Niliwahi kuidukua simu ya Ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua. Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia

Niliwahi kuidukua simu ya Ex wangu kwa kumzawadia simu niliyoidukua bila yeye kujua. Nilichokitafuta nilikipata na siwezi tena kurudia

Acha kuwa mariooo, huoni aibu kujisifia kulelewaa?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Silelewi namaisha yangu mazuri tu, ambayo vijana wengi wanatamani kuyaishi, lakini Mzee alininyang'anya demu wangu, nilikubali coz nilikuwa mlalahoi enzi hizo nabado maisha yangu sio mazuri kivile, lakini pia sio mabaya nikiangalia nilipotoka.

Kuhusu Dem nilimpenda na nilijitoa Kwa uwezo wangu wote,ndio maana baada yeye kunipiga chini lakini ananikubali mpaka kesho na ntaendelea kumtafuna tu.

Haina namna.
 
Uzi huu nimeuandaa baada ya kusoma post flani inatrend jukwaani muda huu kuna dada yetu anahisi mme wake anatumia ushirikina kujua mawasiliano yake ya watu anaoongea nao, Huenda ni kweli lakini kisa hiki kimenikumbusha mbali sana kwamba labda mme wake katumia mbinu niliyowahi kuitumia zamani kwa ex wangu kwa kumnunulia simu mpya ambayo niliidukua kisha kumzawadia. Enzi hizo ilikuwa rahisi sana kudukua simu ila kwa siku hizi sijajua, sijafatilia na wala sina hamu.

Ilikuwa ni miaka ya 2015 hivi, nilikuwa na girlfriend wangu ambae niliingia tamaa ya kutaka kumpeleleza zaidi, alikuwa ni kisu haswa.

mimi ni fundi seremala lakini mambo ya teknolojia napendaga sana kuyafatilia tangu zamani hivyo nilishawishika kumdukua simu yake.

Nilijaribu kudukua smartphone yake lakini ilikuwa na ulinzi imara kuzidi uwezo nilionao so ikabidi nizame mfukoni nikaenda kumnunulia simu used kali kimtindo ambayo nilishaifanyia uchunguzi naweza kuidukua.

Niliidukua kirahisi wala haikunipa shida, step ya kwanza ilibidi nipate access ya mafaili yote ya simu hata yale ya ulinzi ambayo hayaonekani, hapa nilifanya zoezi linaitwa "rooting" ili kudhoofisha ulinzi wa simu ifanye nachotaka. Baada ya hapo nikaweka sasa mtambo wangu ambao ni app, enzi hizo ulikuwa unaitwa android lost nikaongezea na vikorombwezo vya ziada.

Huo mtambo ni kwamba ukiuweka kwenye simu, unaweza kutumia laptop ama simu nyingine kuona meseji zote za simu uliyoidukua, call logs zote hata zikifutwa, unaweza kufungulia maiki mda wowote kunasa sauti, simu inaweza kupiga picha mda wowote uone mazingira, kucheki chats za whatsapp, n.k.

Nilijiona mjanja sana ila kilichotokea ni maumivu tu.

Kwa vile dem alikuwa ni pisi kali, zile meseji za hi sweety, hi mrembo, n.k. zilikuwa hazikauki hata iwe ni mtu waliezoeana kawaida tu, hizi mesej zilikuwa zinanifanya nijawe na wivu na hasira sana.

Wapo jamaa walikuwa ni ving'ang'anizi balaa, wanapiga saundi hadi nakosa amani, si mnajua tena huu ulimwengu wenye simu, hata asipotoa wataipata kwa marafiki. Nikwambie tu ya kwamba mwanamke kutongozwa ni jambo la kawaida sana.

Wivu wangu ulizaa hasira za kutaka kumlinda zaidi, hii ilisababisha kila muda niwe nafatilia sehemu anazokwenda kimya kimya akitoka nje ya chuo, mtambo ulikuwa na uwezo kuonyesha alipo na ruti zake na mda aliokaa hio sehemu, hata hivyo alikuwa ni mtu wa kukaa sana chuoni ila akitoka kwenda sehemu ambayo si gheto kwangu niliingia wivu wa kwenda kupachunguza.

Kelele na ugomvi vilianza pindi nilipooana kuna chats za ex wake ama kuna sehemu kaenda ambayo nina mashaka nayo, sikumwambia nimedukua simu yake ila nilikuwa namwambia kuna watu wameniambia, Nilikuwa na wivu uliopitiliza.

Siku niliyochapiwa !!

Ni siku ambayo walimaliza mitihani yao ya muhula, kuna jamaa nahisi ni class mate wake walienda nae geto kwake, siku hio hata simu yake ilikuwa haipatikani, sasa kesho yake asubuhi ndio kawasha simu, kwenye mtambo naona jamaa anamtumia mesej, vp umerudi salama chuoni, leo uje tena, n.k. jamaa akahamia kuanza kuzungumzia yaliyotokea jana yake, akaanza kuzungumzia mnyanduano wa jana yake, anaomba irudiwe sometimes kwa kiingereza mfano "babe am horny i need a few more pumps to fix the situation", wajaribu style mpya, ex nae anamtania alipiga kimoja basi nae jamaa anajitetea mitihani ilimchosha ana nguvu mpya kumpiga vitatu, n.k. iliniuma sana jamani, kidume hadi machozi yalikuwa yananilenga lenga. Mda wote huo moja kwa moja mawazo yananijia kwamba jamaa kanizidi ufundi na huenda ana mkuyenge mkubwa kunizidi, aish! Dah! Sio poa jamani nyie sikieni tu yani niliumia sana yani.

