Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Big alikuwa anatutisha Hadi Kwa mbali.....Kuna siku nilihisi ananichungulia dirishani, nikaweka pazia vizuriHivi kati ya Amiri na Big nani mnoma?, binafsi Big alikua anafanya naogopa kusoma story nikiwa pekeangu room hasa nyakati za usiku
Thank you bae
Karibu 🥰🥰Thank you bae
Leo akiongeza 2 episodes itakua vizuriNilikua naiwazia..asante mkuu
KwakweliLeo akiongeza 2 episodes itakua vizuri
Thanx dear
Mimi ni muoga sana ila wewe umezidi, hahahahahahaBig alikuwa anatutisha Hadi Kwa mbali.....Kuna siku nilihisi ananichungulia dirishani, nikaweka pazia vizuri
Shukrani sana baby zuu akee!! kitrambo sana hii ngoja niisome!
Bantu Lady Lovelovie Tayukwa leadermoe Unforgettable kitalembwa KatKit Mbobo Advicer mmash Lastmost mtzmweusi Restless Hustler mafian Carter mshaisoma hii episode???Sehemu ya Kumi na Tatu: (EXTENDED)
Nilikitumia chumba changu vema kumshawishi bwana Mgaya, kesho yake tu Zai akanambia atafika nyumbani kwaajili ya kuweka kambi hapo kwa muda kama tulivyokubaliana.
Siku hiyo ya Zai kuja ilikuchwa kama kawaida, kama zilivyo siku zingine, lakini baadae ndo' mambo yalikuja kubadilika kufanya siku hiyo kuwa tofauti na siku zinginewe.
Siku hiyo ilikuwa ni mwisho wa juma, kwahiyo mimi nalikuwapo nyumbani kwaajili ya mapumziko yangu ya kawaida, na kwasababu hiyo niliutumia muda wangu kufanya kazi zangu za hapa na pale mathalani kufua nguo, kuosha vyombo, kusafisha uwanja na kadhalika.
Nikiwa nafyagia uwanja, kama kazi yangu ya mwisho ilobakia kabla sijarejea zangu ndani, Amiri alikatiza akiwa amebebelea nyasi kuelekea kule bandani.
Nilipomwona kijana huyo, niliongea naye mambo machache, mambo na maagizo madogomadogo ya pale nyumbani, nilipomaliza hayo akaniuliza jambo; "kuna mtu anakuja nyumbani leo hii?"
Sikujua kwanini aliniuliza hivyo, nilimuuliza akaniambia ameona baadhi ya maandalizi humo ndani, basi nikamwambia ni kweli, Zai yu njiani anakuja. Akaniuliza yule rafiki yako wa siku zile? Nikamjibu, ndio, hakusema tena akaniaga na kwenda zake.
Baadae katika majira ya jioni hivi, Zai alikuja nyumbani akiwa amebebelaa begi lake moja la mgongoni.
Mwanamke huyo alionekana dhoofu, nilipomtia tu machoni, nilimfuata na kumkubatia kisha nikamsaidia begi lake, begi alilokuwa ameweka humo nguo kadhaa za kuvaa akiwa pale nyumbani, nikamkarimu na kumwongoza mpaka ndani, huko tukaongea mambo machache kabla hatujaongozana kwenye chumba kile nilichomwandalia.
Kabla hajutaingia humo ndani, Zai alisimama akautazama mlango wa chumba kile anacholala Amiri, aliutazama mlango huo kana kwamba anasoma karatasi za kitabu, nikamuuliza kunani na jambo hilo?
Akanitazama kwa macho yake dhaifu kisha akaniuliza, si ni mlango huu? Sikumwelewa anachomaanisha, mlango huu nini? Akauliza tena, si ni mlango huu ndo' niliukanda na mikono yangu siku zile?
Hapo nikakumbuka ya kile kisa chake cha kupandwa maruwani, nami sikutaka ajisikie vibaya nikamwambia aachane na mambo hayo, yashapita, na hata hivyo si muda mrefu tutapata suluhu lake.
Ya nini Zai kuhangaika na doa na dawa yake iko njiani?
Tuliingia ndani akaweka begi lake kitandani kisha akalifungua na kutoa mfuko mdogo humo, akiwa anaufungua mfuko huo alinambia wasaa huu amejipanga kwa kiasi chake mpaka hapo atakapopata suluhu lake la kudumu.
