CARDLESS
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 7,840
- 15,918
Habari zenu ndugu, wadau na wanabodi.
Jana (08/10/22) kulipigwa mbungi la klabu bingwa Afrika kati Yanga vs Al Hilal, na matokeo yalikuwa sare ya 1-1.
Binafsi mimi ni mfuatiliaji wa mpira tangu miaka ya mwishoni mwa miaka 1990. Na ni mpenzi mkubwa na Mwanachama wa YANGA, na huko Majuu basi mimi ni UNITED lialia.
Twende moja kwa moja kwenye mada yetu. Jamani mpira ni sanaa, mpira ni teknikali, mpira ni kazi nk.
Mechi kwa ujumla ilikuwa nzuri kwa pande zote (Kimchezo) na si (Kimatokeo). Kwa ujumla haya ndio nimeyaona na nitaweka zaidi kwa manufaa ya timu yangu ya YANGA. Nina imani yupo yeyote kwenye cycle ya timu yetu ataona hili bandiko, na hapa nitaweka hasa mapungufu ambayo kama tutarekebisha basi tutashinda ugenini kama ilivyotekea miaka kadhaa nyuma
YANGA VS HIGHLANDERS (1-1) AWAY (0-2) Magoli ya Iddy Moshi
YANGA VS APR (1-1) AWAY (2-1) Magoli ya Juma Abdul na Kamusoko
YANGA VS TOWNSHIP ROLLERS
(1-1) Home, AWAY (0-1). Goli la Balinya.
Tuje kwenye mechi hii sasa.
1. Mabeki
Jamani kila siku tunasema hapa, Yanga unaposajili wachezaji wa kigeni hakikisha wanacheza, hawa wachezaji wana mambo makuu ma3 hadi ma4
1. Wanataka kujiuza timu kubwa zaidi.
2. Wanataka kuonesha wana thamani fulani
3. Wazoefu kwenye michuano
Sasa basi YANGA tulimuacha Yasin Mustafa na Kumsajili LOMALISA, Kocha NABI lazima ajue ni bora mara 100 aanze Lomalisa kuliko Kibwana, Lomalisa ana utulivu, kucheza slow ni aina yake ya uchezaji, tuliwahi kuwa na CHIBE CHIBINDU hakuwa mwenye speed mno ila alikuwa anajua mpira. Game ya leo imeharibiwa kwa kiasi kikubwa na KIBWANA, mara zote amekabia ndani au kwa macho. Game ijayo binafsi na kwa uzoefu wangu hafai kuanza, tunahitaji mzoefu mwenye kujua sasa napanda sasa nakaba tu. Umbo dogo ni faida kwa Al hilal.
Pia beki za kati, sasa ni wakati wa kuanza kumuamini Bacca, Yes hata Canavaro alikuja kama mchezaji mdogo lkn alipewa nafasi alifanya vyema, kima, stamina na control ina mbeba mno.
Bangala asogezwe namba 6, namba abaki job na 5 amalize Bacca. Hapa tutapata faida kwa utulivu wa Bangala, na Bacca, lkn pembeni una Djuma na Lomalisa ambao licha ya uzoefu wao ila pia maumbo yao yanawabeba.
2. ENEO LA KIUNGO
Piga bench Aucho, ndio aanze benchi, weka namba 6 BANGALA, na 8 FEISAL, ndio Ni kosa kubwa kumrudisha Namba 6 Feisal kutoka no. 10. Balansi timu kwa kuweka mtu mbele ambaye mipira inayotoa hovyo anaweza amua matokeo.
3. ENEO LA USHAMBULIAJI + WINGS
Jamani hizi game zinahitaji matokeo tu. Ubovu wa Moloko na hata Kisinda umepekea matokeo mabaya. Hawaamui kama timu always mipira yao inatoka nje au inakuwa blocked.
Tuanze na FARID kushoto na MORRISON kulia, hapa timu itabalance sana. FARIDI atakaa upande wa LOMALISA ambaye anaweza kushambulia na kiasi mzito kurudi ambapo FARID yy anaweza kushuka na kukaba kwa wakati na kufuta makosa.
MORRISON mzuri kushambulia ila kusaidia nyuma ni mvivu hivyo upande wa Djuma atacheza kwa uhuru maana DJUMA anajua kukaba.
MAYELE mbele apunguze ubinafsi kidogo, sawa anataka kutetema lkn kuna nafasi hawezi kufunga basi apasie wenzake ili tushinde kwa urahisi
AZIZ KI. Anacheza vizuri ila hana uhuru, NABI amwache huru yaan free role, awe anazunguka uwanja mzima, kama afanyavyo Messi, asimkatie kipande, hawezi tusaidia. KI acheze uwanja mzima anavyoweza ili kuwahamisha mabeki muda wote, hii itamsaidia MAYELE au MAKAMBO kufunga Kirahisi.
Hitimisho, Yanga wana nafasi. Nafasi hii inategemea KOCHA aachane na Vikosi vya RUVU SHOOTING, apange wanaume sio watoto.
Naweka pesa naiona YANGA akisonga mbele MAKUNDI akirudia comeback zake za kibabe kama za miaka kadhaa nyuma huko.