Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 4
Muda wa kunywa chai ilichukua kama nusu saa, mimi nilikunywa fasta nikakimbilia angani kwenye simu yangu nikawasha fasta nikampigia mama angu mpenzi...

Nipo kimya simu inaita nasubiri apokee... ile kapokea tu! Sijui hata mvua ya machozi ilitoka wapi Aisee nikaanza
"Mama huku sipawezi mimi nataka kurudi nyumbani tokea nilivyokuja jana jioni sijalala hata kidogo..." nikamuhadithia yote hapo kwikwi kama zote plus vumbi usoni ningekua na kioo ningejicheka

Mama hajanipa pole vizuri filimbi ikalia uelekeo uwanja wa damu.. basi nikazima simu nikafungia kwenye tranka nikaenda zangu uwanja wa damu. Muda wote sijamuona Anna, nilivyofika uwanja wa damu tukaambiwa tukae kikombania ndo nikamuona Anna sababu wote ni kombania moja.

Tumapewa order kila mtu akalete tranka lake likiwa na kila kitu hasiache kitu angani dakika 5 tuwe tusharudi!
Basi mzee nikawahi tranka langu na kweli kurudi uwanjani kuruta wengi washarudi kule hamna kuremba lah sivyo mabao matusi yanakuhusu.

Tukaanza kukaguliwa wenye simu zikakusanywa, hapo machozi yanatoka namkumbuka mama angu nakumbuka nyumbani.

Nikamsindikiza Anna kwenda kununua vifaa vyake hapo simu sina, namuwaza maza angu tu,
Nikakutana na namesake mjeda kumbe yeye yupo kitengo cha jikoni, huko ni karibu na dukani

Nikamfata nalia kua nataka kurudi nyumbani pia anipe simu niongee na mama.
Akaniambia kurudi nyumbani haiwezekani labda niumwe mahututi, muda ule bakabaka wengi hawezi kunipa simu niongee labda usiku muda wa kulala.

Aisee nikamwambia basi nimpe namba ya mama aongee nae mimi mara ya mwisho kuongea nae nilimzimia simu sababu ya kuwahi kombania hivyo atakua na wasiwasi.
Akakubali nikamuandikia namba chini nikasepa

Tukarudi kombania mazoezi yakaanza hapo mchana
Halafu bakabaka wa kombania yetu akatuambia "Yaani hapa tunarashiarashia tu mazoezi kamili mtaanza wenzenu wote wakija kambini"
Nikashtuka eeh kumbe haya mazoezi, hizi kazi ni cha mtoto mpaka wote tukamilike?

Uwanja una jua ule sijapata ona, huko mjini kipindi nakuja hali ya hewa mbona ilikua shwari kuna kaupepo kabaridi kwa mbali! Sasa mbona hapa jua kali la Dar likasome? Hapo natafakari huku napiga mazoezi
Mazoezi yenyewe sasa "Simama kaa, inama style ya popo anabeba mbingu" piga push up huku umekunja ngumi!

Nafanya huku nimenuna hadi bakabaka wetu alinitania "wewe wa kiume au wa kike"? Sababu sura nimeikunja hatari.

Sasa nikashangaa bakabaka wa kombania nyingine akaja na Mjeda namesake , wakaongea na bakabaka wa kombania B ghafla nikaitwa nikaongozana na mjeda namesake na bakabaka kumbe walikuja kuniombea ruhusa nikaongee nao.

Bakabaka akaniambia "mama ako anasumbua sijui umemwambia nini?" Ndo nikagundua mjeda namesake alimpigia mama muda ule, na mama anataka kuongea na mimi anifate akasingizia nimekuja bila ruhusa yake mimi mgonjwa wa moyo, tumbo mapafu hivyo anifate.

Yule bakabaka akasema "Chukua simu hii ongea na mama ako mtoe hofu najua anadanganya wewe mgonjwa ili akufate ongea nae mbele yngu kua huku upo salama kabisa"
Bakabaka hakua mkali kwangu niligundua ana mahusiano na huyo namesake.

