara mbili.
Kutokuamini kwako hakunipunguzii kitu. Lakini, kama ukiamini na ukafanyia kazi mawili matatu kujiboresha thamani yako, ingeweza kukunufaisha zaidi.
Nakutakia usiku mwema.
 
Wewe ni MD kama MD wengine bwana acha kutuletea motivation zisizo na uhalisia. Huna specification au ujuzi specific tena unadegree tu hakuna bosi chizi wa kukulipa hivyo taaluma yako hairuhusu
Usipende sana kutolea frustrations zako sehemu ambazo si sahihi. Hasira zako kwenye hii post hazikusaidii. Mimi sio sababu ya shida zako.
 
Back
Top Bottom