Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 7
Nashangaa muda unaenda mbona haturuhusiwi kwenda kulala?
Yule bakabaka akastopisha kwata akasema hivi sasa ni saa 2 usiku muda bado kabisaa!
Kuruta tunaulizana muda bado kivipi akati tumetumia muda mwingi kombania.
kuruta wakisinzia wanapewa kazi ya kushindana kukimbia
Mimi sikua nasinzia nilikua najipa moyo muda simrefu tunaenda kulala ila wapiiiii.... kila muda bakabaka anasema ndo kwanza saa 2 kamili usiku.

Tunaimba chenja, mazoezi ya viungo kwenye mazoezi nilikua napenda viroba (squats) hata 100 nashuka tu nasihisi kuchoka. then bakabaka anasema hapohapo ulipo jilaze ulale! Basi watu fasta tunajilaza kwenye vumbi
Dakika 5 nyingi anasema inuka rukaruka kichura
Kuruta tulipata hasira hadi wengine wakaanza kusonya.

Hapa nilishangaa kitu! Kuruta anamsonya bakabaka halafu hafanywi kitu zaidi tu anasmile halafu anasema "kuruta fungua moyo huo"
Ila walikua wanaudhi fikiria mtu anakuambia lala ghafla ruka kichura anarudia mara nyingi zile hasira plus usingizi watoto wengine hawana adabu wanamsonya na yeye anablush tu.

Hamuwezi amini alfajiri ilifika tukishuhudia kwa macho! Sasa tunaulizana "mbona leo hatujaenda kulala?" Tutafanya nini ndo ishapita hiyoo

Tukapanga foleni mabio yakaanza, kama nilivyosema muda wa mabio niliupenda sana zile chenja ndo ugonjwa wangu nikawa nakimbia bila kutegea nafurahia kukimbia.

Tumerudi jogging uelekeo shambani, tukitoka shambani chai kuipata hadi ukimbie 2km, tukitoka chai uelekeo kwata
Sikupenda kwata nilikua nanga nimekula mabao mengi tu mpaka bakabaka akanichoka! Akaniambia labda utaweza vitu vingine kama ngoma coy, karate au kazi mchanganyiko.

Ratiba iliendelea mpaka wiki ikakata hatukurudi angani hatukulala wiki nzima!

Baada ya wiki sasa bila kulala! vituko vilianza mtu anachuma machungwa huku kafumba macho anaota kabisa
Mimi ile mabio nikawa nakimbia huku nasinzia, chenja naitikia miguu inaenda mbele lakini nimelala ila naota nakimbia.
Unaweza usiamini lakini hali ndio hiyo.

Bakabaka wakawa wanasema hawa itabidi leo wakalale wasije kutufia bure hapa!
Kitengo cha kuvuna machungwa tulikua tunapiga story sana na bakabaka.
Wiki ilipita bila kuoga.


Usiku ukafika mimi najua kabisa leo tunaenda kulala, nikawa na furaha , sasa muda unaenda ila haturuhusiwi, njaa ikawa inaniuma nikasema subiri nitoroke niende kunywa chai jikoni halafu nirudi fasta kombania nilihisi tulidanganywa leo tena tunakesha.

Lahaula nilijuta kwanini nilitoroka........

Itaendelea.

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
 
Kambi za kigoma sio powa kabisaa
 
Service man stress za maisha huwa zinawasumbua


Hilo chenja sijui ndo hili

Kumbweku mbweku cheza Mbele mbele cheza🎺

Langu lilikuwa kisantini kisantini kanitukana😃nimekulia familia ambayo kutakana ni dhambi sasa jeshini nikafungulia
 
Service man stress za maisha huwa zinawasumbua


Hilo chenja sijui ndo hili

Kumbweku mbweku cheza Mbele mbele cheza🎺

Langu lilikuwa kisantini kisantini kanitukana😃nimekulia familia ambayo kutakana ni dhambi sasa jeshini nikafungulia
Yah umepatia ndo hilo, nalipenda😄

Bora umenikumbusha nilikua nimesahau wanaitwaje kumbe "service man"

Wakorofi wanoko nahisi wanakua kiherehere ili wapate ajira.
 
Squats huwa wanaita Viroba...
Zoezi jepesi lilikuwa ni hili ... Hapo mmepiga pushups za kutosha mkisikia viroba position mnapumua kabisa

Kambi yetu sisi ilikuwa na shamba la mahindi kubwa wenyewe wanasema hili shamba mwisho ni upeo wa macho yako😃tulivuna mahindi week nzima hayaishi
 

karena
 
Wewe ndo umenikumbusha viroba!!
Majina ya vitu vingi nimesahau siunajua kule wana lugha yao
Kwetu pia mahindi yalikuepo tunapukuchua.
 
Yah umepatia ndo hilo, nalipenda😄

Bora umenikumbusha nilikua nimesahau wanaitwaje kumbe "service man"

Wakorofi wanoko nahisi wanakua kiherehere ili wapate ajira.
Kuna ugomvi jeshini hauwezi isha..

Service Man vs Kuruta

Wazalendo (wakujitolea wanaokuja tukiwa kambini) vs Kuruta maarufu kama ugomvi wa kuku wa kisasa na kuku wa kienyeji😃
 
Wewe ndo umenikumbusha viroba!!
Majina ya vitu vingi nimesahau siunajua kule wana lugha yao
Kwetu pia mahindi yalikuepo tunapukuchua.
Mimi maisha niliyapenda vitu vingi bado nakumbuka...

Nilikuwa napenda sana maelekezo ya mabio

Utasikia kuruti utanyoosha njia hii utakuta kibao kimeandikwa shule fulani hujaja kusoma hapa utapita kushoto utakata njia ya kwenda messi sio muda wa kula huu utanyoka wazi kuruti😃😃
 
Ukisikia one in million ndiyo huyo sasa 😂😂

Wale wa mle JKT’ nilikuwa nawasikia.. kuruti ndiyo afande, kwani mmechoka? Hapana afande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…