Niliyoyaona nilipotembelea mkoani Tanga

Niliyoyaona nilipotembelea mkoani Tanga

wadada wao pia hawana big nyashi nilikua totally disappointed
Weeeeh weeeeh weeeeh!
Tanzania HAKUNA WENYE BIG NYASH KUWASHINDA TANGA.
Tembea Korogwe,Bumbuli,Mashewa,Usambara,Lushoto ukaone hizo NYASH mzee.
 
Tanga kuna ardhi ,na uoto mzuri lakini maendeleo hamna, nafikiri MLOZI mkuu wa Tanga kuwa duni, ni walipuuza elimu ya darasani na kuzingatia tamaduni za kiarabu kwa sehemu kubwa ,sehemu akiyopita Mwarabu kakueleweki kimaendeleo.
Mbega,Iringa,Njombe,Katavi je huku kuna waislamu wengi!?
Mbona huku nako masikini wa kutupwa!?
Laumuni akili zenu za kipumbavu za kiweusi msilaumu dini.
Mbona hao wenye dini Saudi Arabia wameendelea Kuliko taifa lolote hapa Afrika!?
 
Kama Tabora ,Lindi, Mtwara,Rukwa na Mafya kwa baadhi tu, kwa kimombo tunasema are less developing regions sababu kuu kupelekea hivi Mwarabu hukuweka msisitizo kwenye elimu alafu .
Acha kuongea upumbavu wewe.
Mbona waarabu wenyewe wana maendeleo!?
Laumuni akili zenu nyeusi kama ngozi yenu.
 
Tunaendelea tulipoishia.

Basi ilikuwa usiku, ikawa usiku sana, alfajiri na asubuhi ikawadia. Usiku huo sikulala mbali sana na niliposhukia, ni maeneo hayo hayo tu mkabala na round about, kama unatokea Dar es salaam unanyoosha kupita round about mkono wako wa kushoto kuna Lodge na hotel ya gholofa utachagua mwenyewe mimi nililala wapi kati ya hizo sehemu mbili

Ratiba yangu ilikuwa kutembelea maeneo ya mjini kati, makumbusho ya urithi Tanga, kwenda kule Amboni kwenye mapango, kufika Raskazone beach, kutazama makabuli ya vita ya kwanza na ya pili ya Dunia, kujionea bandari kongwe ya Tanga, kuingia ndani ya uwanja wa mkwakwani, usisahau Stesheni ya reli, kufika kule daraja la Amboni, soko la samaki, kuoga maji moto kule Galanos na maeneo mengine yote ambayo ningefanikiwa kuyafikia ikiwa ni pamoja na kuzishangaa barabara zao za namba na kupumzika maeneo tulivu ya Tanga pazuri

Unajua kufanya utalii wa miji hasa hapa nyumbani ni bora sana kwakuwa unaenda kuona moja kwa moja yale yote ambayo unakuwa unasikia kwa watu na mitandaoni, mfano niliambiwa Tanga watu wanalala mapema, tuliambiwa huko uchawi nje nje, na ile habari ya nyumba mganga nyumba naniliu sio kweli aisee, sio kweli kabisa. Maeneo mengi biashara zinafanyika hadi usiku sana na zile simulizi za watu wavivu wavivu sidhani kama ni kweli.

Basi nikiwa na mwenyeji wangu sasa, hii ilikuwa asubuhi ya kwanza ndani ya TA, nilichagua kuanzia matembezi katika mapango ya Amboni mbali kidogo nje ya jiji lao. Binafsi mapango haya nilikuwa napata kuyaona kupitia televisheni hasa kupitia safari channel, kiukweli hawa jamaa wanafanya vizuri na nimeweza kufika maeneo mengi kwa mchango wao mkubwa wa kutuonesha vivutio na maeneo ya kihistoria tunayopaswa kuyatembelea sisi kama watanzania na watalii wa ndani, hivyo nilitamani sana siku moja kufika hapo na kujionea kwa macho yangu kisha kuwahamasisha na watanzania wengine kufika huko.