Katika mfuko ule alitoa vijiti kadhaa vya udi, hivyo nilivitambua, lakini pia akatoa dawa fulani ndani ya chupa ndogo ya plastiki, chupa mithili ya hizi tunazoziona kwenye maduka ya madawa, chupa hiyo ilikuwa imebandikwa 'stika' yenye maelezo maelezo mengi, ya kiswahili na kiarabu, Zai akanieleza dawa hiyo ya ni ya ki-sunna, alipewa na bwana mmoja akimweleza itamsaidia na tatizo lake.
Alinieleza matumizi ya dawa hizo, vema, hatua moja baada ya nyingine, akisema siku au muda ikitokea akabanwa na tatizo basi nisisite kumsaidia haraka niwezavyo, hana mkono mwingine wa msaada isipokuwa wangu.
Nami niseme nini tena? Niliyakubali yote alonambia nikaondoka hapo nikiyabeba kifuani mwangu maana sikuwa na budi, alimradi nilimshawishi mwenyewe aje kuweka makazi pale basi niliwajibika na maamuzi yangu hayo.
Nilienda chumbani mwangu nikafanya kushika simu yangu upesi na kunakili sauti yangu kwa rikaa ya 'recorder', nilifanya hivyo ili nisije kusahau aya alizonipa Zai, aya chache ambazo natakiwa kuzisema punde nikiwa nahangaika na maelezo ya dawa zile alizonionyesha, nilipofanya hivyo sasa nikatulia.
Niliona kila kitu kipo sawa.
Kwasababu hiyo, nilienda zangu kuoga ili basi nipumzike kidogo kabla ya kushika majukumu mengine ya mwisho.
Nililala kama lisaa na nusu hivi, nilipoamka, kabla sijashika kitu chochote, nikapata hisia kuna jambo halipo sawa.
Tangu naongea na Zai, nikalala na sasa nimeamka, sijapata kumwona mwanangu.
Hiyo haikuwa kawaida.
Nilichungulia dirishani kutazama huko nje, nikarusha macho yangu kote pale panapoonekana, sikumwona mtoto.
Nilienda sebuleni, napo mtoto hakuwapo wala kule jikoni vilevile.
Nikaita kama mara mbili, mtoto hakuitika. Nikatoka nje kutazama, sikumwona mtoto. Nilienda hadi kule kwenye mabanda ya mifugo, sikumwona mtoto kabisa, sasa nikaanza kupagawa.
Sasa nikaanza kujihisi mzembe kwelikweli. Kwanini sikumtafuta mtoto muda ule? Vipi kama kaenda mbali? Vipi kama kapotea?
Tumbo lilinivuruga.
Kidogo Zai aliufungua mlango nilotokea, akaniita Mage Mage, nilipoitika na kumjongea aliniuliza namtafuta mtoto? Nilipomjibu ndio akanambia yeye alimwona kwa mbali mtoto wangu kule nje akiwa anaongozana na Amiri.
Hivyo kama namtafuta basi nimtafute kijana huyo.
Kusikia hivyo angalau moyo wangu ukatuama, niliamini mwanangu yuko salama kwenye mikono ya Amiri, haina haja ya kupanda presha.
Nikangoja kidogo, kweli Amiri akajiri pale getini akiwa na mwanangu, wanatembea wakiwa wameshikana mikono.
Amiri alinisalimu kisha akanieleza walipotokea, mkononi mwa mwanangu alikuwa amebebelea pipi kubwa ya kijiti, mbali na pipi hiyo usoni mwake alikuwa amepachika tabasamu pana, bila shaka alikuwa amefurahia 'kampani' ile ya Amiri na mimi sikuwa na hiyana na hilo, nilifurahi kumwona mwanangu ana furaha.
Nilijaribu kumtwaa kutoka kwa Amiri ili niende naye ndani, ajabu mtoto akakataa.
Mwanzoni nilidhani masikhara, labda tamu za pipi tu zinamzuzua, lakini kadiri nilivyotia jitihada kumchukua ndo' nikazidi kufeli na kufeli, mtoto alinikataa kana kwamba mimi sio mama yake mzazi.
Alinikana kana kwamba tumbo nililombebea sio lile ninalotembea nalo, nami nilipoona nimeshindwa basi nikamwomba Amiri amshawishi mtoto akubali kwani yampasa sasa akapate chakula cha jioni.
