Niliwahi kuidukua simu ya Ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua. Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia

Niliwahi kuidukua simu ya Ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua. Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia

Kuna jamaa yangu ye alikua na dem wake ambae alikua tayari kashamzalisha na alikua na mpango wa kumuoa. Akamleta dem kwao ili azoeane na mawifi na wakwe zake kabisa katika kuelekea ndoa. Jamaa ni mtu wa kusafiri safiri, baada ya kumleta dem kwao akawa amesafiri tena. Siku amerudi(kwa alivyohadithia) alijikuta kaona achukue tu simu ya dem akague kague(alikuaga hajawai kabisa kufanya hivyo) alichokutana nacho kilivunja mipango yote. Jamaa anakwambia dem namna anavyochat na wanaume wengine ni kama yupo singo, wakati yupo kwenye process za kuelewa. Jamaa alishindwa kabisa kuelewa
 
Uzi huu nimeuandaa baada ya kusoma post flani inatrend jukwaani muda huu kuna dada yetu anahisi mme wake anatumia ushirikina kujua mawasiliano yake ya watu anaoongea nao, Huenda ni kweli lakini kisa hiki kimenikumbusha mbali sana kwamba labda mme wake katumia mbinu niliyowahi kuitumia zamani kwa ex wangu kwa kumnunulia simu mpya ambayo niliidukua kisha kumzawadia. Enzi hizo ilikuwa rahisi sana kudukua simu ila kwa siku hizi sijajua, sijafatilia na wala sina hamu.

Ilikuwa ni miaka ya 2015 hivi, nilikuwa na girlfriend wangu ambae niliingia tamaa ya kutaka kumpeleleza zaidi, alikuwa ni kisu haswa.

mimi ni fundi seremala lakini mambo ya teknolojia napendaga sana kuyafatilia tangu zamani hivyo nilishawishika kumdukua simu yake.

Nilijaribu kudukua smartphone yake lakini ilikuwa na ulinzi imara kuzidi uwezo nilionao so ikabidi nizame mfukoni nikaenda kumnunulia simu used kali kimtindo ambayo nilishaifanyia uchunguzi naweza kuidukua.

Niliidukua kirahisi wala haikunipa shida, step ya kwanza ilibidi nipate access ya mafaili yote ya simu hata yale ya ulinzi ambayo hayaonekani, hapa nilifanya zoezi linaitwa "rooting" ili kudhoofisha ulinzi wa simu ifanye nachotaka. Baada ya hapo nikaweka sasa mtambo wangu ambao ni app, enzi hizo ulikuwa unaitwa android lost nikaongezea na vikorombwezo vya ziada.

Huo mtambo ni kwamba ukiuweka kwenye simu, unaweza kutumia laptop ama simu nyingine kuona meseji zote za simu uliyoidukua, call logs zote hata zikifutwa, unaweza kufungulia maiki mda wowote kunasa sauti, simu inaweza kupiga picha mda wowote uone mazingira, kucheki chats za whatsapp, n.k.

Nilijiona mjanja sana ila kilichotokea ni maumivu tu.

Kwa vile dem alikuwa ni pisi kali, zile meseji za hi sweety, hi mrembo, n.k. zilikuwa hazikauki hata iwe ni mtu waliezoeana kawaida tu, hizi mesej zilikuwa zinanifanya nijawe na wivu na hasira sana.

Wapo jamaa walikuwa ni ving'ang'anizi balaa, wanapiga saundi hadi nakosa amani, si mnajua tena huu ulimwengu wenye simu, hata asipotoa wataipata kwa marafiki. Nikwambie tu ya kwamba mwanamke kutongozwa ni jambo la kawaida sana.

Wivu wangu ulizaa hasira za kutaka kumlinda zaidi, hii ilisababisha kila muda niwe nafatilia sehemu anazokwenda kimya kimya akitoka nje ya chuo, mtambo ulikuwa na uwezo kuonyesha alipo na ruti zake na mda aliokaa hio sehemu, hata hivyo alikuwa ni mtu wa kukaa sana chuoni ila akitoka kwenda sehemu ambayo si gheto kwangu niliingia wivu wa kwenda kupachunguza.