Tulipanda hiace na ni utaratibu mzuri niliona huko, kusalimia ni jambo jema sana, na ukisema Assalam aleykum utakuwa umefanya jambo jema zaidi. Umbali kidogo tulishuka na kusogea hadi eneo linaloitwa Kisosora hapo hatukuchukua muda mwingi sana, nilipenda kufika hapo na angalau kupata picha ya kumbukumbu katika eneo aliloishi Mr Ebo kwa muda mrefu.
IMG_20240407_085104-01.jpeg

pochani nikiwa katika eneo la Kisosora
Sasa safari iliendelea tena na wakati huu tukitumia usafiri binafsi tuliozaliwa nao, hapo ilikuwa ni mguu kwa mguu na unajua kwa njia ya kutembea kwa miguu unapata fursa ya kuona kila kitu, kusimama na kuongea na wenyeji, kununua vitu, na kuona mandhali bila kupitwa na tukio lolote njiani, usisahau pia unaweza kupata mke au mchumba. Hivyo tulitembea kwa miguu kwa umbali mrefu kidogo hadi pale tulipowasili katika geti kuu la kuingia ndani kabisa zilipo ofisi na mapango ya Amboni. Kutoka getini utapaswa kutembea umbali wa kama mita 500 hivi au zaidi, huku ukikatiza kimsitu kidogo na kisha kuona geti dogo linalokuongoza moja kwa moja hadi mapokezi. Ukiwa hapo utapata maelezo mafupi na utaratibu wote, utalipia na kupewa risiti na karatasi yenye majina yako na inayoonyesha sasa umetembelea mapango ya Amboni. Kiukweli binafsi nilitokea kuipenda sana kutokana na jinsi ilivyobuniwa nimeitunza hadi leo hii.

Sisi na muongozaji wetu tulizama pangoni, tukaingia kwenye pango la uzazi, tukapanda mlima kilimanjaro, tulipanda ndege na kuona makumi elfu ya mapopo yenye sauti kali, huko tuliingia kanisani, tukasoma maandishi ya kiarabu na kuona neno "Allah" na kusikia simulizi za kina Hasan Otango na ushujaa wao, nikiwa ndani pangoni nilibahatika kukutana na kupiga picha na mzimu wa mabavu na utajionea mambo mengine kibao huko siku ukipanga kutembelea mkoa wa Tanga na kwenda moja kwa moja kwenye mapango ya Amboni, usipange kukosa.

IMG_20240407_101719-01.jpeg

pichani nikiwa na muongoza watalii na mzimu wa mabavu katikati yetu.


IMG_20240407_105632-01.jpeg

Baada ya kumaliza vurugu zote hapo na kuuliza maswali yasiyo na idadi, mwishowe tulianza safari nyingine kwenda kulitafuta daraja kongwe la Amboni, huko nilijipima uoga kwa kuvuka juu ya daraja la mbao lenye miongo kadhaa, niliona daraja la zamani za kale na daraja jipya la Amboni, huko tulikatiza katika eneo la viwanda lililotelekezwa, tulitembea kupita eneo lenye minazi mingi ambayo sikuwahi kuona idadi kubwa namna ile toka kuzaliwa kwangu na mwisho majira ya mchana kabisa tulifika katika eneo la Galanos hot springs na hapo tulipokelewa na muhusika mkuu na muongoza matambiko na shughuli zote za masimulizi kwa wageni wanaotembelea eneo hilo. Hapo sasa nilijionea tofauti za kiimani na kisayansi, wenyewe wanasema maji ya maajabu, mimi naamini maji yale yanatokea kutokana na msuguano wa miamba au namna yoyote ile ya kisayansi nisiyoijua kwasababu mimi sio mtafiti lakini sio shida, unaweza kufanya maombi yako hapo na matambiko na kufanikiwa kama wenyeji wanavyotuabalisha. Haikuwa sanaa lakini tuliacha tumeomba kitu pale

Pia nilisahau kitu. Kama ukipata kutembelea huko usisahau kunywa pombe ya mnazi, kama mtumiaji na kama sio mtumiaji unaweza kujaribu vitu vya asili kwa kuwa maeneo hayo kuna uzalishaji mkubwa sana wa kinywaji hicho na mimi pia nilionja kidogo japo sikulewa nadhani haina kilevi sana.

( Hadi wakati ujao, nitaweka mwendelezo hapa )

#allabouttanzanialife 🔴🟠⚪️
 
Kama Tabora ,Lindi, Mtwara,Rukwa na Mafya kwa baadhi tu, kwa kimombo tunasema are less developing regions sababu kuu kupelekea hivi Mwarabu hukuweka msisitizo kwenye elimu alafu .
Kwani mwarabu na muingereza nani alitawala Tanganyika na hali ilikuwaje kwenye utawala wake???