Itaendelea....
Uzalendo huo
 
Yani natamani kuingia kwenye Uzi nilipige mbata..Matoto ya Mama kila kitu linalia tu kama mwanamke[emoji706]..Watoto wa Mama ndio hawa wakikutana na Mitiani ya maisha kidogo tu wanajinyonga,Au kutoa ndogo...Sasa apo poti angesema amuombe TIGO dogo ili apunguziw mazoezi unafkiri huyu Mtoto wa Mama asingetoa??
Watoto wa Mama inabidi mjue Dunia ni katili sana hii lazima uwe MGUMU sio Kuonesha huruma na kulia ovyo Haisaidii.Kuna siku utaishi bila mama ndo utajua dunia ni Katili
Pumba ndio hizi, hapa hujui kusoma au uelewa ni shida?!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA 5
Basi bhana simu ikapigwa wakaeka loudspeaker
Mama akaanza, "Ephen?"
Abee mama
"Eee niambie vizuri kuna shida gani huko au chakula cha shida?"
Hapana mama.. sasa naongea kwa kwikwi huku bakabaka ananikata jicho
Nikajikaza pale nikaongea nae akaniambia "nimeongea na mwanangu hapo, kaniambia ana jina kama lako atakuangalia vizuri jikaze sawa mwanangu?"
Nikaitikia ndiyo mama

Basi tukaagana rasmi na mama huku nikijua kumbe pale ndo nimefika mpaka miezi mitatu ipite.
Duh!! Sina jinsi zaidi ya kupambana na hali halisi.

CHAKULA CHA JESHI
Kwenye msosi jeshini nawapa hongera! nilijaribu kuulizia kambi zingine baada ya mafunzo jinsi walivyokua wanakula nao pia hawalalamiki.

Pale kambini asubuhi ni chai na mkate, mkate ni mkubwa mtamu mlaini wanapika wajeda kila siku.
Tena hawabanii kuongeza kama hujashiba.

Mchana ni ugali maharagwe na nyama, tena nyama ni moja ila kubwa kinyumbani ile ukiikata inatoka vipande vitatu. Na chungwa tumekula karibia kila siku
Kambi yetu ilikua ina shamba la machungwa.

Jioni saa 12 wali, maharage na chai siku mojamoja na mboga za majani. msosi umepikwa vizuri kama wa nyumbani
Huwa stress zangu zinaisha muda wa kula.

Kwenye msosi jeshini chukueni maua yenu.

MAVAZI YA JESHI
Hapa kwanza nicheke zile pitshorts kwa watoto wa kike sijazielewa kabisa, muda wa kukimbia , mazoezi zinapanda usawa wa mapaja inakua kama boxer.

Tukiwa kombania mapaja yoye nje tunaona kawaida sababu mtu una mastress ya kazi hujali kuhusu mwili tena.

Kwanini jeshi wasiweke wanawake wavae suruali ndefu za kitambaa zinazobana chini?
Kuepuka hii shida? Au kwao sio tatizo?

Nikiangaliaga picha zangu za jeshini na marafiki zangu, wote mapaja nje hakuna anayejali walaa nini!

MALAZI NA MAZINGIRA
Malazi ni mazuri, magodoro yanaridhisha, maji yalikuepo ya kumwaga kambini kwetu ila kambi zingine walilalamiKa hamna maji.

Maji yapo Ila muda wa kuoga hamna, kupiga week nzima bila kuoga ni kawaida na harufu husikiii. Sanasana watoto wa kiume.

Mazingira masafi sababu usafi tunafanya wenyewe tunasimamiwa, vyoo vinaridhisha ksbisa.

