Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Niliyoyabaini katika Operesheni ya Polisi dhidi ya watuhumiwa wa Panya Road - Dar es salaam

Jeshi la wananchi wanafundishwa kulenga kichwani tu ndio, lakini polisi wanafundishwa kulenga miguuni ili wamkamate mtuhumiwa na kumpeleka kwenye chombo cha kutoa haki sio kuua.

Tambua Jeshi la wananchi na Polisi ni vitu viwili tofauti. Kama kuna tatizo Jeshi la wananchi hawana majadiliano lakini wana nafasi hiyo kufanikisha upatikanaji wa kiini cha tatizo baada ya kupeleleza.

Polisi walioua, aliyewatuma na kuagiza operesheni hiyo atashitakiwa tu, Kesi rejea ni Lengao Ole Sabaya hii itakuja kuwasumbua sana mpaka kuna baadhi watakimbia nchi
Tatizo Vijana Wa Siku hizi hamfanyi utafiti.
Tanzania Ina Majeshi Matatu.
Jeshi la Wananchi
Jeshi la Polisi na
Jeshi la magereza

Na Majeshi Yote hayo Yana Vikosi maalumu waliofumzwa matunzo maalumu Ndani na nje ya Nchi Kwa gharama Kubwa ya Kodi zetu.

Ukizingua kwenye haya Majeshi unazinguliwa.

Magaidi wanataka kurudi kama Kibiti na wanawatumia wanasiasa mana pesa zinazofadhili ugaidi ni nyingi sana. Zinatoka Mashariki na magharibi Kwa manufaa ya Nchi hizo HUKO nje .

Polisi wakibweteka na kumsikiliza Abdul Nondo wajue wamekwisha mana huyo ni mshika Kibiti Wa Vikundi vya kihalifu vinavyojifungamanisha na Siasa.
 
Duuu, mkuu Kwahiyo vita ya Burundi ilisababishwa na panya road wa huko? Mkuu hao watu wanaobaka, kuvuta bangi nk ni wa taasisi gani ya kimamlaka ili tuseme hawafanyi sawa?
Mbeberu hawapendi kuona amani kwenye Nchi yenye Rasilimali nyingi kama Tanzania .
Tafakari!!!

Kumbuka na Rais Wa Zanzibar ametangaza KUFANYA mchakato Wa kuchimba mafuta .

Mafuta yakichimbwa Zanzibar ni pigo Kubwa sana Kwa Nchi zile na mabeberu walioweka visima vyao Kule.

Wanaotumiwa kule Zanzibar Kwa sasa ni ACT ya Nondo.
 
Panyaroad na Watoto wa mitaani ni kufeli kwa sera mbovu tulizonazo KUHUSU ajira na uwajibikaji!!

Ungetuambia nyie ACT sera Zenu ni zipi za kutatua janga hili!!

Polisi ni watumishi wanaotekeleza sera mnazotunga nyie wanasiasa!!!ziwe sera NZURI au MBAYA!!
 
Watanzania wengi siyo watu wakutafakari. Na inaonyesha wewe ni mmoja wao. Ni hivi: hakuna mtu anayekataa kuwa panya road ni tatizo kubwa na ni hatari sana. Kuna wengi tumeshaathirika na hawa vibaka. Tunataka sana hatua zichukuliwe na watokomezwe wote. Tunachokataa ni hili jambo la polisi kuua baada ya kuwakamata. Historia dunia kote inaonyesha kuhukumu wahalifu namna hii i.e. kwa kuwaua bila kwenda mahakamani na ukweli ukajulikana siku zote husababisha baadhi ya watu wema kuuawa. Polisi siyo malaika, hivyo kuna watakaotumia huu mwanya kutimiza malengo yao maovu. Je, kama kwa mfano ulikuwa umewachomea polisi kula rushwa na wakafukuzwa, wale marafiki zao waliopona hawataweza kutumia mwanya kama huu kukumaliza? Kiufupi ni kuwa polisi mwovu anaweza kukufanya lolote kwani atasingizia kuwa ulikuwa panya road. Pia kuna wengine watatumia huu mwanya kudai rushwa hata kama huna kosa. Hivi ukikamtwa na ukaambiwa kuwa usipotoa kiasi fulani cha fedha utafanywa kama panya road utakataa? Na pia kuna wengine watakaouawa kwa makosa. Hujawahi kuona mtu anashukiwa kuwa ni mchawi wakati hana uchawi wowote? Hivi mtaani kama kuna majirani wenye chuki na wewe wakikuchongea kuwa ni panya road huoni kuwa utakufa bila kufanya kosa lolote? Hebu acheni kuwa na akili fupi kama za ndezi!

una akili nzuri ya kutambua kuliko wachangiaji wooote humu mburura umeeleza vizuri lakini hawatakuelewa
 
Sasa hivi pametulia. tofauti na zamani kabla ya hii operation...
 
Uzuri Kwa Sasa Polisi Wana teknolojia kutoka Marekani ,China, na Israel Kwa hiyo hata Hawa Panya rod. Humu watasakwa TU mana wanahamasisha uhalifu na kuzua taharuki kuwa Polisi wameua watu wengi na upumbavu Mwingine
Hahahha kwahiyo humu napo kuna panya road
 
( A man who has nothing to lose is a dangerous man. ) panya road hawana lakupoteza....enyi nyie wanasiasi vipofu mnakuwa wapi pindi PANYA ROAD WANAPO WAUA RAIA WASIO NA HATIA? mbona mnakuwa kimya, why it inapokuwa vice verser ndipo tu mnatema nyingo?? hii inanipa kufikiri kuwa yawezekana matukio ya kiarifu ni mtaji wa kisiasa kwa WAPINZANI wa Nchi hii Vijana wataftaji kwa jasho letu ni wakati wa kuzinduka hawa Wapinzani ni wapotoshaji
 
Tatizo Vijana Wa Siku hizi hamfanyi utafiti.
Tanzania Ina Majeshi Matatu.
Jeshi la Wananchi
Jeshi la Polisi na
Jeshi la magereza

Na Majeshi Yote hayo Yana Vikosi maalumu waliofumzwa matunzo maalumu Ndani na nje ya Nchi Kwa gharama Kubwa ya Kodi zetu.

Ukizingua kwenye haya Majeshi unazinguliwa.

Magaidi wanataka kurudi kama Kibiti na wanawatumia wanasiasa mana pesa zinazofadhili ugaidi ni nyingi sana. Zinatoka Mashariki na magharibi Kwa manufaa ya Nchi hizo HUKO nje .

Polisi wakibweteka na kumsikiliza Abdul Nondo wajue wamekwisha mana huyo ni mshika Kibiti Wa Vikundi vya kihalifu vinavyojifungamanisha na Siasa.
Jeshi ni moja tu (jeshi la wananchi) polisi na magereza ni raia wakakamavu hilo ndio tambua leo
 
Back
Top Bottom