Nilivyozama kwenye chember ya choo kuokoa mtoto wa adui yangu

Nilivyozama kwenye chember ya choo kuokoa mtoto wa adui yangu

Umefanya jambo la kiungwana,ubarikiwe.
Jirani siku zote ni zaid ya ndugu lkn sisi binaadam baadhi tumejawa na selfish.
Nashauri msamehe tu,Mungu anakulipa hapa na ahera,hata kama yeye hajakushukuru.

Endelea kua mwema Kwa wote binadam,wema hauozi.
Umesema cha muhimu sana.ni kweli kabsa mkuu
 
Tukio hilo limetokea kwasababu maalum ya kuondoa uadui baina yenu. Mwenyezi MUNGU ni mwema, kwenye kila tukio ipo sababu. Wewe uwe msamehevu na mnyenyekevu baadaye yeye ndio atajiona mjinga na ujirani mwema utarejea. Usiwe na kiburi baada ya yeye kujirudi
Nkweli kabisa Mkuu.nipo nae sasa na tunacheka kama mwanzo.nimefurahi sana.maaana alikua swaiba wangu sana
 
hongera sana kwa wema wako yani kuna mijitu cjui ikoje Nina jirani yangu nae anavitabia vya kiselfish
Ni tabia ya ajabu sana hiyo Mkuu.ni vile hatujui ya kesho.nikipatwa na matatizo wa kunisaidia ni nan kama sio jirani yangu.inakera sana
 
Asante Mkuu.ntafanya hivyo

Jana jioni nikiwa nimetoka kwenye shughuli zangu,ghafla akanikimbilia msichana wa Kazi Wa jirani yangu kuomba msaada .Alikuja mbio analia mtoto katumbukia kwenye chamber ya kinyesi.Watoto wakati wanacheza sijui ikawaje mfuniko huenda waliosogeza au palikua wazi.Nilipo fika kuchungulia na kumuona mtoto na maji hayakua mengi nikaruka mpaka chini cha kufanya ilikua nimnyanyue mtoto wakati tunatafuta msaada wa kupata cha kupandia juu.kwa kua maji hayakua mengi nikafanikiwa kumnyanyua nikamuhimiza msichana wa Kazi atafute kamba haraka au mbao ndefu aishushe .wajinga wale sijui wanakulaga moto au mabomu.niliungua kwa kinyesi.nikafanikiwa na kumpa huduma ya kwanza nakumpeleka hospitali.
Sasa baba wa mtoto alikata mawasiliano na Mimi nilipomkataza asibandike mabango yake ya kampeni kwangu kipindi cha uchaguzi .akasema kuanzia siku hiyo nitakua adui yake.baada ya kumpeleka mtoto nadhani alipigiwa simu .nikakutana njiani akanipita bila salamu.
Sasa badae amekuja kujua ndio niliyomuokoa mwanae kaja mbio analia.nimeondoka bila kumsemesha kwanza .nifanye nini ili kumpa adabu?
Kumbe yote wakorofi ila mna utu , hongera kwa kua binadamu mwema, ila msameheane tuu.
 
Mwambie aendelee kukuhesabu kama adui yake tu maana hukumuokoa yeye ila ulimuokoa mtoto kwa wema wako na ubinadamu Mungu aliekujalia.
Nimemsamehe Mkuu.Leo kwake yamempata kesho yanaweza nipata zaidi ya take.
 
Back
Top Bottom