Niliwahi kuidukua simu ya Ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua. Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia

Daa rafiki yangu niliwahi kufanya nae kazi. Yeye pia alifanya jambo hilo kwa mpenzi wake aliyehamishiwa kikazi dodoma yeye akiwa Dsm. Lakini ikifika wikiend wanakutana hadi pale alipoona dada kaanza kubadilika sasa akafanya huo mchezo wa kudukua simu. Akagundua dada ana mtu mwingine tena wanashiriki kabisa uzinzi kula na kupakua. Kumbuka walikuwa wanaenda steji ya ndoa. Dada akapata mimba ya mchepuko wake wa dodoma na wakakubaliana na mchepuko mimba apewe rafiki yangu. Basi dada alipokuwa akija dar jamaa anasema kaenda kikazi pemba. Jamaa si anasoma na kusikia na kuona picha ya mipango yako, dada amekuja dar mara kadhaa jamaaa anamkwepa tu dada akaamua kuitoa mimba baada ya kuona itakuwa kubwa. Mambo yote hayo jamaa anayadukua tu yuko kimya tu. Sasa dada katoa mimba alafu analalamika kwa ndugu wa rafiki yangu Kuwa jamaa hamjali kwa hiyo ndugu wakawa wanamsema rafiki yangu maana dada anaaminika sana maana ni mpole uwezi amini. Kwa kuwa jamaaa alikuwa anamkwepa dada kila uchao ndugu wakaamua kuitisha kikao ili wajue jamaa anatatizo gani . Dada akaja siku ya kikao na alikuwa anajuwa kabisa atashinda kesi maana ndugu hasa mama wa familia alikuwa anampenda sana. Sasa saa chache kabla ya kikao dada alikuwa yuko jikoni na mama mkwe wake wanaandaa chakula na mambo mengine kwa ajili ya kikao jamaa akachukua simu yake akampa mdogo wake wa kike ampe yule dada aisome kabla kikao hakijaanza yule dada alisoma meseji. Baada ya hapo alimka na kuondoka hajawahi kuonekana tena.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]duhhhhhhh

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sms itakuwa ilkuwa kubwa sana
 
....una haki ya u-Legend ulionao mkuu.!
 
Movies hizi duùuu.....basi sawa ...andaa script uza Bongo movies
 
Uwe na roho ngumu kwelikweli Mimi nlishawahi kufanya huo upuuzi ila nafkir ni kipindi kile Cha foolish age. Nlkuwa na wasap mbili kwenye cm yangu Moja yake Moja yangu bila yeye kujua na before alkuwa anatumia wasp so nlipoirudisha ni kama wale jamaa walikuwa wanachat nae walifurahi kuona namba imerudi online [emoji1787] nilikutana na advertise Moja kwnza ikanikata wenge nkataman kuifuta Ile wasap sijakaa sawa nkakutana na nyingine na nyinginezo nkasema huu ni ujinga nkafuta Ile namba wasap alaf nkam face nkamchana yote akakubali akakiri akaomba msamaha nkaendelea kula mzigo mana sijamuoa hanipi pressure
 
Hayo mambo mabaya kabisa...

Kuna maneno utatamani yasiwepo tena kwenye dictionary.
Kuna style hutapenda uzisikie tena.
Kuna sehemu hutataka kuziona wala kupita hapo. ..


Kutokana na jinsi yalivyotumika na mwizi wako [emoji23][emoji23]
 
Jamaa
Anapambamia nini Sasa wakati anapigwa na matukio kibao ?

Demu baada ya lile tukio akaomba waachane,,

Jamaa bado akajikaza amuache demu,,
Siku demu anakuja na kirikuu kusomba vyombo vyake jamaa kazuia tena kirikuu isiondoke...

Jamaa dhaifu sn.
Jamaa fala sana, na hapo demu ndo anasimamia shoo kwa uzaifu wa jamaa
 
Yani mkuu hata kwao hawajui yupo wapi mpaka leo??
 
Hiyo ndio ile maana ya wazaramoo"mwanakulitafuta mwanakulipata"😂😂
 
Sio mkurya na sitoi sababu ya kunipiga
Wengi hawajui Mana ya mwanamke na anahitaji Nini kwa mwanaume. Yaani hajui yeye Ni kiumbe anayetakiwa kulindwa na mwanaume Kama vile Mtoto alindavyo. Mwanao hawezi enda mahala bila ya kujua akaenda wapi ndipo anapopata Mana ya kuwa anajaliwa Fulani.
Yaani kumjali mtu Ina Mana ya kuwa anajulikana anapoenda anachofanya kila wakati so akiwa yeye ana feel needed,secured,guided, watched,Kama unavyojali hela zako ujue zinafanya kitu gani. Yaani mwanamke anapenda mpaka ujue harufu ya mwili wake,nguo yake,harufu za nguo zake,hata nguo zake zote,matendo yaani kwa kifupi umuweke kichwani na umuwaze kila wakati umfanye kipaumbele chako yaani ukipata huzuni ama furaha umueleze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…