Niliweka shada za maua kwenye makaburi matano ya watu wangu wa karibu

Sehemu ya Saba:

Sisi binadamu mwisho wetu ni nini kama sio kifo? Tutaruka turukavyo, twende tuendapo lakini mwisho wa siku makutano yetu ni pahali pamoja, napo si kwingine bali kaburini. Hili halijalishi hadhi wala cheo. Alimradi umezaliwa basi tayari muda wako wa kwenda umeshatiwa muhuri, kinachongojewa ni utelekezaji tu. Bwana ametoa na bwana ametwaa.

Maneno hayo yalinipatia faraja moyoni mwangu, nilikuwa nikiyatamka mwenyewe moyoni, kwenye kiti cha daladala, nilipokuwa nikielekea hospitali kule nilipopewa taarifa mbaya.

Niliyawaza mengi hapo njiani, mojawapo ni endapo nikipewa wasaa wa kusema neno ni nini nitaeleza, hapo ndo' nikaanza kujisema na kujitengenezea mwenyewe kauli na kauli, sijui akili yangu ilikuwa inawaza nini muda huo, saa hii ndo' naona ulikuwa ni ujinga tu, pengine ugeni wa misiba ulikuwa unanizuzua.

Mambo ya kutoa risala na mimi wapi na wapi?

Kwa mara ya kwanza, nilimwona Mgaya akiwa na macho mekundu ya uchungu, uchungu wa kumpoteza mama yake, japo sababu ni mwanaume alijikaza sana kumwaga chozi, kuna muda nilikuwa namwona aking'ata meno yake kwanguvu, sijui ni nini ila kitu kile, katika namna ya ajabu kabisa, kilinifanya moyo wangu kuwa wa bariidi kwa raha.

Kweli maisha ni mbio za vijiti, kukimbia na kupokezana zamu, jana yake ilikuwa ni mimi nikisaga meno kitandani, nararuka na moyo wangu mwenyewe, leo hii asubuhi zamu ya wengine, kijiti hakipo mikononi mwangu tena.

Bwana Mgaya, kwa uso ulolemewa na majonzi, alinambia yale yalotukia huku nyumbani baada ya mimi kuondoka kwenda shule.

Bwana huyo alimngoja mama yake atoke chumbani kwaajili ya kupata kifungua kinywa lakini mama hakutoka, hio haikuwa kawaida yake kukawia kiasi hiko chumbani kwani tangu amjue mama yake, hata akiwa aumwapo, ni mtu wa kuamka mapema kwenda kuota jua la asubuhi labda tu akiwa hajiwezi, na hilo ndo' lilimtisha.

Akiwa nje pamoja na Amiri, wanatazama ustawi wa mifugo, alitazama mara kwa mara pale nje kama atamwona mama yake lakini dakika zilikata asimwone katika upeo wa macho yake, hapo sasa akakata shauri kwenda kutazama.

Aliita mbele ya mlango ule ulokuwa wazi, mlango wa chumba alalacho mama yake, mara tatu kwa sauti kubwa lakini hakujibiwa, aliporusha macho yake ndani aliona mwili wa mama yake umetuama juu ya kitanda kana kwamba kisiwa katika bahari, mwili hauchezi wala kujigusa.

Upesi akamwita Amiri wakasaidiana kuubeba mwili huo mpaka kwenye gari na kutimka haraka hospitali, njia nzima mama hakusema kitu wala hakuomba hata maji, kufika hospitali haikupita hata dakika kumi, daktari akawaambia hamna mtu pale bali uwakilishi wake wa mwili tu.

Baada ya maelezo hayo, nilimkumbatia Mgaya kumpatia pole, nikasema maneno yangu ya faraja kwenye masikio yake, maneno ambayo angependa kuyasikia toka kwa mkewe, lakini maneno yale yalijawa na unafiki mtupu, hakuna hata moja nililomaanisha, walosema moyo wa mtu kichaka hawakukosea kabisa, hapa moyo wangu mimi ulikuwa pori kabisa.

Tena pori lenye giza totoro.

Watu wetu wa karibu, wale ambao wapo katika mkoa wa Dar na maeneo ya jirani, walifika nyumbani kutupatia pole kwa msiba ule. Walimu wenzangu walifika kunishika mkono wakiwa wanaongozana na meneja bwana Salum.

Miongoni mwa walimu hao alikuwamo Beatha. Mwanamke huyo ndiye alinikabidhi rambirambi ya walimu wenzangu kwa pamoja, alinipatia kama mwakilishi wa darasa lile ambalo mimi na yeye tunafundisha.

Lakini mbali na hapo, meneja Salum alinipatia pesa binafsi kutoka mfukoni mwake, kiasi cha kama laki mbili hivi ndani ya bahasha, akinambia itanisaidia kwenye safari ya kwenda na kurudi kwenye mazishi.