Yaani fikiria unamwomba mtoto wako kama pesa? Tena toka kwenye mikono ya mtu mgeni, unajisikiaje?
Amiri aliongea na mtoto na kweli mtoto akaridhia kuja upande wangu, kabla sijaondoka kwenda ndani pamoja na mtoto, Amiri alinitaka tuzungumze jambo kidogo kama nina muda.
Nami sikuona ubaya, nikasonga kando tukazungumza.
Amiri alinieleza jambo fulani ambalo kwa kiasi chake lilinishtua.
Kama haitoshi alinisisitiza kile akisemacho ni kweli, kweli kabisa iliyo uchi na hivyo nisipuuzie nichukue hatua.
Baada ya hapo, akaenda zake akiniacha natafakari.
Natafakari kile alichonieleza.
Ni kweli ama ni hekaya?
Nilikuja kuubaini ukweli si muda mrefu, Amiri hakuwa ananiongopea hata kidogo.
Sikuchukua sekunde nyingi pale nje, nikaingia zangu ndani kisha nikafanya mpango wa chakula, tukala kwa pamoja isipokuwa Amiri, na baada ya kumaliza Zai akaniambia ana habari njema anataka kunieleza.
Habari hizo alizihifadhi kifuani mwake akiningojea niamke na tutulie ili tupate kuzungumza.
Basi nikamwazima sikio.
Kwa furaha, Zai alinieleza kesho ama keshokutwa ataondoka pale nyumbani, kuna kazi amepata pahali na kazi hiyo ni ya pesa nzuri sana, hawezi kuacha fursa hiyo iende kombo.
Alinambia: "Mage, shule ile ni ya wazungu, mshahara wao si haba, hata nikifanya kazi miezi mitatu tu naweza nikamiliki biashara ya maana."
Kitu ambacho Zai hakujua, mimi nilikuwa namsikiliza nikiwa naujua ukweli wote, ukweli ya kwamba ananiongopea, hata macho yake yalikuwa yanamsaliti.
Nilimsikiliza mpaka mwisho wake, nikampa kongole zake alafu nikampa na ushauri juu yake, baada ya hapo nikaenda zangu chumbani maana sikuwa nahitaji msongamano, nalihitaji muda wangu wa pekee kwaajili ya tafakari.
Nilipofika huko, nilijilaza kitandani nikawianisha yale alonambia Amiri na yale alonambia Zai, niliona bayana ukweli uko wapi, nilipoyamaliza mambo hayo nikaona ni stara kwenda kuonana na Amiri kuyakiri yale alotamka.
Nilitoka nikaenenda na njia mpaka nje, huko kutazama kushoto na kabla sijamaliza kulia nikamwona Amiri upande wa mabanda.
Nilimwita nikamweleza vema kuwa yale alonambia yamejiri kama alivyoyatamka.
Mwanamke yule, yaani Zai, ameniambia anataka kuondoka muda si mrefu, kesho ama keshokutwa, na basi anishauri cha kufanya maana nahisi nachanganyikiwa.
Amiri alitikisa kichwa chake akanambia: "najua hakuniona, na ndo' maana aliyaongea mambo yale kwenye simu. Yule mwanamke anajua kila kitu kuhusu wewe na ubaya hizo taarifa anazitumia kama silaha aidha kukuangamiza wewe ama kujikwamua yeye na hali yake. Mimi ninachokushauri ni uongeze umakini zaidi kwake, la sivyo siri zako zitakuwa barabarani kila mtu akizitazama kisha anageukia upande wa pili maana ni chukizo!"
Aliponieleza hayo, nilitafakari kwa ghadhabu nikijiuliza ni nini niliwahi kumkosea Zai mpaka akafikia hatua ile, hatua ya kuamua kutoa siri zangu za ndani kwa watu anaojua wanaweza kuniumiza?
Hapa nikaelewa vema yale ya Yuda kumsaliti Yesu, haikuwa sababu nyingine bali vipande kadhaa vya fedha, vipande hivyo ndo' hivi sasa vinavyomwehusha Zai mpaka anasahau ya urafiki wangu wa dhati?
Pamoja na kumsaidia yote yale?
Sasa anataka shikana na ndugu za Anwari kunitokomezea familia?