Hizo ni mindset na stereotype zako zisizo na kichwa na miguu......
 
Mbega,Iringa,Njombe,Katavi je huku kuna waislamu wengi!?
Mbona huku nako masikini wa kutupwa!?
Laumuni akili zenu za kipumbavu za kiweusi msilaumu dini.
Mbona hao wenye dini Saudi Arabia wameendelea Kuliko taifa lolote hapa Afrika!?
Sio Afrika tu ni duniani kote wakati fulani Trump akiwa rais wa Marekani alikuwa akilalamika serikali yake kutoa ulinzi kwa saudia wakati nchi yenyewe ina uwezo kiuchumi kiasi wanaweza kufanana na Marekani!!!
 
Kama Tabora ,Lindi, Mtwara,Rukwa na Mafya kwa baadhi tu, kwa kimombo tunasema are less developing regions sababu kuu kupelekea hivi Mwarabu hukuweka msisitizo kwenye elimu alafu .
Rukwa mwarabu gani alikaa? Vipi dar es salaam mwarabu aliweka msisitizo kwenye elimu?
 
Sio Afrika tu ni duniani kote wakati fulani Trump akiwa rais wa Marekani alikuwa akilalamika serikali yake kutoa ulinzi kwa saudia wakati nchi yenyewe ina uwezo kiuchumi kiasi wanaweza kufanana na Marekani!!!
Mbona UMEROPOKA sasa hapo!?
Suala la ulinzi na uchumi linakuja je!?
We ulidai mikoa ambayo uislamu mwingi ni mikoa masikini,je hao Saudi Arabia ni nchi masikini!?
Kuna taifa hapa Afrika linaipata Saudi Arabia kiuchumi!?
Huyo Trump anazungumza hivyo ilhali watangulizi wake ndio wameanzisha uhusiano na Saudi Arabia mpaka kusaini masuala ya petrodollar.
Kwani hao USA hawanufaiki!?
 
View attachment 3033842Habari, karibu Tanga, huko wanapaita TA, Tanga rahaa na mahali pekee hapa Tanzania kwenye sifa ya kuwa nyumbani alipozaliwa bwana Mapenzi!!..

Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu nilibahatika kutembelea mkoa huu unaotoa jiji mojawapo kongwe zaidi Tanzania.. Dhumuni kuu likiwa kwenda kujionea mambo kadhaa kuhusu mkoa huo ikiwa na pamoja kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana huko na kubwa zaidi kujiwekea kumbukumbu binafsi ya kukanyaga ardhi ya mkoa huo kama ilivyo kwa mikoa mingine niliyotembelea hapa nyumbani Tanzania.

Haikuwa safari ya kuchosha sana kama vile niliyotembelea mkoa wa Tabora na Songwe mbali kabisa mpakani mwishoni mwa Tanzania huko. Kufika hapa itakuchukua masaa machache tu , na kutokana na hali hiyo nililazimika kuunganisha usafiri na kuweza kushuka mpakani eneo kati ya mkoa wa Pwani na Tanga na kupata picha kadhaa hapo kwaajiri ya kumbukumbu, na nikiwa maeneo hayo niliweza kubahatika kuona mashine ya kusagia nafaka kwa ukubwa wake ikisafirishwa kwa kutumia bodaboda 😁 , niliweza kuchangia michango binafsi kadhaa ya ujenzi wa majengo ya ibada niliyokutana nayo njiani ( kwa ufafanuzi ni kuwa pembezoni mwa barabara kunakuwa kumewekwa kitu mfano wa kibubu kikubwa na maelezo machache juu ya sadaka yako utakayoweka hapo) pia nilifanikiwa kuhakikisha kwa macho yangu kuwa eneo hilo hakuna bango linalokuonyesha sasa unaondoka mkoa wa Tanga, hapo kuna karibu Tanga pekee, lakini kwaheri mkoa wa Tanga utalipata kichwani mwako siku ambayo utafanikiwa kutoka huko.

View attachment 3033851

Kiukweli unaweza kufanya aina fulani hivi ya utalii wa kushangaza kabisa, mfano nilifanikisha kutembea zaidi ya kilomita tano kutoka mpakani mwa Mkoa wa Pwani na Tanga huku nikifanikiwa kuona kwa ukaribu maisha halisi ya wakaazi wa vijiji, kuona kwa macho jinsi mabasi na magari binafsi yanavyokatiza kwa kasi ya ajabu, usisahau watu kukushangaa, wewe unaona mambo mapya nao wanaona kitu kipya😁 pia ukipenda kutembea katika maeneo mapya au maeneo ambayo hukutegemea kabisa kama siku moja utakuwa huko unakuwa unajijengea hali fulani tofauti sana na furaha ya nafsi na utulivu wa ajabu sana.