Pesa hiyo alinipatia kando, mbali kidogo na waombolezaji wengine, nami kwasababu hiyo niliitia pesa hiyo mahali pangu pa siri, sikutaka mtu mwingine ajue. Baada ya siku moja, tulisafirisha mwili kwenda Iringa, huko tukamzika mama yule mimi nikiweka shada kubwa juu ya kaburi lake, shada lililoandikwa kwa herufi kubwa - MAMA

Niliweka shada hilo machozi yakinishuka, sikufahamu kama nina uwezo mkubwa wa kuigiza kiasi kile, tabu ile ilinifanya nikatambua nina kipaji ndani yangu.

Baada ya mazishi, pale nyumbani kulifanyika kikao kidogo cha familia, bwana Mgaya pamoja na ndugu zake kujadiliana kuhusu mambo kadha wa kadha ukizingatia mama yule ndo' alikuwa mzazi pekee alobakia, baba yao alikwishafariki kitambo hata kabla sijaolewa na bwana Mgaya.

Katika kikao hicho kilichokuwa kinasimamiwa na kuongozwa na kaka mkubwa wa familia yao, bwana Mgaya alitambulika kama mume mwenye wake wawili, mimi na yule Momo alokuwepo pale.

Na katika mengi waliyojadiliana na kuafikiana katika kikao hicho, mojawapo lilikuwa ni la bwana Mgaya kuondoka na mkewe pale nyumbani kwani mama aliyekuwa anamuuguza hayupo tena.

Nilipokuja kuelezwa swala hilo na bwana Mgaya, sikuliafiki katukatu, sikuwa radhi nalo na nilimwambia bwana Mgaya mwanamke huyo ataingia ndani ya nyumba yangu mimi nikiwa mfu lakini si kwa uhai wangu huu.

Swala hilo likapelekea tafarani sana, sasa bwana Mgaya hakutaka kuonekana dhaifu mbele ya ndugu zake, kitendo cha maamuzi kufikiwa na kikao cha familia kisha yeye kushindwa kutimiza alikiona ni kama fedheha, tena fedheha zaidi kwa maana mwanamke ndo' amemshinikiza, ataambia nini ndugu zake? Mwanamke amempanda kichwani?

Tulipishana sana maneno hata kufikia mimi na mwanangu kuondoka wenyewe kurudi nyumbani, niliondoka hata pasipo kuaga. Nilipofika nikapokelewa na Amiri akinitua begi langu na kunipa pole ya msiba.

Baada ya siku mbili tangu nirejee ndo' bwana Mgaya akajileta nyumbani kama kifaranga kilichomwagiwa maji, mikono nyuma kama bwana mshauri, uso umeparwa na haya hawezi hata kunitazama usoni.

Nami, kama hakuna kilichotokea, sikuhangaika naye. Niliendelea na shughuli zangu tukisalimiana kama wapita njia mitaa ya mjini. Mwishowe, bwana huyo aliniangukia akiniomba msamaha kwa yalotokea. Alinitaka nitulie naye tujenge familia na nyumba yetu kama tulivyokuwa tunafanya hapo awali.

Kuhusu Momo, Mgaya alinieleza mwanamke yule amemrejesha nyumbani kwao, hayuko naye tena, na anachoshukuru mwanamke huyo amerejea kwao akiwa hana mtoto wala ujauzito wake.

Bila hiyana nikayaamini maelezo yake, sikuwa na budi nyingine, maisha yakarejea katika hali yake ya kawaida, hali ya amani, amani ambayo ililetwa kwa udhamini wa kifo cha yule mama mkwe. Kifo chake kilikuwa ni kama sadaka ya kutuliza tafarani ya familia muda ule.

Niliwasiliana na rafiki yangu Zai, sikuwa nimeonana naye muda kidogo kwani hata kwenye msiba hakufika sababu alikuwa anaumwa, hakuwa yuko sawa, alipewa 'bed-rest' hospitali fulani baada ya kuonekana anasumbuliwa na presha, hivyo nilivyorejea nilimpa taarifa kuwa nimerudi na tukakubaliana niende kumwona majira ya jioni kesho yake baada ya kutoka shuleni.

Kesho yake niliporejea shuleni baada ya siku zile chache za maombolezo, nilikuta shule nzima ina habari kuhusu pesa ile nilopewa kwa siri na meneja Salum.

Kumbe siku ile, mimi na meneja, hatukuwa peke yetu kama tulivyodhania, kuna macho ya wenye husda yalituona na kisha midomo ya wambea ikaenda kutenda kazi ya kusambaza taarifa, na hapa sikumdhania mtu mwingine isipokuwa Beatha. Hamna mtu mwingine bali yeye.

Hata nilipofika, alinikarimu kinafki akisema, "naona mke wa boss umewasili." Nami sikuhangaika naye nikaendelea na shughuli zangu, nilishakubali ana utindio wa ubongo hivyo kuhangaika naye niliona ni kujidhalilisha tu, kumbe pia kukaa kwangu kimya kukawa kunamuumiza, ama kweli hasidi hakosi sababu.

Kabla ya siku hiyo kuisha, nilionana na meneja Salum kwaajili ya kumshukuru.