Amiri aliniuliza ni kwanini mwanamke yule yuko hapo nyumbani, amefuata nini hapo, mimi nikamweleza ni shida yake ya kupandwa maruwani ndo' imepelekea tabu yote hiyo, shida hiyo imechochea mpaka mwanamke huyo kuwa na tatizo la presha ya kupanda kiasi kwamba moyo wake ukatanuka.
Anwari akasema vema, basi nitilie maanani yale alonambia, baada ya hapo akaenda zake na mimi nikaenda zangu.
Kila mmoja na shughuli zake.
Baadae bwana Mgaya alirejea nyumbani kwenye majira ya saa tatu au nne usiku hivi, nikamkutanisha na Zai kama mgeni wetu wa pale nyumbani, Zai akasalimiana na bwana huyo na wakateta mambo kadhaa.
Zai alisema, "nashukuru sana, shemeji. Ni muda mrefu kweli tangu siku ile ya harusi, nafurahi leo tumeonana."
Zai akamwambia bwana Mgaya angependa kukaa hapo nyumbani kwa muda mrefu lakini kuna dharura imemtokea hivyo basi hatodumu hapo kwa zaidi ya siku mbili, itambidi aondoke.
Bwana Mgaya akawa hana la zaidi la kusema, yote kwake yalikuwa kheri, alimkaribisha Zai kwa mara nyingine pale nyumbani kisha akala chakula chake na kwenda zake kulala.
Ulipowadia usiku wa manane, usiku mzito wenye utulivu mkubwa, ndipo visa vikaanza rasmi chini ya paa lile.
Nikiwa sina hili wala lile, niko ndani ya ulevi wa usingizi, nikasikia sauti ya mtu akiita, akiita vitu nisivyovielewa.
Awali nilidhani sauti hiyo ni ndoto ama inatokea mbali huko mashambani lakini ilipoendelea kuita nikahisi tofauti, nikahisi sauti hiyo inatokea mule ndani na si kwingine.
Niliamka nikaketi kitako kitandani, nasikiliza kwa umakini kuhakikisha kile nisikiacho, nilipopata uhakika nikafanya jitihada za kumwasha bwana Mgaya, kumwamsha asikie na tusaidizane.
Mgaya ... Mgaya ... Amka! .. we Mgaya!
Nikamwita nikimtikisa lakini hakuamka, aliendelea kukoroma kana kwamba hamna kinahojiri.
Sikukata tamaa, nikaita tena na tena, tena na tena, huko nje ya chumba sauti inazidi kumea na sasa si kuita tena, sauti ile inanguruma kana kwamba simba ama tuseme mbwa anayemtishia mvamizi, lakini bado Mgaya hakuamka.
Ni kama vile hakuwa katika usingizi huu wa kawaida tunaoujua, kwa mtu aliyekuwepo usingizini asingeweza kumudu pale kitandani pasipo kuamka kwa namna ile nilivyokuwa namwamsha.
Nilimsukumia huku na kule kazi yake ikawa kubadili tu mikao, lakini kuamka 'nehi nehi'. Alilala usingizi mkubwa ambao hata samaki pono haufahamu abadan!
Nilikuwa napoteza muda na nguvu yangu bure kuhangaika naye, na nilipobaini hilo niliachana naye nikanyaka simu yangu kisha nikaelekea mlangoni.
Sasa sauti inazidi kunifikia masikioni, tena vema sana, sauti ya mtu akinguruma kama mnyama, na mtu akipiga mayowe kama mfiwa.
Nilifungua mlango nikashika sakafu baridi ya korido, kitu cha kwanza kufanya, nikaelekea kwenye mlango wa Amiri nikabisha hodi kwa lengo aje kunisaidia na janga lile.
Nilibisha hodi nikiita Amiri Amiri, Amiri amka njoo upesi, Amiri njoo unisaidie, kweli kitambo kidogo mlango wa Amiri ukafunguliwa akatoka kijana huyo akiwa amevalia bukta tu, uso wake umejifinyanga na mang'amung'amu ya usingizi, macho yake yamefunikwa na ndita za sin'tofahamu.
Akaniuliza, kuna nini? Mbona majra haya mlangoni kugonga?
Nikastaajabu, ina maana mambo yale yananibughudhi peke yangu ama? Hawa wengine wanalalaje na songombingo zile? Ngurumo na mayowe?
