Yale ya wizara nayo yana shida mkuu..?Sio kwa Serikali hii, tumeweka SIASA kwenye kila kitu. Utaambiwa usiwaguse ni msimu WA Uchaguzi tutakosa Kura. Nchi ya ajabu Sana sana, kuna siku Yale majengo ya Wizara pale Dodoma yataanguka, msisahau KUHUSU Hall Five UDSM na Ile Magufuli Hostel. Nakumbusha Tu kwa wema
Vibaka wengi sana huko lazima watandeJW wametanda sana Kkoo hata pa kupita hamna
Serious??Mpaka mda huu naondoka....nilichoshuhudia ni harufu Kali ya maiti
Kupata mtu akiwa hai...ni MUNGU AAMUE
Serikali inayoweka chama mbele unadhani hayata jirudia haya. ..? Uokoaji wenyewe eti mawaziri wapo wamekunja nne tu pale. V8 kibao ila wagonjwa wana bebwa na kirikuuIlikua siku ya kawaida kama siku nyingine kwa wafanyabiashara.
Baada ya kushinda mpaka saa saba usiku napokea mzigo na kupanga mipango kazi ya wiki nzima...niliondoka kariakoo mtaa wa Narungombe nikapita mtaa wa mchikichini nitokee barabarani MSIMBAZI road.
Lakini wakati nipo mtaa wa mchikichini mkabala na mtaa wa Kongo nikapokea simu hivyo ikanibidi nisimame pembeni mwa jengo ambalo masaa machache mbele lingeua watu kwa ajali ya kuanguka.
Nikapokea simu ya mdau nikaongea kama dakika 30 nzima.
Laiti ningekua najua kama hili ghorofa nililosimama mbele yake kesho linaanguka....ningewapigia kelele wale walinzi kua kesho wasiruhusu mtu yoyote kuingia ndani itakapofika asubuhi.
Usiku kwa kawaida mitaa yote ya kariakoo inakua imetulia na watu wanakua sio wengi kama mchana... zaidi ya wafanyabiashara wa chakula na wakazi wa mule mule kariakoo na walinzi shirikishi na walinzi wa makampuni binafsi......na vijana wanaopiga deiwaka za ufundi au kubeba mzigo.
Nilipita katika jengo lile Wala sikuwaza kama kesho litaanguka na kuua watu.
SIRI YA UHAI ANAYO MUNGU.
ASUBUHI SIKU YA TUKIO****
Sikumbuki ni mda Gani, lakini nachokumbuka nilipokea simu asubuhi kutoka kwa mmoja wa matajiri wa kariakoo....i mean mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa pale kariakoo...na mazungumzo yetu yalikua katika namna hii.
BOSI : Dogo upo wapi???
MIMI : Nipo mitaa ya agha khan hospital.
BOSI : Umesikia kilichotokea.
MIMI : Wapi bosi????
BOSI : Sina mda wa kukuelezea:
BOSI : Chukua pesa peleka vifaa vya uokozi
BOSI : Kariakoo ghorofa imeanguka
BOSI : Tuwasaidie ndugu zetu hali ni tete.
BOSI : Mpigie..*****atakupa taarifa kamili
BOSI : Kuhusu pesa usijali..uhai ni muhimu.
BOSI : Wahi dogo kasaidie ndio ubinadamu
**********************************
Baada ya mazungumzo yangu na tajiri ndipo nilipoacha kila kitu na kukimbilia eneo la tukio kuangalia ni nini naweza kusaidia pale mwanzoni.
Nilipofikia tu nikagundua hakuna vifaa vya uokozi vya kutosha ..na maji na chakula......na tukahakikisha vikosi kazi vyote havikosi vifaa vya uokozi,maji na chakula.
Nikakuta pia wadau wengine kutoka sekta binafsi na serikali wameshafika....tukasaidiana na tulipambana mno usiku na mchana!
KIUKWELI.
Jeshi la polisi...walitupa ushirikiano
Jeshi la magereza walitupa ushirikiano
Jeshi la zimamoto walitupa ushirikiano
Jeshi la uhamiaji walitupa ushirikiano
Jeshi la JWTZ walitupa ushirikiano
Wadau wa red cross na red crescent
Wadau wa jumuiya za wahindi.
Wadau wa BAKWATA.
