ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
2022 tulipata kazi fulani nanyumbu Ilikuwa tunaifanya katika kambi za Jeshi ni special task kuwafanyia geo survey so tulipomaliza tu wenzangu wakarudi home mimi nikawa interest na stori za Msumbiji nikatamani kwenda. Kweli nikapata rafiki fulani anaitwa Kwimba ni mtu mzima kidogo ila chapombe huyo mkatili kweli kweli anakunywa 24 hours ila sio mjeuri, akakubali kwenda kunitembeza Mueda Kwa siku tatu. Yeye alikuwa anayo ile pass ya miezi sita ila mimi sikuwa nayo na hatukuamua kwenda Mtwara kukata hio pass uhamiaji tulichofanya tukawapa rushwa askari picha linaanza rushwa yenyewe Ilikuwa ni konyagi na k vant kubwa wakakubali walikuwa watatu.
Basi tuliingia Mueda Mida ya mchana saa tisa rafiki yangu huyu mmakua wa masasi alikuwa na watu wa ukoo wake Kule aisee Kule wanathamini sana ukoo yaani ukoo una nguvu sana. Mtu yupo tayari akuamini fasta na kukuchukua mkae kwake kisa tu amejua ni wa ukoo wake hata kama una skendo za Ukorofi huko ulipotoka.
Kesho yake rafiki yangu nilienda naye alikwenda kuonyeshwa makaburi ya babu zake mimi nikabaki na ndugu zake tunakunywa pombe aisee kwanza mueda ni kama wilaya ila ukilinganisha na kwetu huku ni kama mkoa. Niliyoyaona Kule mueda
1. Hakuna sheria zozote zinazosimamia suala La nyama Pori. Huku kwetu sheria nyingi ni za ajabu yaani hata kanguruwe Pori tunauziana kama bangi yaani Kwa kificho mno. Kule msumbiji hamuwezi kuwa mnakunywa pombe bila ya kula nyama za kutosha yaani ukienda center ya kijiji unakutana na wachuuzi wa nyama hata zaidi ya aina za Wanyama 10 ni wewe tu unachagua. Huku kwetu hata ng'ombe wako akipata ajali ukaamua umchinje uuze rejareja bado watakusumbua askari wenye njaa hata kama dokta amethibitisha.
2. Pombe Kule ruksa kabisa muda wowote mmekaa bar anakuja mwanajeshi anaweka bunduki pembeni mnakunywa na ni muda wa kazi hapo asubuhi kabisa saa tatu. Na Kule kazi ya jeshi haina thamani sana wanakuona kama mgambo ila sisi huku jeshi ndo wako top. Kule kazi ya maana uwe fundi au sekta ya afya mfano dokta au hata muuguzi tu Kule ni bonge la deal.
3. Bunduki nje nje Mpaka kuna watoto niliona wanawinda na bunduki ya baba yao ila wameweka goroli wametoa risasi. Kule hata wanawake Wana silaha bastola hizi zimejaa unafika lodge na danga lako unashangaa anaweka silaha kwenye Meza.
4. Watoto wa kike wenye ujauzito ruksa kuendelea na shule. Na Kule hakuna cha form six wala college yaani ukimaliza form ya Kule tayari una fani yako. Sisi huku tunapambana Mpaka kuchukua master degree Kule aisee wasomi hakuna sana hawafagalii.
5. Kilichonifurahisha ni kuhusu mavazi aisee hawajui kuvaa wanavaa vaa makoti yaani Kule ukikaa week unashangaa wenyeji wanakuja kukuazima jeans lako ili wakaonekane huko kwenye ngoma maana ngoma huko ni Sanaa kubwa inayotisha wanapenda sana. Yaani nguo moja kuazimana watu watano ni kawaida.
6. Mabaki ya wareno aisee unakutana na mtoto mweupe ana nywele Mpaka mgongoni ila anatokea nyumba ya udongo ila Wana nyumba nzuri na magari mazuri kuliko sisi na pikipiki za kizungu nyingi Sana na mademu wa Kule wanawapenda sana wa tanzania.
7. Mawingu ya msumbiji na Tanzania ni tofauti yaani sijui niielezee vipi hii hali ila ukiingia tu msumbiji baada ya kuvua mto ruvuma unakutana na hali fulani tofauti na ya kwetu angani in short ni kuzuri kuliko anga letu hata great ruvuma yenyewe inachangiwa na mito kutoka msumbiji zaidi ya 60% hivyo wanapata sana vyakula hakuna njaa.. Yaani Kule nilichokiona kuhusu wamiliki wa hotels hawanunui vyakula Bali wanakuwa ni wakulima wakubwa wamevuna in short hakuna shida ya njaa kama huku kwetu unaweza kukaa Mpaka mchana hujala chochote.
8. Kuhusu mitandao ya simu sijui wame set nini yaani Kule hakuna kujiunga ukinunua tu vocha unaweka unaongea sana dakika za kutosha kabisa.
9. Nyerere na sokoine ndo watu popular zaidi Kule. Unakutana na majina ya barabara na shule ya nyerere na sokoine Kwa wingi na barabara zao nzuri Sana yaani zile alama za barabarani zipo quality sana.
10. Magari kama ma v8 au ma cruiser haya ambayo hata matajiri wanamiliki huku kwetu Kule ni special Kwa ajili ya viongozi pekee wa serikali na wakijeshi nahisi kama labda kuna sheria inayokataza watu wanunue gari zenye Hizo hadhi.
Yako mengi niliienjoy sana ila Kule aisee pombe wanakunywa sana Kule kitu haramu kabisa ni bangi yaani usikutwe unavuta bangi ila pombe kunywa anytime.. Umbali wa kutoka nanyumbu (mangaka) Mpaka mueda ni chini ya km 100.watu wa mueda Bara ni wazuri wamakonde na wamakua wanajua kiswahili japo sio sana hata ukienda border ya mkenda songea na wenyewe hawajui kiswahili wanajua sana kireno.. Ila Wana utu sio kama wapemba wa msumbiji pwani huko Wana roho mbaya na ndo penye vita vita ila huku mueda ni peace kama ilivyo bongo tu.
Nauli nakumbuka nililipa kama elfu 30 na kitu.