Niliyoshuhudia Kariakoo

Niliyoshuhudia Kariakoo

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2022
Posts
9,576
Reaction score
13,545
Ilikua siku ya kawaida kama siku nyingine kwa wafanyabiashara.

Baada ya kushinda mpaka saa saba usiku napokea mzigo na kupanga mipango kazi ya wiki nzima...niliondoka kariakoo mtaa wa Narungombe nikapita mtaa wa mchikichini nitokee barabarani MSIMBAZI road.

Lakini wakati nipo mtaa wa mchikichini mkabala na mtaa wa Kongo nikapokea simu hivyo ikanibidi nisimame pembeni mwa jengo ambalo masaa machache mbele lingeua watu kwa ajali ya kuanguka.

Nikapokea simu ya mdau nikaongea kama dakika 30 nzima.

Laiti ningekua najua kama hili ghorofa nililosimama mbele yake kesho linaanguka....ningewapigia kelele wale walinzi kua kesho wasiruhusu mtu yoyote kuingia ndani itakapofika asubuhi.

Usiku kwa kawaida mitaa yote ya kariakoo inakua imetulia na watu wanakua sio wengi kama mchana... zaidi ya wafanyabiashara wa chakula na wakazi wa mule mule kariakoo na walinzi shirikishi na walinzi wa makampuni binafsi......na vijana wanaopiga deiwaka za ufundi au kubeba mzigo.

Nilipita katika jengo lile Wala sikuwaza kama kesho litaanguka na kuua watu.

SIRI YA UHAI ANAYO MUNGU.
ASUBUHI SIKU YA TUKIO****
Sikumbuki ni mda Gani, lakini nachokumbuka nilipokea simu asubuhi kutoka kwa mmoja wa matajiri wa kariakoo....i mean mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa pale kariakoo...na mazungumzo yetu yalikua katika namna hii.
BOSI : Dogo upo wapi???
MIMI : Nipo mitaa ya agha khan hospital.
BOSI : Umesikia kilichotokea.
MIMI : Wapi bosi????
BOSI : Sina mda wa kukuelezea:
BOSI : Chukua pesa peleka vifaa vya uokozi
BOSI : Kariakoo ghorofa imeanguka
BOSI : Tuwasaidie ndugu zetu hali ni tete.
BOSI : Mpigie..*****atakupa taarifa kamili
BOSI : Kuhusu pesa usijali..uhai ni muhimu.
BOSI : Wahi dogo kasaidie ndio ubinadamu

**********************************

Baada ya mazungumzo yangu na tajiri ndipo nilipoacha kila kitu na kukimbilia eneo la tukio kuangalia ni nini naweza kusaidia pale mwanzoni.

Nilipofikia tu nikagundua hakuna vifaa vya uokozi vya kutosha ..na maji na chakula......na tukahakikisha vikosi kazi vyote havikosi vifaa vya uokozi,maji na chakula.

Nikakuta pia wadau wengine kutoka sekta binafsi na serikali wameshafika....tukasaidiana na tulipambana mno usiku na mchana!

KIUKWELI.
Jeshi la polisi...walitupa ushirikiano
Jeshi la magereza walitupa ushirikiano
Jeshi la zimamoto walitupa ushirikiano
Jeshi la uhamiaji walitupa ushirikiano
Jeshi la JWTZ walitupa ushirikiano
Wadau wa red cross na red crescent
Wadau wa jumuiya za wahindi.
Wadau wa BAKWATA.
Wadau wa KKKT.
Mkuu wa mkoa brother Chalamila
Wadau wa ROMAN CATHOLIC.
Na wafanyabiashara wenzetu waliotuzunguka hapa kariakoo mchango wao ni mkubwa mno..!!
KINACHOUMIZA NI KWAMBA WALIOFARIKI NI VIJANA WENZETU TUNAOPAMBANA NAO KILA SIKU ILI MKONO UENDE KINYWANI.

WATU TUNAOWAFAHAMU.
VIJANA WALIOJIAJIRI.
WALIKUA NA FAMILIA
WALIKUA NA WAZAZI.
WALIKUA WANATEGEMEWA.
NA WALIKUA WASHIRIKA WETU KIBIASHARA.
MAISHA HAYAPO FAIR.
UKIONA UPO HAI MSHUKURU MUNGU.
UHAI HAUNA MWENYEWE.

Screenshot_20241118-035934.png
Screenshot_20241118-035852.png
Screenshot_20241117-124220.png
Screenshot_20241117-124147.png
Screenshot_20241117-111727.png
 
Karikakoo inahitaji kuchunguzwa yale majengo yote.
Tujifunze kupitia ajali hii tusije tukajisahau mbeleni
Sio kwa Serikali hii, tumeweka SIASA kwenye kila kitu. Utaambiwa usiwaguse ni msimu WA Uchaguzi tutakosa Kura. Nchi ya ajabu Sana sana, kuna siku Yale majengo ya Wizara pale Dodoma yataanguka, msisahau KUHUSU Hall Five UDSM na Ile Magufuli Hostel. Nakumbusha Tu kwa wema
 
Sio kwa Serikali hii, tumeweka SIASA kwenye kila kitu. Utaambiwa usiwaguse ni msimu WA Uchaguzi tutakosa Kura. Nchi ya ajabu Sana sana, kuna siku Yale majengo ya Wizara pale Dodoma yataanguka, msisahau KUHUSU Hall Five UDSM na Ile Magufuli Hostel. Nakumbusha Tu kwa wema
Mkiambiwa muipige chini CCM mnajikwepesha

Ngoja tuendelee kufa hadi tuzinduke usingizini
 
Back
Top Bottom