Complicator
JF-Expert Member
- Aug 23, 2013
- 2,198
- 3,580
Kampeni za uchaguzi mkuu wa uraisi,ubunge na udiwani 2020 zimevuka wiki ya kwanza sasa huku kila chama kikihaha kuzunguka nchi nzima kuomba kura na kuungwa mkono na wananchi,yafuatayo ni mambo matano (5) niliyoyabaini baada ya hili wiki moja.
1. CHADEMA ndio Chama Kikuu cha Upinzani chenye kuweza kutoa ushindani mkali kwa CCM
Baada ya Magufuli kuingia ikulu 2015 kazi ya kwanza aliyoamini itamfanya aongoze kwa kutulia basi ni kuzuia platform zote zinazoweza kuwapa wanaotaka uraisi kuonekana,kumbuka mwisho wa uchaguzi mmoja ndio mwanzo wa mwingine, Magufuli alizima Bunge live kupitia waziri wa habari muda huo bwana Nape alitangaza wazi kwamba sasa siasa basi hadi Uchaguzi mwingine, akazuia mikutano ya vyama vya siasa hasa CHADEMA, akawabana kwa kuanza kuwarubuni viongozi ndipo likatokea wimbi la waunga mkono juhudi...wakafanya kila aina ya hujuma na propaganda kuwafanya watu waamini kwamba hakuna kama Magufuli (katika hili alishinda)
Kuliibuka wimbi kubwa la watu hasa vijana kujinadi wazi kuwa wao ni CCM, wengi wakirubuniwa kwamba kwa kusema hivyo watapata connection za kazi na urahisi wa kufanya mambo yao n.k
Miaka mitano baadaye ndio hii, kampeni zimeanza na tumeona kumbe yote yaliyofanyika hayakufua dafu, upinzani ni kama dini utawakataza watu kwa muda na watakutii sababu ya nguvu ya dola unatumia, siyo kwa sababu wamekuelewa...tofauti na ilivyotegemewa mwamko umekua mkubwa sana kwenye kampeni za CHADEMA ambako hakuna msanii wala burudani yoyote kabla ya mkutano.
CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani na wana nafasi na muda wa kufanya makubwa na kuchukua dola siku moja, waliyoyapitia miaka hii mitano ni makubwa kama wasingekuwa imara tusingekuwa na CHADEMA leo hii.
Hongereni sana.
2. CCM inafanya kampeni kwa mazoea/wanajiamini
CCM wao wanafanya kampeni za nguvu,kwa sasa ni kama kwa mazoea sababu mgombea wa Uraisi wao Magufuli ni kama anafanya mikutano ya kawaida kabisa ile ya ziara za Uraisi,amesimama zaidi kama raisi kuliko mgombea wa uraisi kitu ambacho anawanyima watu wengi cha kusikia
Chama cha mapinduzi kilitakiwa kujikita katika kujibu hoja za wapinzani hasa CHADEMA. Uhuru, haki na maendeleo VS kazi tu inaendelea. Hapa tu palitosha kupasuana kwenye majukwaa, kampeni zimekosa mvuto kwa CCM sababu hawajibu hoja, hawazingumzii ilani yao iliyopita imetekelezwa kwa kiasi gani ahadi kama
1.milioni 50 kila kijiji
2.mchakato wa katiba mpya
3.uhuru wa vyombo vya habari
4.usalama wa raia na mali(utekaji)
5.hali mbaya za maisha ya watu
Kampeni za 2015 hoja kubwa ya CCM ilikuwa ni VIWANDA, mbona sasa hivi hakuna anayesemea kiwanda chochote, je vimejengwa na kutosha kutufikisha kwenye uchumi wa kati?!!Raisi kutosafiri nje ya nchi siyo sifa na kutosafiri kwake kumeleta tija gani?! hii inapaswa kutolewa maelezo ya kina
Miradi mikubwa iliyoanzishwa imeleta tija gani au inatarajiwa kuleta tija gani kwa wananchi masikini/yaani tukinunua ndege mpya 11 masikini kijijini asiye na mia ya panado ananufaika vipi?! Kampeni ingekua rahisi na za kuvutia kama mgombea angejikita kwenye mambo hayo na mengine anayotarajia kufanya kupitia ilani yao. Ila kwa sasa hazivutii, hakuna kitu kipya unapata zaidi ya maneno ambayo tumeyazoea kwa miaka yote mitano ni yale yale.
3. Hashim Rungwe Spunda kapuuzwa lakini hoja zake ni zaidi ya wengine haswa kwa wananchi masikini.
Ilani za vyama vyote zinazungumzia miradi, sheria, wafanyakazi, wafanyabiashara, kodi, madini na mavitu makubwamakubwa tu ambayo kuna watu hata hayawagusi moja kwa moja. Tukirudi kwenye maisha halisi ya watu mahitaji yao ni CHAKULA/MAJI, MAVAZI NA MALAZI haya ni mambo basic kila mtu anataka halafu ndio aanze jitafutia ziada
Kundi la watoto linatengwa sana,ni kweli tunawapa elimu bure je ni vipi kuhusu lishe yao? ,issue ya ubwabwa kuku ni neno tu la jumla kumaanisha watoto wanahitaji lishe wakiwa shule ili kuwafanya hiyo elimu bure walifaidi, kwa hali mbaya za maisha watoto wengi wanashinda njaa mashuleni, hakuna motivation yoyote ya watoto kubaki shule hii inachoche utoro n.k. Hii hoja natamani sana CCM na CHADEMA waiibe na waijenge vizuri ili kuinadi, ni ya msingi sana kiukweli, kwanini watoto wasipate chakuna cha mchana shule?! Rungwe anatuulizwa, kwani tunawahi wapi?!!
4. ACT-Wazalendo, mbadala halisi wa CUF. MEMBE anawavusha tu ila siyo mgombea sahihi hasa akiwa upinzani.
Kinachoendelea sahivi mikoa ya kusini na visiwani ni rasmi sasa kwamba ACT ni chama kikuu cha upinzani zanzibar na mikoa ya pwani ya kusini...kimeshika vyema nafasi ya CUF huko. Benard membe ni kama katumika tu lakini hastahili kugombea,wala hana lolote la maana zaidi ya kuwa candidate pale ni wale wamezoea siasa za kiungwana huko CCM ndani ya chama ambako kila kitu kinatoka kwa order na msaada wa dola (rejea bashiru)
Membe hana ushawishi nje ya CCM huo ndio ukweli,kwahiyo kama ni plan kumpandikiza upinzani basi intelijensia ya CCM this time imefeli kabisa. Membe anagombea ili kusubiri muda wa ZITTO KABWE ufike rasmi agombee, 2025 atagombea ZITTO/LISSU kwa muunganiko wa vyama kusimamisha mgombea mmoja. Membe plan imefeli kabisa kuchallenge uraisi, hawezi kumchallenge magufuli na hatoshi hata kidogo kumpa ushindani nje ya CCM labda ndani ya chama huko.
5. Upinzani Tanzania unazidi kuimarika,2020-2025 tutashuhudia ukandamizaji zaidi,na 2025 ndio mwisho wa CCM kubaki madarakani.
Mwaka huu CCM itashinda,kwa mbinu yeyote ile ila sasa upinzani utapitia tena tanuru la moto zaidi, kama ambavyo farao alizidi kupata kiburi wakati wa mapigo ndio watawala watavyokua kwa lengo la kuua kabisa upinzani, ila sasa 2025 CCM itapasuka tena na hakutakua na namna tena ya kuiokoa kufanya ibaki madarakani.
Tuendelee kuijenga nchi yetu.