Huwezi amini nilijifanya sijui chochote, nikampigia simu ex aje, ex alivyo mshenzi ndio kwanza aliniletea zawadi ya t-shirt na akawa anazuga jana simu yake ilikuwa na matatizo flani. (nimeyasahau ).

Nikamkalisha kitako na kumwambia jana umenichiti na nikamwambia nimepata taarifa kutoka kwa mtu wa hapo chuoni kwao kanipa A - Z wa usaliti ulionifanyia, nilimtajia hadi jina la huyo jamaa waliekuwa nae jana, alipiga magoti na kulia sana na kuomba msamaha akaanza visingizio sijui shetani kampitia machozi kama yote analia, nadhani wengi mnajua kipaji walichonacho wanawake kwenye kulia, Kwa upande wangu nilikuwa nimeumia sana kwamba kuna jamaa kamcharaza mkwaju, Very painful na hasira kwa juu.

Nilimtolea uvivu kuna vinguo nguo na kibegi alikuwa nacho hapo gheto vya siku akija kwangu nikavifungasha ovyo ovyo nikamrushia hicho kibegi aondoke mara moja, alikuwa mbishi nami hasira zimenipanda nilimtandika vibao vya nguvu sana kama vitatu hivi timua nje kabisa nikafunga mlango, uzuri hio siku nilikuwa peke yangu hakuna wapangaji wengine.

Nilikuwa nafatilia mesej zake kwa wiki hivi huku nikiwa na maumivu, alikuwa anapiga sana simu ikabidi namba yake niliblok asinipigie, hivyo alikuwa anatumia simu za rafiki zake ila nikigundua sauti yake nakata, kwenye mtambo naona alikuwa anapitia kipindi kigumu alikuwa anachat na marafiki zake juu ya break up, kuomba ushauri, wanamliwaza, n k. kiukweli niliona kajutia nami nilihisi pengine kweli kashetani kalimpitia ila maumivu niliyokuwa nayapata kila nikiwaza alivyonisaliti ni kama kisu kikali kimegonga mfupa, yule jamaa aliemtafuna jana nilikuwa naona kafura analalamika dem hajibu text wala kupokea simu bila kujua msala uliotokea huku, mda ulienda niliacha hata kumfatilia nikafuta huo mtambo maana ulikuwa unanifanya nimuwaze badala ya ku move on.

that was the end.
Kufikirikaaaaaa zaidii uhalisia...tembeza bahasha kgaki tafuta kazi.....
 
Hii michezo ilinifanya kumkamata demu akiingiza njemba geto kwangu kwa kuzuga kuwa dadaake anakuja kumtembelea na atapenda afikie geto kwake. Tulikuwa tunaishi pamoja kiunyumba kama kawaida ya mchezo wa wanachuo ili kujihakikishia all time supply ya utelezi.

Nikaona nimpe chance alale na ndugu yake, kufuatilia convo kwenye tambo kumbe kuna njemba ilikuwa inaandaliwa shoo! Nlichokifanya nikawahi eneo la tukio nikabana chocho nikishuhudia chezo lote hadi njemba inaingizwa geto. Baada ya njemba kuingia tu nkavuta pumzi nkaenda kushika kitasa mara demu anafungua haamini kama ni mimi ndio nmemfumania.

Jamaa alikuwa ndo anaandaliwa maji ya kuoga chumba knanukia maua rose balaa, sitakaa nisahau ile siku. Bila demu kukimbia leo ningekuwa selo nanyea debe.
Mnawatoaga wapi mademu wa hivyo?😂
Au ndio Vile Ndege wanaofanana
 
Nilitry hii kitu juzi kati aaahhh kmmmk kama una moyo mdogo unaweza jikuta unafukiwa chini au upo ICU au pengine upo jela unasubiri hukumu tu....

Vitu nilivyoviona vilizidi kuniongezea umakini na kuamini ya kua hakuna mwanamke mwaminifu karne hii, hata kama atakaza sana kuna muhuni mmoja tu ata muotea na atamkunja kila styles.
 
Nilitry hii kitu juzi kati aaahhh kmmmk kama una moyo mdogo unaweza jikuta unafukiwa chini au upo ICU au pengine upo jela unasubiri hukumu tu....

Vitu nilivyoviona vilizidi kuniongezea umakini na kuamini ya kua hakuna mwanamke mwaminifu karne hii, hata kama atakaza sana kuna muhuni mmoja tu ata muotea na atamkunja kila styles.
Ulitumia app gani?
 