Wadau wa KKKT.
Mkuu wa mkoa brother Chalamila
Wadau wa ROMAN CATHOLIC.
Na wafanyabiashara wenzetu waliotuzunguka hapa kariakoo mchango wao ni mkubwa mno..!!
KINACHOUMIZA NI KWAMBA WALIOFARIKI NI VIJANA WENZETU TUNAOPAMBANA NAO KILA SIKU ILI MKONO UENDE KINYWANI.
WATU TUNAOWAFAHAMU.
VIJANA WALIOJIAJIRI.
WALIKUA NA FAMILIA
WALIKUA NA WAZAZI.
WALIKUA WANATEGEMEWA.
NA WALIKUA WASHIRIKA WETU KIBIASHARA.
MAISHA HAYAPO FAIR.
UKIONA UPO HAI MSHUKURU MUNGU.
UHAI HAUNA MWENYEWE.
View attachment 3156686View attachment 3156687View attachment 3156693View attachment 3156694View attachment 3156696
Vibaka wanaitumia fursa vzr yaaniVibaka wengi sana huko lazima watande
Ova
ULinzi uimarishwe kwa sanaVibaka ndiyo wamehamia huko
Ova
Tapeli apewe maua tena!?Mpeni Nifa maua yake.
Hata kwa akili zake aliwaza sana.
kinachotia matumaini wamefanikiwa kushushiwa maji,glucose na oxygen walau kama kutakuwa kuna ambao bado wapo wataendelea kusurvive...Mungu awape wepesi na kuendelea kuwapa nguvu wahanga na waokoajiJanga la K/Koo linaumiza sana, bado najiuliza walio chini ya kifusi bado wako hai?
Ninaendelea kumfanyia research, karibia napata conclusion.Tapeli apewe maua tena!?
Siyo nchi hii,kwa anayekumbuka mwaka 2012 hapa Kariakoo kati ya mtaa wa Mafia na Swahili kuna jengo la floor 8 lipo kulia kama unaingia sokoni Kariakoo wakati likiwa ktk hatua za mwisho za ujenzi lilipata crack likiwa limesimama lenyewe ilikuwa siku ya jumapili wala hakukuwa na mafundi.Karikakoo inahitaji kuchunguzwa yale majengo yote.
Tujifunze kupitia ajali hii tusije tukajisahau mbeleni
Upo sahiiSiyo nchi hii,kwa anayekumbuka mwaka 2012 hapa Kariakoo kati ya mtaa wa Mafia na Swahili kuna jengo la floor 8 lipo kulia kama unaingia sokoni Kariakoo wakati likiwa ktk hatua za mwisho za ujenzi lilipata crack likiwa limesimama lenyewe ilikuwa siku ya jumapili wala hakukuwa na mafundi.
Nakumbuka alikuja mkuu wa mkoa kipindi hicho akaamuru libomolewe ila kilichofanyika ujenzi ulisimama baada ya miaka miwili ukaendelea napoandika hapa limeshajaa frame zote mpaka za 2nd floor zimejaa nadhani kinachosaidia juu hakuna wapangaji,Waafrika sisi kinatulinda Mungu na mizimu tu huko serikalini hamna kitu.
DuuhNilisha sema hapa na nitazidi Kusema.
Waafrika wengi wanakufa kutokana na ujinga, uzembe, rushwa, kuishi kwa mazoea, siasa, tamaa na njaa.
Wala hakuna Mungu anayepanga kifo au uhai wa watu.
Nahisi hivyo... au alikua muokoajiNaomba kuuliza yule kijana aliyepost video anatoka jasho na hajaongea lolote kuna mwenzie jirani akawa anaongea alitoka?
Ulinzi upoULinzi uimarishwe kwa sana
YeahSerious??
Nilikua nagawa vifaa vya uokozi na chakula.....sikua kwenye vikosi kazi vya uokozi.Mleta uzi bw. Nelson Kagame mbona reflector yako, jeans ulovaa na viatu havionyeshi hata chembe ya vumbi ????
Kwa hiyo badala ya kusaidia uemeenda kibishooo uwachora wahanga ???? Acha hizo
Uokozi unaendeleaPoleni sana, kwa ninyi mliokuwepo eneo la tukio.
Ni kitu gani hasa kinakwamisha uokozi??