Tuliongea naye mambo kadhaa, kama dakika kumi tu, kabla ya kumuaga na kwenda zangu kufungasha ili nielekee hospitali kuonana na Zai.

Nikiwa nafungasha, mara nikapata wito wa kufika ofisi ya mkuu wa shule mara moja. Ujumbe huo ulifikishwa kwangu na mwanafunzi mmoja wa madarasa ya juu, nami pasipo hiyana nikauitikia wito huo upesi ili nisikawie na ratiba yangu.

Ajabu nilipofika huko, nikakutana na malalamiko kwenye meza ya mkuu wa shule, Madam Bibiana, ya kwamba mimi nimekuwa nikipuuzia mamlaka yake pale shuleni.

Madam yule alinikumbusha ya kwamba kuna utaratibu wa kimamlaka kwenye taasisi yoyote ile na ni makosa kwa mwalimu kwenda kuonana na meneja moja kwa moja kana kwamba mhudumu wa mgahawani, kama kuna lolote linalonisibu basi natakiwa nianzie kwake kwanza kabla ya kugonga mlango wa meneja.

Hapo nikakumbuka yale matamko ya meneja kuhusu mimi kupunguziwa majukumu, lakini pia mawasiliano yangu naye kuhusu urefu wa likizo yangu ya uzazi, kumbe yote yale yalikuwa ni makwazo?

Nilimkubaliana mwanamke huyo kwa kila alichoongea maana nilikuwa na haraka zangu, hata mengine aloyaongea sikuyasikia vema, akili yangu haikuwepo hapo, nilipotoka tu humo ofisini nilinyookea moja kwa moja hospitali kumwona mgonjwa kabla muda haujanitupa mkono.

Bahati nilifika ndani ya muda. Nilimkuta Zai akiwa anaendelea vema kabisa hata akaniambia muda si mrefu ataondoka hapo hospitalini punde tu akikamilisha kulipia bili yake, kuna pesa fulani anaingoja atumiwe.

Tuliongea pale, mambo ya hapa na pale, tukielezana kwa uchache yale yalotukia wakati hatujaonana, kuanzia ya msiba mpaka yale ya kule Iringa, alipoyasikia hayo akacheka sana kwa songombingo zangu ila mwishowe akanipa pole akisema hayo ndo' maisha na changamoto zake.

Lakini kabla sijamuaga niende zangu, aliniuliza swali, swali ambalo lilifanya nikameza mate kwa ukavu wa koo langu.

Alisema;

"mara ya mwisho umeongea na Anwari lini?"

Nikasita kujibu, akatambua nimekwama, akanitazama kwa macho ya 'mwana mpotevu' kisha akasema kwa stara: "niambie ukweli, Magreth. Mimi ni rafiki yako."

Kwenye kufikiri kwangu, nikaona ni vema kukanusha taarifa ile. Mimi nilikuwa naamini hata rafiki yangu wa undani kabisa ni lazima awe na mipaka yake, si kila kitu ni cha kumshirikisha mtu, binadamu ndimi mbili, huwezi jua ni lini mambo hayo unayomjaza yatakuja kugeuka kuwa silaha ya kukuangamiza wewe mwenyewe. Nguruwe hukaangwa na mafuta ya mwilini mwake.

Hivyo,

Nikakataa, nikasema sikumbuki mara ya mwisho lini kuwasiliana na bwana huyo. Hapo Zai akatoa simu yake na kunionyesha ujumbe, ujumbe toka kwa Anwari, ujumbe mrefu uliokwangua sakafu ya moyo wangu na kuniachia majeraha.

Kwenye ujumbe huo Anwari alimlalamikia Zai ya kwamba ananitafuta sana hanipati hewani. Amefanya kila jitihada za kuniona lakini Zai hataki hata kumwambia sehemu yangu mpya ya kazi achilia mbali makazi yangu, sasa amechoka, kama sitaki kuonana naye basi angalau nimpe haki ya kumwona mwanae.

Hapo kwenye mwanae ndo' palitibua mzunguko wangu wa damu, nikahisi kizunguzungu na tumbo kunivuruga. Niliona kitanda cha hospitali kinaenda kaskazini kisha kinarudi kusini kwa haraka, ikanibidi nishike kingo zake kwanguvu kisije kikanivamia na kunilaza chini.

Na huo ndo' ukawa mwanzo mpevu wa safari ya kifo cha Anwari.

***
 
Mkuu endelea weka episode mbili mbili
 
Dr Restart njoo Mkuu.

Duh, baada ya Mama Mkwe anayefuata ni Anwari sasa. Baadae atafuata Zai na kisha Bwana Mgaya huku Mwanga Amiri akihitimisha idadi ya watu watano.

Au Madam Beatha naye yumo kwenye list? Momo je? Tusubiri tuone.

SteveMollel twashukuru kwa Story tamu na ya kusisimua. Ila Mkuu, ngoja ngoja ya kipindi kirefu chaumiza 'Hippocampus' kukumbuka yaliyopita.

Dr Restart tuendelee kushtuana Mkuu.
 
Back
Top Bottom