Kelele na ugomvi vilianza pindi nilipooana kuna chats za ex wake ama kuna sehemu kaenda ambayo nina mashaka nayo, sikumwambia nimedukua simu yake ila nilikuwa namwambia kuna watu wameniambia, Nilikuwa na wivu uliopitiliza.

Siku niliyochapiwa !!

Ni siku ambayo walimaliza mitihani yao ya muhula, kuna jamaa nahisi ni class mate wake walienda nae geto kwake, siku hio hata simu yake ilikuwa haipatikani, sasa kesho yake asubuhi ndio kawasha simu, kwenye mtambo naona jamaa anamtumia mesej, vp umerudi salama chuoni, leo uje tena, n.k. jamaa akahamia kuanza kuzungumzia yaliyotokea jana yake, akaanza kuzungumzia mnyanduano wa jana yake, anaomba irudiwe sometimes kwa kiingereza mfano "babe am horny i need a few more pumps to fix the situation", wajaribu style mpya, ex nae anamtania alipiga kimoja basi nae jamaa anajitetea mitihani ilimchosha ana nguvu mpya kumpiga vitatu, n.k. iliniuma sana jamani, kidume hadi machozi yalikuwa yananilenga lenga. Mda wote huo moja kwa moja mawazo yananijia kwamba jamaa kanizidi ufundi na huenda ana mkuyenge mkubwa kunizidi, aish! Dah! Sio poa jamani nyie sikieni tu yani niliumia sana yani.

Huwezi amini nilijifanya sijui chochote, nikampigia simu ex aje, ex alivyo mshenzi ndio kwanza aliniletea zawadi ya t-shirt na akawa anazuga jana simu yake ilikuwa na matatizo flani. (nimeyasahau ).

Nikamkalisha kitako na kumwambia jana umenichiti na nikamwambia nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa hapo chuoni kwao kanipa A - Z wa usaliti ulionifanyia, nilimtajia hadi jina la huyo jamaa waliekuwa nae jana, alipiga magoti na kulia sana na kuomba msamaha akaanza visingizio sijui shetani kampitia machozi kama yote analia, nadhani wengi mnajua kipaji walichonacho wanawake kwenye kulia, Kwa upande wangu nilikuwa nimeumia sana kwamba kuna jamaa kamcharaza mkwaju, Very painful na hasira kwa juu.

Nilimtolea uvivu kuna vinguo nguo na kibegi alikuwa nacho hapo gheto vya siku akija kwangu nikavifungasha ovyo ovyo nikamrushia hicho kibegi aondoke mara moja, alikuwa mbishi nami hasira zimenipanda nilimtandika vibao vya nguvu sana kama vitatu hivi timua nje kabisa nikafunga mlango, uzuri hio siku nilikuwa peke yangu hakuna wapangaji wengine.

Nilikuwa nafatilia mesej zake kwa wiki hivi huku nikiwa na maumivu, alikuwa anapiga sana simu ikabidi namba yake niliblok asinipigie, hivyo alikuwa anatumia simu za rafiki zake ila nikigundua sauti yake nakata, kwenye mtambo naona alikuwa anapitia kipindi kigumu alikuwa anachat na marafiki zake juu ya break up, kuomba ushauri, wanamliwaza, n k. kiukweli niliona kajutia nami nilihisi pengine kweli kashetani kalimpitia ila maumivu niliyokuwa nayapata kila nikiwaza alivyonisaliti ni kama kisu kikali kimegonga mfupa, yule jamaa aliemtafuna jana nilikuwa naona kafura analalamika dem hajibu text wala kupokea simu bila kujua msala uliotokea huku, mda ulienda niliacha hata kumfatilia nikafuta huo mtambo maana ulikuwa unanifanya nimuwaze badala ya ku move on.

that was the end.
“Mtambo”
 
Kuweka kidukuzi kufuatilia mawasiliano ya simu kwa mpenzi wako,,unayempenda sana,,
kunataka uwe na roho ngumu haswa,,
Vinginevyo utakuja kuaibika mwishoni.

Kuna rafiki yangu fulani alikuwa na msichana wake ,,
ambaye alikuwa anampenda sn ,,
hata kwa kuangalia mapenzi yao kwa macho tu,
jamaa alikufa na kuoza kwa yule msichana mwanachuo..
jamaa alimpenda Sana yule demu..

