Niliyoyaona Jana kwenye mechi ya Yanga

Niliyoyaona Jana kwenye mechi ya Yanga

Rule L

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2020
Posts
1,846
Reaction score
2,754
Hii ni makala ambayo nitaelezea kidogo yaliyokuepo Jana.

Baada ya shamrashamra za kujiandaa kupokea ubingwa ilibidi lipigwe kabumbu Moja matata sana,, kabumbu ambalo lilianza kwa furaha kedekede.

Lakini kipindi mchezo unaendelea nyuso za wapenda soka walioipenda young African's zilikosa furaha, mawazo yakajaa vichwani mwa Hawa wapenda soka.

Swali ni je, nani kaleta huzuni katikati ya maelfu wa washabiki Hawa? ni kijana kutoka Zanzibar anaitwa feisali salum muite fei toto.

Huyu alifanikiwa kuziweka nyuso za wanayanga kuwa na maswali mengi sana, goli mbili alizoweka kambani zilileta pressure kwa kila mwanayanga.

Ni vita ya kiatu Cha mfungaji Bora ndo inacheza vichwani mwa kila mwanasoka ambaye aliamua kumchagua mchezaji wa kumpa furaha.

Kwa mtu asiyejua kinachoendelea huenda angeshangaa sana, timu imetangaza ubingwa, bado inaongoza kwa 2-0 lakini kwanini hawana furaha? Kimewakuta nini?

Ni nani anayesuburiwa kuleta furaha na kuindoa huzuni yote mioyoni mwa Hawa wapenda soka? ni kijana mmoja ambaye kuna baadhi ya watu waliponda na kuushusha uwezo wake.

Si mwingine bali ni Stephani Aziz ki,
Si Mashabiki tu ambao walimkatia tamaa, bali hata yeye alijikatia tamaa.

Kuna msemo hua upo japo hauna nguvu kutokana na kutimizwa mara chache kwa msemo huo.
Msemo usemao kwamba (Haijaisha mpaka iishe)

Na ndipo ikawa dakika ya 90+3 mpira wa cross uliotoka mguuni kwa Joyce lomalisa kumwendea Aziz ki.

Mpira ukiwa unamuendea alitafakari kwa haraka sana, akapiga hesabu zake kichwani ikabidi afanye maamuzi magumu kwake yeye huku akijua kabisa kua hii ni golden chance, nikipoteza hapa sina changu tena, ikabidi autwange kichwa ule mpira. na ukajaa kambani

Ziliibuka kelele kali sana zenye furaha isiyopimika, sio watoto sio vijana wala wazee wote walilipuka kwa furaha ya viwango vya juu sana, wanayanga wakafufuka toka kwenye wimbi la huzuni na kusahau yote.

Kumbe hata kama yanga angeshinda 10_0 pasipo Aziz ki kufunga ilikua ni kazi Bure tu.

Hongera ziwafikie wachezaji wote kwa nguvu kubwa waliyoitumia kuhakikisha washabiki wake hawarudi majumbani na huzuni.
 
Hii ni makala ambayo nitaelezea kidogo yaliyokuepo Jana.

Baada ya shamrashamra za kujiandaa kupokea ubingwa ilibidi lipigwe kabumbu Moja matata sana,, kabumbu ambalo lilianza kwa furaha kedekede.
zaji wote kwa nguvu kubwa waliyoitumia kuhakikisha washabiki wake hawarudi majumbani na huzuni.
Ni kweli kwa wanayanga nguvu zote sasa zinaelekezwa kwa Azizi Ki awe mfungaji bora.
 
Wote tunamaliza na game dume ila kwa yanga ni ngumu zaidi ingawa uwanja unatoa advantage na kwa Azam wako na Geita na vita Yao ya nafasi ya pili plus tahadhari ya FA cup final
Huenda Fei akawa mfungaji bora ngoja tuone hiyo kesho
 
Back
Top Bottom