Nilimweleza kuna tatizo, akaniambia anasikia, nikamwomba afuatane na mimi kwenda kumkabili mwanamke yule chumbani mwake, mimi najua kila kitu, 'ei to zedi' ya namna ya kuenenda naye maana alishanielekeza.
Amiri hakukataa, akiwa vilevile asichukue kitu wala kufanya jambo jingine, aliongozana na mimi moja kwa moja mpaka ndani ya chumba alichokuwemo Zai.
Humo tukamkuta mwanamke huyo, akiwa amevalia nguo ya ndani pekee, anahaha na kurandaranda huku na kule akijitutumua kama mpambanaji, tena mpambanaji mwenye nguvu kama Awafu, macho ameyatoa kama mtu aliyenigwa na tonge kubwa kooni.
Alivyotuona, alisimama akituangazia, kweli sijawahi kuona mapepo sijui maruwani kama yale, nalikuwa nashuhudia kwenye runinga vipindi mbalimbali vya maombi lakini sijawahi kutana na kitu halisi kama kile, kitu cha kutisha kweli, yani kama una roho ndogo huwezi kuhimili, aidha uzirai ama ukimbie.
Kufumba na kufumbua Zai alimkimbilia Amiri akipiga kelele, akamvaa wakapelekana mpaka chini, sasa ikawa mielekea aidha yeye ama Amiri, Amiri ama yeye.
Waligaragazana huku na kule kupishana nguvu, Zai anahangaika kumjeruhi Amiri na Amiri anahangaika kujizuia, yani ni kelele, ngurumo na miguno ya maumivu na jitihada za kujikwamua kutoka kwa mwingine.
Nilijaribu kumshika Zai lakini kamwe sikufanikiwa, mikono yangu ilikuwa kama ubua vile kwenye mwili wake, sikuweza hata kumsogeza msuli.
Amiri akaniambia, tena akipiga kelele ya mamlaka, fanya ile dawa!...fanya ile dawa! Mama, fanya ile dawa, fanya haraka!
Hapo ndo' nikakumbuka kumbe kuna jambo natakiwa kulifanya, tena jambo hilo ndo' limelileta humo ndani, basi upesi nikaangaza hapa na pale, kwenye kona ya chumba kile nikaona begi la Zai, upesi nikaliendea na kulifungua kutoa ile chupa ya dawa na vijiti vya ubani.
Nikakimbilia jikoni kuwasha ubani ule na pia kubeba kisosi kwaajili ya dawa, nilipofika chumbani nikafanya yale ambayo Zai alinielekeza pale awali, hatua kwa hatua, lakini nilipofika kwenye kunuwia yale maneno ya lugha nyingine, maneno ambayo niliyarekodi kwenye simu yangu, sikuweza kabisa!
Kila nilipojaribu nilikwama, ulimi mzito, ulimi una ukakasi, maneno hayatamkiki kabisa, wakati huo bado pambano la Amiri na Zai linapamba moto, hakuna anayekubali kuzidiwa na mwenziwe.
Nikiwa nahangaikahangaika, bado sijajimudu na maneno lakini mazingira nimeyaweka sawa, Amiri akaanza kutamka maneno ambayo binafsi sikuyaelewa, maneno hayo yalikuwa machache tu lakini aliyatamka kwa marejeleo, marejeleo ambayo yalinifanya nikayashika maneno hayo kwa upesi sana.
Kidogo akanambia, kwa sauti ileile ya mamlaka huku aking'ang'ana na Zai, tamka hayo maneno, Mama, tamka hayo maneno kama mimi! Fanya upesi!
Nikafanya hivyo, sikuwa na budi, nilifanya nikiwa nauzungusha ule udi kwenye kichwa cha Zai mara tatu kwenda, mara tatu kurudi, mara tatu kwenda na tena tatu kurudi.
Ajabu, Zai akanitazama kwa macho makali, kabla sijafanya kitu, akamwachia Amiri kisha akanirukia mithili ya paka, sikuweza kumhimili tukaenda wote mpaka chini, nilifikia mikono nikajiumiza sana.
Zai alinikaba kwanguvu mno nikawa natapatapa kujikwamua lakini kila nilivyojifaragua sikuweza kumshinda, alikuwa na nguvu mno mno, nilitumia mikono na miguu yangu kujiokoa lakini sikuweza kabisa.
