Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 3
Watu tunang'oa visiki huku tunasinzia, yule mjeda namesake akanifata "njoo huku" nikaenda sasa kuna vichaka vingi akanipeleka kichaka flani hivi majani yamekaa kimduara katikati uwazi upepo unapita. Akaniambia "lala hapo muda wa kuondoka ukifika nitakufata" nikapiga zangu mbonji.

Nakuja kushtuliwa na mateke, nimekurupuka namuona bakabaka ananitizama tena ana nyota mbili (bakabaka - mwanajeshi aliyeajiriwa) "toka huko chuchumaa hapa haraka" nikatii amri mzee.
Umefikaje huku? Swali nimepigwa...

Nikafikiria nikaona siwezi kumchoma mjeda namesake ni vyema nipambane na hali yangu.
Nikaanza kujitetea pale, "Mimi naumwa vidonda vya tumbo nimezidiwa nikaona nipumzike hapa" akamwita mjeda hana cheo akamwambia naomba umshughulikie huyu.
Yule mjeda akaniambia "adhabu yako utabeba kisiki kikubwa peke yako kupeleka kambini". Nikaona nishaanza kupata msala mapema muhimu nikurudi nyumbani.

Nimekaa kihuzuni mjeda namesake akaja "nimekutafuta kule sijakuona" nikamwambia nilifumwa nikampa mkasa wote akaniambia nisijali atanisaidia. Kweli saa 4 ikafika filimbi ikalia kisiki kimoja mnabeba watu wawili kwenda kambini. Yule bakabaka akasema yule mwenye adhabu yangu yuko wapi? Nikaenda akanipa kisiki kikubwa machozi yakaanza kunilenga.

Akaniambia unatoka mkoa gani nikamwambia Dar! Akacheka sana "mbona watu wa dar wajanja? Wewe kitu kidogo unalia ebu acha usen....."

Nikapewa kisiki kikubwa peke yangu yeye akaondoka, namesake akawapasia kile kisiki kuruta wengine, akawaita wakaka wawili akawaambia kisiki chao wanipe mimi changu wabebe. Hawakupinga fasta wakabeba.
Kama kawaida uelekeo kambini, umbali kutoka pale shamba hadi huko ni kama 2km, kutembea ni mchakamchaka.

Tumefika tukaenda dining, tukakuta bakabaka kama wote
"Aya kila mtu ana kikombe chake! chukua ndoo nenda kituoni kajaze mchanga ulete hapa ndo uchukue chai"
Kituoni ni kule siku ya kwanza tuliposhuka na gari
Njaa inauma, muda huo nikawa sisikii tena kulia ila hasira kama zote nikajuta kwenda jeshi.

Kufika huko kituoni michanga yenyewe ina maji, nikatiliwa mchanga nikamuomba yule mjeda aniwekee ndoo nusu sababu kipara plus ndoo ya mchanga nzito, akaniwekea.
Niliporudi jikoni kumbe bakabaka wanakagua kama ndoo imejaa au ipo nusu........

Tupo kwenye foleni ya kukaguliwa machozi yananilenga najua kabisa narudishwa nikajaze ndoo, akaja mjeda namesake akaniuliza "ndoo yako imejaa? Nikamwambia hapana
Basi kuna kuruta alikua anapita amerudishwa akajaze ndoo mjeda namesake akamwambia chukua mchanga wako muongezee huyu wewe ukajaze tena!

Yule akupinga akanijaziwa ndoo nikakaguliwa imejaa nikachukua chai na mkate.

Uzuri chai imekolea sukari na mkate mzuri mkubwa nikala nikashiba ila majonzi yakawa palepale ninayo moyoni.

Yaani siwezi kupewa msosi mpaka jasho linitoke?

Nikipata upenyo lazima nimpigie mama aje kunifata.

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
 
🤣🤣dah ndo maana hawa jamaa wakuaga na hasira na makasiriko hivi
 
Nakumbuka tulipewa order ya kuleta passport size photo ndani ya masaa ma 3 na Wakati huo ni saa 12 na nusu jioni. Anaefanikiwa ajira Usalama.
Hapo ina maana walisha WA shortlist wakajua mko fit kuanzia kichwani utatumia mbinu Gani upate Simu yenye kamera pamoja na kuwa haziruhusiwi kuwa nazo kambini ujipige passport size urushe Kwa Whatsapp internet cafe Kwa Simu na mwenye internet cafe atume bodaboda au gari alete mbio hizo picha ndani ya muda ukabidhi
Hiyo ilikuwa interview ya kufa mtu swali la mwisho kupima kama mna uwezo wa kikomandoo na IQ Iko juu sana na kupima muda umekaa kambini je mazingira ya nje wayajua vizuri au ukipewa ile ruksa siku mnaambiwa Leo mko huru uliitumiaje muda wote wa mafunzo? Kama hujui hata internet cafe Iko wapi na hujui Wana msàada wowote kwako?

Order ilikuwa Iko vizuri sana na lilikuwa agizo limetimilika kwenye Kila eneo la boss wa Jeshi Mwenye akili nyingi za kijeshi
 

Njiani kuna mjeda akaniona ni wale wanaojitokea ni binti mzuri mweupe sijui alifata nini kule Wallah!
Akaniambia usilie utazoea mwaya, unaitwa nani nikamwambia Ephen, kumbe ni namesake wangu bhana akafurahi akaanza kunitambulisha kwa wale wajeda wengine huyu ni mdogo wangu.
 
Tranka kichwani , 2kms ukiruka kichura
Duuh 😯😹😹😹🙌
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…