Baada ya jamaa kupigwa sn matukio na yule demu Kwa muda mrefu,,
Akaamua adukuwe mawasiliano ya mchumba wake,,
Basi sms pamoja na calls zote msichana akipigiwa na jamaa nae anazipata tena bila msichana wake kujuwa.

Siku Moja msichana akaaga atatoka kwenda chuo,,
Jamaa akamruhusu atoke lakini awahi kurudi,,
Yote hayo jamaa ni ktk kutaka kujikaza kiume,,
Lakini alikuwa anajuwa kila kitu demu wake anakwenda kwa msela kupigwa mbupu,,
Lengo lake ni kutaka kumkamata Kwa ushahidi akiwa na yule msela.

Demu kaita bodaboda,,,jamaa kuona bodaboda imefika,,,demu wake yupo juu ya bodaboda,,
Jamaa uzalendo ukamshinda akazuia bodaboda isiondoke.
Jamaa akaanza kupaza sauti Kwa kelele hata kujaza mtaa mzima,,
"Najuwa Kila kitu kwamba unakwenda kwa jamaa.."
Jamaa akaanza kulia kabisa mbele ya demu ,
"Nini umekosa kwangu"

Ikawa vurugu tupu...
Huwezi amini pamoja na matukio yote hayo,,Bado jamaa amemuoa hyo demu na ana watoto nae 2 tayari.
Ila amejiapiza kutodukuwa tena simu ya mkewe,,
Japokuwa bado hamuamini.
Mapenzi ni kitu kingine kabisa, haha.
 
Miaka ya nyuma, Yupo jamaa yangu alidukua simu ya gf wake single maza mmoja hivi, kumbe huyo dada alikuwa anaendelea kumpea baba mtoto.

Nakumbuka siku hiyo jamaa alikuwa anatembea tu hasimami, anataka aende kwa demu akakinukishe, nikimshika ananirushia ngumi.

Hakuna kitu kinaumiza kama mapenzi.
Acha kabisa mkuu.
 
Hii michezo ilinifanya kumkamata demu akiingiza njemba geto kwangu kwa kuzuga kuwa dadaake anakuja kumtembelea na atapenda afikie geto kwake. Tulikuwa tunaishi pamoja kiunyumba kama kawaida ya mchezo wa wanachuo ili kujihakikishia all time supply ya utelezi.

Nikaona nimpe chance alale na ndugu yake, kufuatilia convo kwenye tambo kumbe kuna njemba ilikuwa inaandaliwa shoo! Nlichokifanya nikawahi eneo la tukio nikabana chocho nikishuhudia chezo lote hadi njemba inaingizwa geto. Baada ya njemba kuingia tu nkavuta pumzi nkaenda kushika kitasa mara demu anafungua haamini kama ni mimi ndio nmemfumania.

Jamaa alikuwa ndo anaandaliwa maji ya kuoga chumba knanukia maua rose balaa, sitakaa nisahau ile siku. Bila demu kukimbia leo ningekuwa selo nanyea debe.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii michezo ilinifanya kumkamata demu akiingiza njemba geto kwangu kwa kuzuga kuwa dadaake anakuja kumtembelea na atapenda afikie geto kwake. Tulikuwa tunaishi pamoja kiunyumba kama kawaida ya mchezo wa wanachuo ili kujihakikishia all time supply ya utelezi.

Nikaona nimpe chance alale na ndugu yake, kufuatilia convo kwenye tambo kumbe kuna njemba ilikuwa inaandaliwa shoo! Nlichokifanya nikawahi eneo la tukio nikabana chocho nikishuhudia chezo lote hadi njemba inaingizwa geto. Baada ya njemba kuingia tu nkavuta pumzi nkaenda kushika kitasa mara demu anafungua haamini kama ni mimi ndio nmemfumania.

Jamaa alikuwa ndo anaandaliwa maji ya kuoga chumba knanukia maua rose balaa, sitakaa nisahau ile siku. Bila demu kukimbia leo ningekuwa selo nanyea debe.
Hahahaha dah
 
Back
Top Bottom