Niliwahi kutoa wazo kama hili kwenye mkutano wa kijiji, watu wakaishi kucheka. Sasa natoa mfano!

Niliwahi kutoa wazo kama hili kwenye mkutano wa kijiji, watu wakaishi kucheka. Sasa natoa mfano!

Watu wanasemaga hesabu nitatumia wapi? Hapa sasa hesabu za kutafuta ujazo wa mcheduara ndiyo zinahusika.
Yeah, hesabu inatumika katika harakati za kila siku. Na hapa ilikuwa lazima nijue nachimba urefu gani na diameter gani ili nipate lita elfu hamsini.
 
mkuu ERoni, una akili sana aisee umenipa hamasa zaidi!

nina hekala 4 ambazo nataka zipate maji kila siku msimu hadi msimu.
unaonaje nipunguze litres?
Lita milioni moja itakugharimu pesa ndefu sana kujenga, kama eneo unaloishi maji ya chini hayapo mbali sana ni heri ukachimbiwa kisima tu. Maji ya kuvuna itakugharimu hela ndefu na huenda usiweze kupata hizo lita milioni. Kwanza angalia kiwango cha mvua katika eneo lako, pili ukubwa wa bati la nyumba yako, lakini pia kujenga kisima cha ukubwa huo utaalam unahitajika, sio lele mama.
 
Habari za wakati huu expert mwenzangu[emoji4]
siku moja nitauliza ni kwanini tunaitwa "experts"
isije kuwa ni maexperts wa kuandika nyuzi[emoji23][emoji119]

..mnaokaa karibu na bahari, maziwa na mito, jamani mungu awape macho, hiyo ni fursa.

ninaishi sehemu ambayo upatikanaji wa maji ni shida sana, kwahyo nawaza na kuwazua jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hii.

wazo:
kwa sababu nipo nje ya mji,eneo kubwa nk, nataka ninunue cement ya kutosha, nijenge tank ambalo litahifadhi maji angalau lita mil. 1 (one million litres of water) na nitahakikisha linajaa kabla msmu wa mvua haujaisha..
lengo nipate maji ya kutosha kumwagilia bustani zangu.
maana
ninapata matokeo hasi kwa kutegemea mvua zisizoeleweka.
niko serious kabisa. Nataka niwaonyeshee mfano walionicheka, naamini hii wataipenda tu[emoji4]

rafiki yangu hapo, unasemaje/ unauonaje mpango huu?[emoji4]
unaweza kuniongezea wazo au maarifa zaidi?

karibu sana
Unalosema liliwahi wastaajabisha wazungu.
Kuna sehemu moja huko karagwe walikuja wazungu kutembelea shule ya karaseco. Sasa baadaye wakawa wanapita kwenye vijijj huko na mvua ikanyesha kubwa. Jambo la kushangaza mvua ilipokoma wakaona wanakijiji na ndoo na madumu wanaenda kutafuta maji kwasababu nyumba zao ni za nyasi hata kukinga maji ya mvua ilikuwa shughuli.
Maji sasa wanapokwenda kuchota ni kama dimbwi.
Ikabidi waje na project kama hiyo ya kwako ya kukusanya maji ya mvua na kuyahifadhi.
Walistaajabu mbona inayesha mvua ya kutosha lakini bado maji ni shida.
 
Tank/shimo la lita 1,000,000 ni kubwa sana. Ni sawa na tank za lita 1,000 ziwe 1,000 au tank za lita 10,000 ziwe 100.

Gharama ya kujenga hilo tank/shimo ni kubwa sana, unahitaji materials nzuri kuliimarisha na ufundi madhubuti wenye usimamizi wa kitaalam kabisa. Otherwise utakuwa unalifanyia ukarabati kila msimu.

NB: Nina shimo la lita kama 50,000, linajaa kwa maji ya bati tu, tena mvua zikinyesha kubwa mara tano linafurika. Likijaa situmii maji ya dawasa, nililijenga kipindi hakukuwa na maji, ila linanisaidia hadi leo maji ya dawasa yakiwepo.
Dimension zake zikoje
 
wazo zuri sana hili! niliwahi kuwatafuta hao jamaa wanaodrill visima wakaniambia malipo milioni kumi

asante sana mkuu sayoo nitalinganisha gharama na faida
Gharama ya kisima bado iko chini sana, sababu kwa ujazo huo wa 1,000,000lt (1000cub mt) unahitaji tank lenye urefu wa 30mt upana wa 15mt na kina cha 2.3mt.
Ujenzi wa tank lenye vipimo hivyo unahitaji zaidi ya 130cbm za zege ambazo kila moja si chini ya 200k. Utahitaji zaidi ya tani5 za nondo @2,700k. Utahitaji mbao kwa ajili ya formwork ya kuta za zege, Utahitaji kemikali maalum kuzuia uvujaji wa maji (waterproofing materials), ongeza na labourcharge.
Pia tank litakupa gharama kubwa ya kusambaza maji kufikia kila kona ya shamba, wakati kwa gharama ya chin unaweza kuchimba hata visima vinne katika kona tofauti za shamba zikapunguza gharama ya mtandao wa usambazaji.
 
Dimension zake zikoje
Kipenyo cha shimo(mduara) = 3.4m or radius=1.7m
Urefu wa shimo = 5.5m
Ujazo kwa mita za ujazo= 50m³ or 50,000L

Kanuni, V= 3.14r²h

Ukiwapa mafundi hivi vipimo unapata exactly 50m³ au pungufu/nyongeza kidogo.
 
Gharama ya kisima bado iko chini sana, sababu kwa ujazo huo wa 1,000,000lt (1000cub mt) unahitaji tank lenye urefu wa 30mt upana wa 15mt na kina cha 2.3mt.
Ujenzi wa tank lenye vipimo hivyo unahitaji zaidi ya 130cbm za zege ambazo kila moja si chini ya 200k. Utahitaji zaidi ya tani5 za nondo @2,700k. Utahitaji mbao kwa ajili ya formwork ya kuta za zege, Utahitaji kemikali maalum kuzuia uvujaji wa maji (waterproofing materials), ongeza na labourcharge.
Pia tank litakupa gharama kubwa ya kusambaza maji kufikia kila kona ya shamba, wakati kwa gharama ya chin unaweza kuchimba hata visima vinne katika kona tofauti za shamba zikapunguza gharama ya mtandao wa usambazaji.
Lita milioni kwa kuchimba shimo ni gharama kubwa sana, ni heri akachimba kisima tu.
 
Mkuu naona kama utatumia gharama kubwa sana aisee, Cha msingi chimba kisima tu , pia tafuta solar pannel za kutosha na betttery uwezo mkubwa , utazalisha umeme mwingi tu ambao utakusaidia kuvuta maji ya kisima na utapata maji mengi tu kwa ajili ya matumizi yako ya Kila siku
Hata Mimi ningemshauri hivi. Tena kipindi hiki cha mvua za hapa na pale, ndio kipindi kizuri Kwa kuchimba kisima.
 
Habari za wakati huu expert mwenzangu[emoji4]
siku moja nitauliza ni kwanini tunaitwa "experts"
isije kuwa ni maexperts wa kuandika nyuzi[emoji23][emoji119]

..mnaokaa karibu na bahari, maziwa na mito, jamani mungu awape macho, hiyo ni fursa.

ninaishi sehemu ambayo upatikanaji wa maji ni shida sana, kwahyo nawaza na kuwazua jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hii.

wazo:
kwa sababu nipo nje ya mji,eneo kubwa nk, nataka ninunue cement ya kutosha, nijenge tank ambalo litahifadhi maji angalau lita mil. 1 (one million litres of water) na nitahakikisha linajaa kabla msmu wa mvua haujaisha..
lengo nipate maji ya kutosha kumwagilia bustani zangu.
maana
ninapata matokeo hasi kwa kutegemea mvua zisizoeleweka.
niko serious kabisa. Nataka niwaonyeshee mfano walionicheka, naamini hii wataipenda tu[emoji4]

rafiki yangu hapo, unasemaje/ unauonaje mpango huu?[emoji4]
unaweza kuniongezea wazo au maarifa zaidi?

karibu sana
Mkuu nikupongeze kwa kuwa na wazo la kufanya mapinduzi kwenye kilimo kwa kufanya kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, binafsi naomba nikupe wazo mbadala katika kufikia lengo lako.
Binafsi nakushauri kwakuwa imeonekana pesa sio tatizo, ni vyema ukachimba kisima kirefu ambacho kitakuwa na uhakika wa kukupatia maji msimu mzima wa mwaka na kisha ununue tank lenye ujazo wa 10,000/=ltrs.
Hii ni kwa sababu utaingia gharama mara moja tu wa kuchimba kisima husika na gharama za kupandisha maji kwenye tank ni himilivu kuliko kuingia gharama kujenga tanka kubwa halafu utokee uhaba wa mvua mwisho hata hilo tank utaliona ni useless.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
wazo zuri,una kipato cha kuweka nondo za kutosha?
 
Back
Top Bottom