TUKUTANE KESHO KWENYE WEEK 6 ZA MATESO, KUMBE TUNAWEZA KUKAA ZAIDI YA WEEK BILA KULALA!
Sijui nitakuja tena?
 
mimi niliishia kwa kuku🤣 na ng'ombe...kwa ng'ombe nilikuwa naweza kumnyonya ng'ombe kama ndama...harafu siku kaa sana hapo...

tulipigwa kibogo cha kwenda dodoma kwenye dhabibu kisha oljoro...nikamaliza muda nikarudi uraiani...

hivi sasa naendesha tu boda boda yangu jiji la darisalama...wenzangu wananishangaa jinsi ninavyo kamatwa na trafick na kuachiwa muda huo huo bila kutoa chochote🤣🤣🤣

jeshi limeniwekea kinga kubwa sana ya kukamatwa 🤣🤣🤣 kwa kifupi sijawahi kukamatwa na haitatokea nikamatwe​
Mbona unasema unakamatwa then unasema hujawahi kamatwa?
 
Asante kwa ufafanuzi.

Ila kwa hapa bongo wanajeshi wengi mdebwedo.
sio kweli...ndugu yangu usije ukaingia kwenye 18 zao...ila kikubwa timings tu ukimuwahi umemuweza akikuwahi amekuweza...!

juzi tu hapo kawe Luternant amechomwa bisi bisi ya moyo na boda boda akakata moto...

game la mapambano ni la kuwahiana. ukizubaa umeuawa.

wenyewe wana msemo wao "ADUI SIO BABA YAKO..."​
 
Hivi kupita jeshi kuna umuhimu gani haswa?
hakuna umuhimu wowote ni utumwa kama utumwa mwingine mimi nimeshaapa nikiwa hai nita pambana watoto wangu wasije wakafanya kazi zinazo husiana na Ulinzi...iwe JESHI, POLISI, USALAMA, MAGEREZA na Taka taka nyingine kama hizo .

hizo kazi ni za kitumwa sana...!

 
Habari!

Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"

Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana! Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.

Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.

Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.

Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.

Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.

Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.

Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂

SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.

Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.

Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.

Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiance zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.

Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiance asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.

Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"

Basi tulivyokua kwenye Hiance tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.

Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.

Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini"
Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu

Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.

Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.

Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita service man (mjeda anayejitolea) chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.

Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.

Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.

Itaendelea......
Hizo mambo za mazoezi kugeuka kuwa adhabu ndizo zilinifanya nichukie aina yoyote ile iitwayo jeshi.Sijawahi kutamani wala kwenda na sitoruhusu mtoto wangu kwenda huko.
 
Interview huanzia kuanzia siku ya kwanza unaripoti hapo getini ripoti wanaandika huyu tumepokea ni selule yaani mtoto wa mama huyu Jeshi hamna kitu wanaweka na marks zinahifadhiwa.Baadaye kwenye Kila eneo la mafunzo unatizamwa na wafunzi tofauti marks zinahiadhiwa Kwa Siri baadaye Kuna lile zoezi la kulenga shabaha unatizamwa unaangaliwa uwezo wako Kuna hizo ajira wengine huondoka nazo siku ya kufunga mafunzo tu anaambiwa Kwa Siri wewe ukitoka hapa karipoti Jeshi Fulani Nenda na barua hii au ukifika pale jitambulishe wewe Fulani usimwambie mambo mengi faili lako litakuwa limemfikia
Sio kuwa tu kuwa umekanyaga JKT ajira ipo.Perfomance ilikuwaje huko ?
Tafuta pesa na connection mkuu hizo performance utapata kiurahisi tu acha kuteseka.
 
Form six gani Hiace anaita Hiance? Halafu wewe huu uandishi wako ushaharibiwa. Hakuna kitu umebaki nacho. Ndo maana mzee wako alitaka uende jeshini ukakaze misuli ya matako. Umeshalegea sana. Mwanaume hawezi omba saidiwa na mwanamke na hawezi lia eti anamwita mama yake. Wewe ni takataka. Ondoka hapa na uzi wako.
Wapi kasema ni mwanaume?
 
Back
Top Bottom