Amiri alikuja kunisaidia kwa kumvuta mwanamke huyo kwanguvu, nami nikamsaidia kwa kutumia miguu yangu kumsukumia Zai mbali na mimi.
Nilitumia nguvu kubwa kiasi nikamtupa Zai kwenye kingo ya kitanda.
Aliruka akakita hapo kwanguvu akitoa kishindo kikubwa - KIH! kisha akatulia tuli, tuli sana.
Amiri alimsogelea kwa karibu akamtazama kwa umakini, alimshika nyuma ya kisogo akaona damu vidoleni mwake, akanitazama na kunambia, amekufa.
Hapo moyo wangu ukararuka, nikauliza unasemaje, Amiri? Amiri akarudia tena, Zai amekufa.
Jasho likaongezeka kunitiririka, nikanyanyuka upesi kwenda kumtazama Zai, nikamwita mara tatu nikimpigapiga makofi, hakuamka wala hakuitika hata kwa kuguna, nikaamini kweli mwanamke yule amekufa.
Sasa inakuaje? Nikajiuliza mimi mwenyewe, sasa inakuaje, nikamuuliza Amiri.
Nilihisi akili imeniruka kwakweli, kwa muda kidogo nikawa kama mtu alochanganyikiwa, Amiri alijaribu kunituliza akinambia sasa yatupasa kufikiri na sio kuwehuka, ikanichukua muda kidogo kurejea katika fahamu zangu za kawaida.
Amiri alinambia: "sasa tuubebe huu mwili tukaufukie mashambani, hamna atakayejua!"
Nikamuuliza ana uhakika, akasema ndio, ninyanyuke tufanye hilo zoezi upesi.
Basi kwa kusaidiana, tukaubeba mwili wa Zai mpaka jikoni, tukafungua mlango kisha tukaongozana mpaka nje ya uzio, huko tukaulaza mwili wa Zai chini kisha Amiri akaendea chepe ndani kwaajili ya kuja kuchimba ardhi tumfukie Zai.
Nilisimama hapo shambani nikiwa naogopa sana, kweli tuko wenyewe? Hamna mtu anayetuona? Nilitazama huku na kule kila saa, mwili unatetemeka, si kwa baridi bali kwa hofu.
Kidogo Amiri alifika akiwa amebebelea chepe mkononi, jasho lamtiririka kwenye paji lake la uso, akanambia, "sikia, wewe kazi yako imekwisha. Huku niachie mimi. Nenda ndani kahakikishe mazingira yanakuwa sawa."
Nikaenda ndani upesi, kuanzia pale mlango wa jikoni mpaka ndani chumbani alimokuwamo Zai kulikuwa na matone na michirizi mingi ya damu.
Nikaanza kufuta damu hizo upesi kwa kutumia tambara na ndoo ndogo, nilipomaliza jikoni nilishika korido ya kuelekea chumbani, kabla sijamaliza korido hiyo, nikasikia mlango unafunguliwa.
Upesi nikarusha macho mwisho wa korido, hapo moyo unalipuka vipande vipande, ni nani huyo?
Sauti ikaita, mama! ... Kumbe alikuwa mtoto, upesi nikamkimbilia na kuingia naye chumbani nikimuuliza mbona hajalala? Anafanya nini macho muda huo? Nilimuuliza nikihofia kama atakuwa ameona chochote.
Lakini kumbe yeye hakuwa shida pale, shida ilikuja pale nilipoingia naye ndani nikamkuta bwana Mgaya akiwa amesimama anatazama nje ya dirisha, nikahisi haja zote kwa pamoja! Sikujua nianze na ipi nifuatie na ipi.
Nilijikuta nasema mwenyewe kama mwehu, "Mgaya, ngoja nitakueleza, tafadhali nisikilize."
Mgaya hakusumbuka na mimi, aliendelea kusimama pale dirishani, alisimama kama mwanasesere, hajigusi wala hasogei, nikamsogelea nikimuita, bado kimya, sijui alikua anawaza nini, sijui alikuwa amepanga nini.
Nilipomkaribia kabisa nilisimama nyuma yake, kidogo nikahisi kishindo cha miguu, kutazama kule mlangoni nikamwona Amiri amesimama, chepe lake mkononi.
Akanambia, "tayari nimeshamaliza."
