Niliyoyanena kuhusu watu X na Y yametimi.

Niliyoyanena kuhusu watu X na Y yametimi.

Dhahiri namna gani Wanaume tunazidi kubaki Wachache.

Watu wamejitolea kwa member watakaopenda kukutana wawe pamoja angalau kwa masaa machache, nilitegemea kama mwanaume ungekuja kuhoji wamekwama wapi ili uwasaidie kimawazo, Pathetically unakuja na furaha kwa kushindwa kwao!

Wadada hili nalirudia tena, sio kila anaepizi ni Mwanaume!
[emoji2955]
 
Mkuu shukurani
Watu kama nyie mkifanikiwa watu wanabak wakijiuliza mbona furan mambo yanaenda tuu, hajawai kulia...
Kumbe una mema mengi.

Achana nao wasiopenda ukweli
Watapata tabu sana mm nawatabilia kabisa na pia imeandikwa, watapata mapigo yao tu.
Ninajivunia kukomboa kundi kubwa la watu ambao kimsingi walikuwa wanaenda kutapeliwa na wanawake X na Y ambao walitaka kutumia mgongo wa JF kujipatia pesa kwa kigezo cha kuandaa party.

Kiukweli nilikuwa nina mashaka nao sana hata kama miaka ya nyuma kweli walikuwa wanaandaa party na zinafanikiwa ila kulingana na michango yao ya mwaka huu ilikuwa inaonesha wana shida kwa kiasi gani na ni mbaya sana kumkabidhi mtu pesa haswa yule ambaye ana matatizo ya kiuchumi.

Mbali na hilo niliwahoji itakuwaje watu wakatoa michango halafu kwa bahati mbaya party isifanyike watafanya utaratibu gani wa kuwarudishia watu pesa zao, kiukweli walinitukana sana tena kwa id's tofauti tofauti badala ya kutoa majibu ya kuridhsha ila nikaamua kukaa kimya tu.

Ninakumbuka pia nilishauri ni vyema wachague sehemu halafu kila mmoja aje na pesa yake mkononi sio masuala haya ya kuchangishana mitandaoni mbaya zaidi kwa watu ambao huwajui kabisa sura zao.


Nina imani yale mashaka yangu yametimia party haijafanyika na waliotoa pesa ambao ninadhani hawafiki hata 10 pesa zao zimeenda na maji ,poleni sana kwa hilo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
 
[emoji23][emoji23] shenzi sana hawa walikuwa wanatafuta Pesa za skukuu.. bad enough wamekuwa nje ya malengo ya Makusanyo yao.
Sidhani kama wachangiaji walifika 10
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu shukurani
Watu kama nyie mkifanikiwa watu wanabak wakijiuliza mbona furan mambo yanaenda tuu, hajawai kulia...
Kumbe una mema mengi.

Achana nao wasiopenda ukweli
Watapata tabu sana mm nawatabilia kabisa na pia imeandikwa, watapata mapigo yao tu.
Inshaallah.
 
Je kama wamefanya?

Feedback ni muhimu iwe wamefanya au hawajafanya. Fikiria kama wamefanya na hawajatoa feedback halafu huku kuna hizi kelele unadhani wadau watabaki na majibu gani?

Na hili siyo hapa tu, watanzania wengi tuna shida ya kutotoa feedback, hasa kama jambo halikifanikiwa ilivyopaswa, unakuta mtu umemtuma kazi fulani, anakwama mahali halafu anajikausha mpaka ule muda mliokubaliana unapita, mpaka wewe umpigie ndo unapewa taarifa au anakurusha ntakupigia! Tunahitaji kubadilika kwa kweli.
 
Back
Top Bottom