Sasa si ulipata ulichokitaka ila ina uma sana haswa kwa wewe uliewekeza hapo😅
 
Kuweka kidukuzi kufuatilia mawasiliano ya simu kwa mpenzi wako,,unayempenda sana,,
kunataka uwe na roho ngumu haswa,,
Vinginevyo utakuja kuaibika mwishoni.

Kuna rafiki yangu fulani alikuwa na msichana wake ,,
ambaye alikuwa anampenda sn ,,
hata kwa kuangalia mapenzi yao kwa macho tu,
jamaa alikufa na kuoza kwa yule msichana mwanachuo..
jamaa alimpenda Sana yule demu..

Baada ya jamaa kupigwa sn matukio na yule demu Kwa muda mrefu,,
Akaamua adukuwe mawasiliano ya mchumba wake,,
Basi sms pamoja na calls zote msichana akipigiwa na jamaa nae anazipata tena bila msichana wake kujuwa.

Siku Moja msichana akaaga atatoka kwenda chuo,,
Jamaa akamruhusu atoke lakini awahi kurudi,,
Yote hayo jamaa ni ktk kutaka kujikaza kiume,,
Lakini alikuwa anajuwa kila kitu demu wake anakwenda kwa msela kupigwa mbupu,,
Lengo lake ni kutaka kumkamata Kwa ushahidi akiwa na yule msela.

Demu kaita bodaboda,,,jamaa kuona bodaboda imefika,,,demu wake yupo juu ya bodaboda,,
Jamaa uzalendo ukamshinda akazuia bodaboda isiondoke.
Jamaa akaanza kupaza sauti Kwa kelele hata kujaza mtaa mzima,,
"Najuwa Kila kitu kwamba unakwenda kwa jamaa.."
Jamaa akaanza kulia kabisa mbele ya demu ,
"Nini umekosa kwangu"

Ikawa vurugu tupu...
Huwezi amini pamoja na matukio yote hayo,,Bado jamaa amemuoa hyo demu na ana watoto nae 2 tayari.
Ila amejiapiza kutodukuwa tena simu ya mkewe,,
Japokuwa bado hamuamini.
Hahahahaha
 
Mtu hujamuoa unamdukua wa nin? Hata kumfumania mtu unatakiwa uwe na cheti cha ndoa kama hujamuoa sio wako
Moja ya ukatili nilishuhudia ni mwamba m'moja tukiwa chuo, alienda kumfumania demu wake. Jamaa kaenda kagonga mlango mwenye chumba akafungua.

Jamaa akamwambia amwambie demu atoke nje. Jamaa akawa anashangaa nani huyu ananiamrisha kwangu na demu wangu.

Demu alishajua fumanizi limekamilika na jamaa yake ameshamkamata bila ubishi na ushahidi wa wazi mara kadhaa. Na inaonekana demu alishaona kama vipi waachane ila mwamba hakubali kuachia anamtaka sana demu.

Demu akasogea mlangoni ambapo jamaa alikuwa kasimama akafungua mlango. Neno la kwanza akamwambia mshikaji "Unataka nini"?

Jamaa akapangawa, mori ikampanda akauliza,"we malaya unaniambia mimi nataka nini". [emoji23][emoji23][emoji23] Macho yashakuwa mekundu kwa hasira na mauchungu.

Demu akamwambia "ndio nakuuliza unataka nini unaleta fujo kwenye nyumba za watu"

Wakawashiana moto demu akamwambia jamaa live sikutaki katafute mwanamke mwingine mimi wangu huyu hapa.

Mwamba akawa amefura balaa hana la kusema hasira zimemjaa kifuani, yaani hadi huruma. Yule mshikaji mwenye sehemu alipokuwapo demu amesimama tu kimya maana akashajua yeye ana advantage kubwa na demu amemchagua. Demu akawa nae kapandisha akamwambia jamaa ondoka, jamaa anamwambia ndio naondoka malaya wewe utaishia kut*mbw* na kuachwa na kubadilisha wanaume.

Demu huku anatoa kicheko cha kejeli akamwambia ndio me ni mwanamke kut*mbw* ni kawaida nenda katafute na wewe wa kut*mb*[emoji23][emoji23][emoji23].

Akamshika jamaa akaanza kumkiss mbele ya mwamba, halafu anamwambia haya ondoka bwana tupishe sisi tukat*mban*.

Aisee ikabidi tumsihi jamaa aondoke maana kuendelea kukaa pale angefanya mambo ya ajabu.

Jamaa alivurugwa akawa kama mgonjwa wa maralia iliyopanda kichwani. Alikuja kukubali matokeo baadae sana.

Ila nina uhakika ile kitu ilimuachia kovu kubwa sana moyoni na atakuwa anamuombea kila balaa yule demu wake baada ya pale.
 
Software ipi hiyo mkuu maana kuna manzi 1 nataka nimbwage kwa kumtegea mtambo? Ni kifaa lakini nataka nikiache tu
Sasa kama mtu ameshakupa ishara kuwa ana mambo meusi why unataka kuchunguza na unajua kuwa outcome itakuwa ni kumjua au kuwajua anao ruka nao. Why usimwambie tu kuwa mwenendo wake haukufurashi unataka amani achague kubadilika au umpe uhuru wake.
 
Back
Top Bottom