Kurudisha uso kwa Mgaya nikamkuta mwanaume huyo ananitazama kwa macho ya woga, mdomo wake unatetemeka.
Amiri akasema, "na huyo ndo' afuataye."
Mimi nikadakia, "hapana, hapana! Sio hivyo, Mgaya. Mgaya, ngoja nikueleze."
"UNIELEZE NINI?"
Nikakurupuka kitandani kama mwivi, macho yamenitoka, kutazama pembeni yangu namwona Mgaya akiwa amejilaza, nusu ya mwili wake umemezwa na shuka, ananiangalia kwa macho ya wasiwasi na kuchanganyikiwa.
Kutazama dirishani bado giza, nikamuuliza bwana Mgaya saa hii ni saa ngapi? Akaniambia saa kumi na moja sasa.
Haraka nikakurupuka kitandani, nikakimbilia chumba cha Zai.
Sikuamini ile ilikuwa ni ndoto, nilijikuta nakumbuka yale ya mama mkwe na yale yalotokea baada ya ndoto ile.
Nilipofika huko wala sikubisha hodi nikazama moja kwa moja, kutazama kitandani sioni mtu. Zai hakuwapo.
Ndani humo kunanukia ubani si utani.
Nilitazama kwenye kingo za dirisha nikaona vijiti vya ubani vikiishilia, na pale juu ya meza ya chumba hicho kuna kisosi chenye dawa, kisosi kilekile nilichokiona katika ndoto yangu.
Basi upesi nikatoka humo nikimbilie nje, bwana Mgaya ananifuata akinistaajabu nimepatwa na nini, nilipofika jikoni, hamaki, nikamkuta Zai akiwa anakunywa maji.
Mwanamke huyo alinitazama akaniuliza, "vipi, Mage? Kuna shida?"
Sikuelewa kitu.
Nilimsogelea nikamkagua mwili wake mzima kwa macho na vidol vyangu, alikuwa yu mzima mtupu, hana hata mchubuko, nikarudi koridoni upesi kwenda kwenye chumba cha Amiri.
Hapo nikagonga mara tatu na kuita, Amiri, Amiri!
Kimya.
Niliendelea kuita lakini Amiri hakuitika wala hakutoka ndani.
Bwana Mgaya akanisogelea na kunambia, Amiri yuko nje kitambo, ameshadamka kukamua maziwa.
Nikasema mwenyewe hapana, hapana, haiwezekani.
Akili yangu ikanambia sasa nielekee kule shambani tulipoupeleka mwili wa Zai kuufukia.
Niende huko nikatazame.
***
Asante sana ccyBantu Lady Lovelovie Tayukwa leadermoe Unforgettable kitalembwa KatKit Mbobo Advicer mmash Lastmost mtzmweusi Restless Hustler mafian Carter mshaisoma hii episode???
Mambo ni motroo
Asante cousin. [emoji120]Bantu Lady Lovelovie Tayukwa leadermoe Unforgettable kitalembwa KatKit Mbobo Advicer mmash Lastmost mtzmweusi Restless Hustler mafian Carter mshaisoma hii episode???
Mambo ni motroo
Enjoy the story cousin !Asante cousin. [emoji120]
Ya leo ndefu, uliweza kusoma?Enjoy the story cousin !
Bado ndio nataka kuianza hapa jamani hapo umetuma ndefuu kuja kutupia tena mpaka tusahau usifanye Hivo mkuu!!Ya leo ndefu, uliweza kusoma?
KeyaaYa leo ndefu, uliweza kusoma?
Asante dear Antonnia Mambo yanazidi kuwa 🔥🔥🔥🔥Bantu Lady Lovelovie Tayukwa leadermoe Unforgettable kitalembwa KatKit Mbobo Advicer mmash Lastmost mtzmweusi Restless Hustler mafian Carter mshaisoma hii episode???
Mambo ni motroo
Big ndio nani tena kitkat? [emoji1787]Hivi kati ya Amiri na Big nani mnoma?, binafsi Big alikua anafanya naogopa kusoma story nikiwa pekeangu room hasa nyakati za usiku
Big alikuw chenga sana bora amiri [emoji28][emoji28]Hivi kati ya Amiri na Big nani mnoma?, binafsi Big alikua anafanya naogopa kusoma story nikiwa pekeangu room hasa nyakati za usiku