streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 475
Naamini Kila mtu anajua kuwa maisha ni safari, safari yenye wingi wa changamoto za Kila Aina.
Kila mmoja kapitia Mapito yenye wingi wa simulizi zenye kuleta hisia tofauti.
Lakini Kwa pande wangu nimekutana na changamoto ya upofu iliyofanya nikashuhudia mambo yafuatayo:-
1. Nilimuona shetani kama malaika.
Kiukweli inaweza kutatiza kidogo Lakini ndio ukweli Wenyewe huo. Upofu ulinifanya nione mambo wanayofanya baadhi ya viongozi wa nchi, wazungu na baadhi ya viongozi wa dini kuwa yana malengo mazuri Kwangu/ kwetu, kumbe ni njama na ulaghai ili waweze kutimiza adhima yao ya unyonyaji. Kwa mfano rejea kipindi cha umisionary, globalization, misaada ya wazungu, na hata vyama vya siasa hapa nchini kwetu. Upofu ulinifanya niwaone malaika kumbe ni mashetani wa hatari.
2. Niliona mwafrika ni mtu aliyelaaniwa.
Kiukweli upofu sio tu ulemavu bali ni tatizo baya sana. Kiukweli niliwaona watu weusi kuwa wamelaaniwa kutokana na rangi ya ngozi yao na uduni wa maendeleo yao. Kumbe haikuwa ivyo waafrika ni bara ambalo lina baraka za Kila namna, Mali asilia za kutosha, amani, upendo na vitu vingine vingi. Nikagundua kwamba wazungu wanatuaminisha tuamini kuwa tulilaaniwa ili tujisahau na tuendelee kuwa nyuma ya muda.
3. Niliona madhaifu yangu na kuyachukua kama sababu ya kutenda uovu.
Nilipokuwa sina macho niliufanya udhaifu wangu kuwa sababu ya kutenda dhambi. Nilijiona Mi ni mwanadamu sijakamilika ivyo nikajipa tiketi ya Kua mlevi, mzinzi na mengine mengi. Sikujua kua udhaifu upo sio tuutumikie bali iwe sababu ya kuenenda vyema ili tuutokomeze.
4. Niliona sitakuja kuona tena.
Kiukweli ni changamoto kubwa hasa unapokata tamaa, niliamini nitakua ivi milele kwamba sitakuja kuona, kufanikiwa, kusoma, kuoa/kuolewa, kuokoka na mengineyo. Ila baada ya kupata macho kila jambo liliwezekana.
Ivyo naamini kila mtu alikua ana upofu kwenye jambo fulani au kipindi flani. Hebu tueleze uliona nini ambacho hakikuwa sahihi ?