SEHEMU YA 4
Muda wa kunywa chai ilichukua kama nusu saa, mimi nilikunywa fasta nikakimbilia angani kwenye simu yangu nikawasha fasta nikampigia mama angu mpenzi...
Nipo kimya simu inaita nasubiri apokee... ile kapokea tu! Sijui hata mvua ya machozi ilitoka wapi Aisee nikaanza
"Mama huku sipawezi mimi nataka kurudi nyumbani tokea nilivyokuja jana jioni sijalala hata kidogo..." nikamuhadithia yote hapo kwikwi kama zote plus vumbi usoni ningekua na kioo ningejicheka
Mama hajanipa pole vizuri filimbi ikalia uelekeo uwanja wa damu.. basi nikazima simu nikafungia kwenye tranka nikaenda zangu uwanja wa damu. Muda wote sijamuona Anna, nilivyofika uwanja wa damu tukaambiwa tukae kikombania ndo nikamuona Anna sababu wote ni kombania moja.
Tumapewa order kila mtu akalete tranka lake likiwa na kila kitu hasiache kitu angani dakika 5 tuwe tusharudi!
Basi mzee nikawahi tranka langu na kweli kurudi uwanjani kuruta wengi washarudi kule hamna kuremba lah sivyo mabao matusi yanakuhusu.
Tukaanza kukaguliwa wenye simu zikakusanywa, hapo machozi yanatoka namkumbuka mama angu nakumbuka nyumbani.
Nikamsindikiza Anna kwenda kununua vifaa vyake hapo simu sina, namuwaza maza angu tu,
Nikakutana na namesake mjeda kumbe yeye yupo kitengo cha jikoni, huko ni karibu na dukani
Nikamfata nalia kua nataka kurudi nyumbani pia anipe simu niongee na mama.
Akaniambia kurudi nyumbani haiwezekani labda niumwe mahututi, muda ule bakabaka wengi hawezi kunipa simu niongee labda usiku muda wa kulala.
Aisee nikamwambia basi nimpe namba ya mama aongee nae mimi mara ya mwisho kuongea nae nilimzimia simu sababu ya kuwahi kombania hivyo atakua na wasiwasi.
Akakubali nikamuandikia namba chini nikasepa
Tukarudi kombania mazoezi yakaanza hapo mchana
Halafu bakabaka wa kombania yetu akatuambia "Yaani hapa tunarashiarashia tu mazoezi kamili mtaanza wenzenu wote wakija kambini"
Nikashtuka eeh kumbe haya mazoezi, hizi kazi ni cha mtoto mpaka wote tukamilike?
Uwanja una jua ule sijapata ona, huko mjini kipindi nakuja hali ya hewa mbona ilikua shwari kuna kaupepo kabaridi kwa mbali! Sasa mbona hapa jua kali la Dar likasome? Hapo natafakari huku napiga mazoezi
Mazoezi yenyewe sasa "Simama kaa, inama style ya popo anabeba mbingu" piga push up huku umekunja ngumi!
Nafanya huku nimenuna hadi bakabaka wetu alinitania "wewe wa kiume au wa kike"? Sababu sura nimeikunja hatari.
Sasa nikashangaa bakabaka wa kombania nyingine akaja na Mjeda namesake , wakaongea na bakabaka wa kombania B ghafla nikaitwa nikaongozana na mjeda namesake na bakabaka kumbe walikuja kuniombea ruhusa nikaongee nao.
Bakabaka akaniambia "mama ako anasumbua sijui umemwambia nini?" Ndo nikagundua mjeda namesake alimpigia mama muda ule, na mama anataka kuongea na mimi anifate akasingizia nimekuja bila ruhusa yake mimi mgonjwa wa moyo, tumbo mapafu hivyo anifate.
Yule bakabaka akasema "Chukua simu hii ongea na mama ako mtoe hofu najua anadanganya wewe mgonjwa ili akufate ongea nae mbele yngu kua huku upo salama kabisa"
Bakabaka hakua mkali kwangu niligundua ana mahusiano na huyo namesake.
Itaendelea....
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini