Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,610
Najua wote hamjambo na pia mnaelewa vizuri kuhusu ugumu wa kupata kazi kwenye kitengo cha vinywaji kwenye sherehe hasa harusi kubwa kubwa na zenye kuhusisha watu wakubwa.
Mimi sema kweli nimewahi kuwa mkuu wa kitengo cha Vinywaji harusini ni ngumu kuwa katika hicho kitengo bila kutazamwa uaminifu wako katika hiyo kazi. Ilikuwaje nikawa mkuu wa kitengo hicho nyeti yaani (Chief manager of Liquid and alcohol).
Mwaka 2011 nikiwa naendelea na shughuli zangu za kilimo nilipata simu kutoka kwa mwanakijiji mwenzangu akiuliza uko wapi? Nikamwambia nalima huku shambani kwangu akanitaka niende haraka kwao watu wamegawana vitengo mimi nipo tu sijui hili wala lile!
Kumbe yule mwanakijiji alikuwa na ndugu yake ambaye ni mtoto wa binamu wa mjomba wake aliyekuwa mjini na ameleta mpenzi wake nyumbani kutambulishwa kwa ndugu na jamaa na majirani. Kwangu na kwao si mbali ila wananiita jirani kutokana na ukarimu wangu wa kumpenda kila mtu. Basi nilitoka shambani nikakimbia kuelekea kule nilipoitwa na kukuta watu wengi wanaongea kuhusu ugeni huo na namna ya kutambulisha mwanamke huyo nyumba moja baada ya nyingine.
Nilipofika nikaulizwa kama najua majina ya vinywaji tofauti na Pepsi, Mirinda, Fanta na Coca nikasema najua, hivyo wakaniteua kuwa mkuu wa kitengo cha Vinywaji na idara yote ile chini yangu, nilifurahi sana na nikampigia simu mama yangu akanipongeza na pia wadogo zangu hata waliopo shule niliwaambia na wakanitakia mafanikio mema, niliondoka pale na usafi wa pikipiki maana yule kijana aliyekuwa analeta mpenzi wake kutambulishwa alisema nisiende nyumbani kwa miguu nipande pikipiki.
Nikapanda pikipiki napita mtaani watu hawaamini kama nimepanda pikipiki kwenda nyumbani na wakati huo kijijini nikawa naitwa mkuu wa kitengo, mimi nilikuwa natabasamu tu hata siongei maana nilitaka nikifika nyumbani ndipo nifurahi na kucheka. Basi nikaenda nyumbani majira ya saa 12 nikaomba yule dereva awashe taa ili waone naenda nyumbani kwa pikipiki.
Tukafika nyumbani nikiwa nimelowana mwili mzima na jasho linatoka siamini kama kweli mimi ndiye nitakuwa natoa vinywaji stoo na nikisema sitoi basi wote hawapati, mama alichinja kuku nikala na nikawahi kuoga siku hiyo na kulala mapema na hata simu nikazima ili isije ikaishia chaji.
Siku moja kabla ya harusi nikaitwa na yule jamaa aliyetoka mjini akanipa hela nyingi niende na dereva wa pikipiki tununue vinywaji vingi na vya aina mbalimbali, basi nilinunua vinywaji vingi na vingine sikuvijua na kuweka kwenye stoo usiku baada ya kufika. Nililala palepale ili kuhakikisha kuwa vinywaji viko salama na nikapiga simu nyumbani walete nguo zangu na viatu.
Asubuhi siku ya harusi nilikuwa mtu wa kwanza kuvaa vizuri pale na watu wakaanza kunishangaa nikiwa na miwani yangu pia na nikaanza kufanya kazi ila vinywaji vilikuwa havitoki hadi umalize kula. Basi saa 7 mchana nikaitwa na Bwana harusi kwenye Mic. Naomba Chief wa vinywaji aje, nikaenda na ilikuwa mara ya kwanza kuitwa kwenye mic nikaenda na kuniambia gawa vinywaji watu wanywe.
Nikaanza kugawa watu wakawa wanakunywa soda, juice, pombe nyingi ile ya uefa na ile pombe nyingine ya caf huwa inaonekana kwenye mechi za caf hata wakati Simba anacheza Misri walikuwa wanaionesha hiyo pombe. Vinywaji vile hawakuvijua nilivinunua mimi pekee yangu bila kuuliza vinaitwaje majina kwa wengine.
Tukalewa sana vijana wengine wakawa wanaona wivu mimi kuwa kwenye kitengo kile ila nikasema mtetezi wangu yu hai siwezi kudhurika kwani mimi nilikuwa na ujanja kidogo kuliko wao nilikaa Dar miaka 3 hivyo nilikuwa na ujanja sana.
Sherehe ikaishia vizuri nikaaminiwa na watu nikawa nafanya kazi kule kijijini nikawa maarufu kwenye harusi.
Sent using Jamii Forums mobile app