Niliwahi kuchomwa sindano ya kichaa cha Mbwa.

Niliwahi kuchomwa sindano ya kichaa cha Mbwa.

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2015
Posts
23,372
Reaction score
54,943
Tuachane na yaliyopita huko mwanzo ila asilimia 80 ya habari zile zilikuwa ni habari za kweli ambazo zimetokea katika mzunguko wa maisha yangu.

Nadhani mnakumbuka niliwahi kuokoa Simba asiuwawe na wananchi huko kanda ya ziwa kwa sababu alikuwa anakula mifugo ya wananchi hadi ikafikia hatua wananchi wakaanza kumuwinda ila nikifanikiwa kuokoa maisha yake.

Nikiwa na bibi yangu mpenzi ambae amenilea sana (nakuombea maisha marefu sana bibi yangu) niliwahi kwenda machungani nikiwa pekee yangu na pindi jua lilipokuwa linaelekea kuzama matarajio ya wengi walikuwa wanajua nitakuwa karibu kurudi ila hali haikuwa vile.

Hadi saa mbili sijarudi na sababu ni kulala nikiwa malishoni na mifugo yote ikapotea na sikujua ilipo hivyo nilivyoamka nilijikuta niko pekee yangu hakuna ng'ombe kondoo wala mbuzi. Nikaanza kubabaika kuwasaka na juhudi zangu zikagonga mwamba. Kutokana na utoto wangu nikaona nibaki porini ili nisiende kukutana na vitasa vya bibi yangu siku ile.

Kumbe ng'ombe walienda wakala mashamba ya watu na baadae kurudi nyumbani kama saa moja hivi kwa mujibu wa maelezo ya bibi, baada ya mifugo kurudi waliifungia zizini na kuanza kunitafuta huko porini na wakweli kwa mbali nilianza kuona mwanga wa tochi na nikaufuata nilikuta ni yule mjomba wangu wa Italia na mdogo wake wakiwa na panga na rungu wananitafuta.

Mjomba aliniuliza nini tatizo mbona huna mifugo nikamwambia kuna mbwa kichaa kanitimua huko porini nikaacha mifugo na hapa naitafuta. Mjomba aliuliza kama nimepata madhara yoyote yale kuhusiana na ule mkasa wa uongo. Nilikwambia nilikimbia na hakufanikiwa kunikamata.

Mjomba alinichukua hadi kwa daktari mmoja pale kijiji alikuwa na duka la dawa na kumtaka anidunge sindano ya kichaa cha Mbwa, nilikubali kuwa mjinga na kupigwa sindano ya kichaa cha Mbwa.
 
Back
Top Bottom