Hello guys, natumai mnaendelea vema.
Kwa upande wangu wiki hii na ile ilopita hazikuwa nzuri sana kwani wiki ilopita tulikuwa tunapambana na kuuguza na wiki hii tulikuwa tunapambana na msiba wa mama yangu mkubwa, mwanamke aliyenilea na kunienzi kama mtoto wa kutoka tumboni mwake na hivyo sikumtambua kwa kumuita mama mkubwa bali mama kama mama.
Amesumbuliwa vibaya mno na sukari pia presha, tukahangaika hospitali ya Kitengule, Lugalo kisha Muhimbili na hatimaye kuhamishiwa Mloganzila ambako ndipo alipofia.
Nashukuru tumemaliza salama shughuli ya msiba hapa Mbezi beach, tukasafiri salama kwenda Kilimanjaro alipozikiwa na tumerudi salama hapa Dar.
Zilikuwa ni siku 'tough' lakini hakuna kinachodumu, nazo zilipita.
Samahani kwa kuwakwaza popote pale, haikuwa kusudi langu. Nami sijabeba kebehi wala shutuma zozote kutoka humu ndani maana usilolijua litakusumbua, na nafahamu sisi watu ni wazuri sana kwenye kutoa hukumu tusijue tunatofautiana viatu tunavyovaa.
Pasaka njema.