Niliyoyanena kuhusu watu X na Y yametimi.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ninajivunia kukomboa kundi kubwa la watu ambao kimsingi walikuwa wanaenda kutapeliwa na wanawake X na Y ambao walitaka kutumia mgongo wa JF kujipatia pesa kwa kigezo cha kuandaa party.

Kiukweli nilikuwa nina mashaka nao sana hata kama miaka ya nyuma kweli walikuwa wanaandaa party na zinafanikiwa ila kulingana na michango yao ya mwaka huu ilikuwa inaonesha wana shida kwa kiasi gani na ni mbaya sana kumkabidhi mtu pesa haswa yule ambaye ana matatizo ya kiuchumi.

Mbali na hilo niliwahoji itakuwaje watu wakatoa michango halafu kwa bahati mbaya party isifanyike watafanya utaratibu gani wa kuwarudishia watu pesa zao, kiukweli walinitukana sana tena kwa id's tofauti tofauti badala ya kutoa majibu ya kuridhsha ila nikaamua kukaa kimya tu.

Ninakumbuka pia nilishauri ni vyema wachague sehemu halafu kila mmoja aje na pesa yake mkononi sio masuala haya ya kuchangishana mitandaoni mbaya zaidi kwa watu ambao huwajui kabisa sura zao.


Nina imani yale mashaka yangu yametimia party haijafanyika na waliotoa pesa ambao ninadhani hawafiki hata 10 pesa zao zimeenda na maji ,poleni sana kwa hilo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
Aibu nimeona mimi🤣🤣🤣🤣🤣mwanaume kama binti
 
Dhahiri namna gani Wanaume tunazidi kubaki Wachache.

Watu wamejitolea kwa member watakaopenda kukutana wawe pamoja angalau kwa masaa machache, nilitegemea kama mwanaume ungekuja kuhoji wamekwama wapi ili uwasaidie kimawazo, Pathetically unakuja na furaha kwa kushindwa kwao!

Wadada hili nalirudia tena, sio kila anaepizi ni Mwanaume!
 
Waandaaji wa hiyo pati tieni neno hapa ili kuleta uaminifu kwa wengine kama party itaandaliwa tena kwa siku zijazo,je party ilifanyika? na kama haikufanyika tatizo lilikua ni nini? nadhani mnahitaji kuliwekea ufafanuzi hili jambo zaidi kuliko tu kumtukana mleta mada,watu kama hawa hujibiwa kwa hoja na sio kwa matusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…