Nilifanya matembezi hayo ya hisani hadi pale nilipoona inatosha sasa miguu inajaa vumbi na jioni inaingia, na uzuri zaidi ni kuwa njia hii ni rahisi sana kupata usafiri wowote kusonga mbele , ambapo ukiwa umesimama eneo zuri unaweza kusimamisha mabasi ya Tanga na ukapanda kama daladala tu, muhimu ujue kutofautisha mabasi yaelekeayo Tanga na mikoa mingine kama Kilimanjarona Arusha. Hivyo nikiwa njiani nikaiona Simba mtoto inakuja imechochea kweli kweli, umbali kama mita 500 hivi nikapunga mkono hewani na chini ya nusu dakika chuma kilikuwa mlango wazi na vile nilikuwa mwepesi ikawa kudandia tu juu kwa juu kama katekwa mtu.

Masaa kadhaa mbele tulikuwa ndani ya jiji la Tanga, njiani kukaribia jiji niliona majengo marefu ya kiwanda cha saruji, mashamba ya mkonge na vinyumba vingi vingi vya nyasi na udongo, barabara nyembamba na miji kadhaa iliyochangamka kiasi. Nilishukia kwa Minchi, kama sikosei, sehemu hiyo ilikuwa njiani mbele kidogo tu baada ya round about na huo ukawa usiku wangu wa kwanza ndani ya jiji la Tanga, siku yangu ya kwanza kukanyaga ardhi tukufu ya mkoa wa Tanga.

Kwa kuwa ilikuwa usiku sikuwa na mambo mengi zaidi ya kufanya utaratibu wa kupata sehemu ya kulala na nikiwa nimepanga kulala sehemu karibu kabisa na mji, na ilivyo bahati nzuri au mbaya kwangu na nafsi yangu nilitembelea jiji hili wakati ndugu zangu waislamu walikuwa katika kipindi cha mfungo mtukufu hivyo kwa mara ya kwanza niliingia kwenye mji huu kipindi hasi sana. Na sikutarajia tena kuona au kukutana na yale niliyokuwa nikisimuliwa na watu kuhusu mkoa huu, maajabu yote ni kama yalishapotea kutokana na wakati wenyewe.

"Haya ni masimulizi ya kweli, itaendelea hapa baada ya kuweka sawa kumbukumbu "

Muendelezo unapatikana maoni no 24 chini.

#Allabouttanzanialife 🔴🟠⚪️
Tanga hamna kitu mwezi wa 8 naenda Tanga, ukweli Tanga pabovu mno
 
Tanga hakujapiga hatua kabisa.
Hata mjini kwenyewe aisee ni nyumba za kale hawajazifanyia renovation kabisa.
Ila kwa uzuri asilia Tanga ni kuzuri kimandhari asilia.
Tanga mademu hadi usiku na members of the family wanacheat au kujiuza sana ucku
 
Tanga kuna ardhi ,na uoto mzuri lakini maendeleo hamna, nafikiri MLOZI mkuu wa Tanga kuwa duni, ni walipuuza elimu ya darasani na kuzingatia tamaduni za kiarabu kwa sehemu kubwa ,sehemu akiyopita Mwarabu kakueleweki kimaendeleo.
Tanga kuna ardhi ,na uoto mzuri lakini maendeleo hamna, nafikiri MLOZI mkuu wa Tanga kuwa duni, ni walipuuza elimu ya darasani na kuzingatia tamaduni za kiarabu kwa sehemu kubwa ,sehemu akiyopita Mwarabu kakueleweki kimaendeleo.
Safiri uende Dubai,Kuwait,Qatar,,Bahrain,Saudia,Oman nk,zote ni nchi za kiarabu,maendeleo yalioko huko,hutatamani urudi uliko toka.Hawa waarabu maendelea,kupita maelezo.Hasa hawa Oman,ndio walikuja Tanzania na sehemu nyingi za Afrika,nenda kwao ukaone maendeleo,utabaki kinywa wazi,kwa kushangaa.
 
Back
Top Bottom