Niliyoshuhudia; Safari Yangu Kuokoa Wahanga Kariakoo

Niliyoshuhudia; Safari Yangu Kuokoa Wahanga Kariakoo

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Mosi; kabisa nasikitika kushindwa kugika eneo la tukio sababu sihusiki na sina kibali cha kuniruhusu kufika eneo la tukio.

20241118_162403.jpg

Pili; nimeshindwa kupiga picha yoyote maana nilifukuzwa kama haramia.

Tatu; nimeshindwa kuelewa huu ulinzi wa leo kwa nini leo na siyo jana na juzi wakati tukio bado la moto na wengi waliopo chini wakiwa na nguvu za kuimiri ku-survive?

Hakika afrika bado na tuna safari ndefu mno yaani. Naanza na safari kutoka Mbezi mwisho pale, baada ya kukata tiketi ya mwendokasi nimekaa masaa 2+ ndipo basi likaja na tulijazana mithili ya nyuki wanamuua mvamizi kwenye mzimga wao.

Njiani mwendokasi haikupita kwenye barabara yake bali ilitumia njia ya magari ya kawaida, kisa na mkasa kwamba kuna basi mwendokasi lililoharibika njiani, kero hiyo.

Hiyo sijui kampuni ya mabasi ya DART ni mbaya sana, hawana utaratibu mzuri, hawatoi taarifa zozote kwamba mabasi yao yanaishia njiani ili abilia wapande wakijua alternative nyingine baada ya kushuka, bladfkn.

Sijui ndiyo mnaitwa express!, maana haikusimama kituo chochote hadi pale kituo mnaita fire (zimamoto) gafla naulizwa wewe hushuki? Nikajibu ndiyo, nashuka mwisho gerezani, nikaambiwa kule haiendi kuna uokoaji wa maporomoko.

Sikujua kwa nini pale ila nilishuka nikaanza kutembea kwa kuuliza kuelekea kuokoa ndg zetu bana, sijafika hata mita 100 nazuia tena na mgambo "weweeee usipiiiteee hapooooo!!"

Nilimwambia naenda kwenye jengo kusaidia kukokoa akaniambia huruhusiwi na marufuku, nikasikia askali anamuuliza mgambo "anatakaaa niniiiii huyooooo!"

Kutokea hapo ndg yangu msomaji, nikarudi nyuma kuuliza mwananchi mmoja mmoja jinsi ya kufika eneo husika na sikufanikiwa kufika, kisa ulinzi.

Makosa makubwa ya kiusalama; kufunga barabara kuu inayotumika katika uzalishaji na usafirishaji katikati ya jiji, mtu anatoka kwa miguu fire hadi gerezani.

Hapo nimewashangaa viongozi wote hadi jeshi la polisi, kushindwa kusimamia matumizi ya upande mmoja kwa mbasi ya mwendokasi yapite na upande wa pili ukabaki kwa wao waokoaji.

Kuweka ulinzi wa hali ya juu utadhani kuna uvamizi wa hali ya juu (high level crime robbery) tena baada ya siku mbili kupita, kichekesho hiki ndg.

Mwisho lakini sinkwa umuhimu; Afrika bado tunatakiwa kutawaliwa (colonize)
 
Na usisahau kuchangia maafa ndugu yangu msomaji.
View attachment 3155422
Kwa hili sikubaliani nawe. Tulishachangia pesa zikaenda ndiko siko. Pia hiyo ofisi ya maafa inapaswa kuwa na fedha ya tahadhari kwa mambo kama haya. Hili la kusubiri michango ya watu linachelewesha kutoa misaada haraka kwa wahanga. Mipango yetu haipo sawa. Tuna pesa nyingi kwa mambo ya anasa. Linapokuja suala la kuokoa watu waliopo hatarini kupoteza maisha, pesa inakuwa haipo kabisa hadi tuchangishane.
 
Asante sana mkuu!.
Mkuu sikujui haunijui ila kama kweli ulikuwapo kama mmoja ya waokozi basi Mungu huyu anaenibariki akubariki mara 1000000000000000000000 na zaidi
Kama umesoma story yote nimeandika ila kwa bahati mbaya ni kwamba sikufanikiwa kufika eneo la tukio!.
 
Mnaenda kujazana tu hapo hilo ghorofa linaweza kuwaangukia muongeze vifo.
UPDATE; Inakuhusu hii.
IMG_20241119_094751.jpg

Hawa wajomba zako walikuwepo, nao waliongeza uzito?.
IMG_20241119_094824.jpg

Pengine unataka kusema hawa ni special, sawa je, wakifika sehemu jengo linataka kuanguka kwa sababu they're so special jengo linatulia kwanza eeh?.
 
Back
Top Bottom