Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

SEHEMU YA 5
Basi bhana simu ikapigwa wakaeka loudspeaker
Mama akaanza, "Ephen?"
Abee mama
"Eee niambie vizuri kuna shida gani huko au chakula cha shida?"
Hapana mama.. sasa naongea kwa kwikwi huku bakabaka ananikata jicho
Nikajikaza pale nikaongea nae akaniambia "nimeongea na mwanangu hapo, kaniambia ana jina kama lako atakuangalia vizuri jikaze sawa mwanangu?"
Nikaitikia ndiyo mama

Basi tukaagana rasmi na mama huku nikijua kumbe pale ndo nimefika mpaka miezi mitatu ipite.
Duh!! Sina jinsi zaidi ya kupambana na hali halisi.

CHAKULA CHA JESHI
Kwenye msosi jeshini nawapa hongera! nilijaribu kuulizia kambi zingine baada ya mafunzo jinsi walivyokua wanakula nao pia hawalalamiki.

Pale kambini asubuhi ni chai na mkate, mkate ni mkubwa mtamu mlaini wanapika wajeda kila siku.
Tena hawabanii kuongeza kama hujashiba.

Mchana ni ugali maharagwe na nyama, tena nyama ni moja ila kubwa kinyumbani ile ukiikata inatoka vipande vitatu. Na chungwa tumekula karibia kila siku
Kambi yetu ilikua ina shamba la machungwa.

Jioni saa 12 wali, maharage na chai siku mojamoja na mboga za majani. msosi umepikwa vizuri kama wa nyumbani
Huwa stress zangu zinaisha muda wa kula.

Kwenye msosi jeshini chukueni maua yenu.

MAVAZI YA JESHI
Hapa kwanza nicheke zile pitshorts kwa watoto wa kike sijazielewa kabisa, muda wa kukimbia , mazoezi zinapanda usawa wa mapaja inakua kama boxer.

Tukiwa kombania mapaja yoye nje tunaona kawaida sababu mtu una mastress ya kazi hujali kuhusu mwili tena.

Kwanini jeshi wasiweke wanawake wavae suruali ndefu za kitambaa zinazobana chini?
Kuepuka hii shida? Au kwao sio tatizo?

Nikiangaliaga picha zangu za jeshini na marafiki zangu, wote mapaja nje hakuna anayejali walaa nini!

MALAZI NA MAZINGIRA
Malazi ni mazuri, magodoro yanaridhisha, maji yalikuepo ya kumwaga kambini kwetu ila kambi zingine walilalamiKa hamna maji.

Maji yapo Ila muda wa kuoga hamna, kupiga week nzima bila kuoga ni kawaida na harufu husikiii. Sanasana watoto wa kiume.

Mazingira masafi sababu usafi tunafanya wenyewe tunasimamiwa, vyoo vinaridhisha ksbisa.

TUKUTANE KESHO KWENYE WEEK 6 ZA MATESO, KUMBE TUNAWEZA KUKAA ZAIDI YA WEEK BILA KULALA!

Muendelezo soma Niliyoyashuhudia Jeshini
 
Mimi nimesoma shule ambayo waalimu ni majeda mnaamshwa saa kumi jua lile lile le mkemama ayaya iya iya mama mnarudia times ns fimes mbazunguka kiwanja mara 10,ukipumzika unakula teke hadi unazima unatulizwa kama mpira.

So tunajua hilo . Push za kijeda ,sio za kidada, na vingine vingi
Hivi huwaga unasoma comment zako kabla hujatuma 😀😀😀
 
SEHEMU YA 5
Basi bhana simu ikapigwa wakaeka loudspeaker
Mama akaanza, "Ephen?"
Abee mama
"Eee niambie vizuri kuna shida gani huko au chakula cha shida?"
Hapana mama.. sasa naongea kwa kwikwi huku bakabaka ananikata jicho
Nikajikaza pale nikaongea nae akaniambia "nimeongea na mwanangu hapo, kaniambia ana jina kama lako atakuangalia vizuri jikaze sawa mwanangu?"
Nikaitikia ndiyo mama

Basi tukaagana rasmi na mama huku nikijua kumbe pale ndo nimefika mpaka miezi mitatu ipite.
Duh!! Sina jinsi zaidi ya kupambana na hali halisi.

CHAKULA CHA JESHI
Kwenye msosi jeshini nawapa hongera! nilijaribu kuulizia kambi zingine baada ya mafunzo jinsi walivyokua wanakula nao pia hawalalamiki.

Pale kambini asubuhi ni chai na mkate, mkate ni mkubwa mtamu mlaini wanapika wajeda kila siku.
Tena hawabanii kuongeza kama hujashiba.

Mchana ni ugali maharagwe na nyama, tena nyama ni moja ila kubwa kinyumbani ile ukiikata inatoka vipande vitatu. Na chungwa tumekula karibia kila siku
Kambi yetu ilikua ina shamba la machungwa.

Jioni saa 12 wali, maharage na chai siku mojamoja na mboga za majani. msosi umepikwa vizuri kama wa nyumbani
Huwa stress zangu zinaisha muda wa kula.

Kwenye msosi jeshini chukueni maua yenu.

MAVAZI YA JESHI
Hapa kwanza nicheke zile pitshorts kwa watoto wa kike sijazielewa kabisa, muda wa kukimbia , mazoezi zinapanda usawa wa mapaja inakua kama boxer.

Tukiwa kombania mapaja yoye nje tunaona kawaida sababu mtu una mastress ya kazi hujali kuhusu mwili tena.

Kwanini jeshi wasiweke wanawake wavae suruali ndefu za kitambaa zinazobana chini?
Kuepuka hii shida? Au kwao sio tatizo?

Nikiangaliaga picha zangu za jeshini na marafiki zangu, wote mapaja nje hakuna anayejali walaa nini!

MALAZI NA MAZINGIRA
Malazi ni mazuri, magodoro yanaridhisha, maji yalikuepo ya kumwaga kambini kwetu ila kambi zingine walilalamiKa hamna maji.

Maji yapo Ila muda wa kuoga hamna, kupiga week nzima bila kuoga ni kawaida na harufu husikiii. Sanasana watoto wa kiume.

Mazingira masafi sababu usafi tunafanya wenyewe tunasimamiwa, vyoo vinaridhisha ksbisa.

TUKUTANE KESHO KWENYE WEEK 6 ZA MATESO, KUMBE TUNAWEZA KUKAA ZAIDI YA WEEK BILA KULALA!
Poleeee muziki wa jeshi si mchezo
Mwaka wetu tuliponea chupuchupu
 
Yani natamani kuingia kwenye Uzi nilipige mbata..Matoto ya Mama kila kitu linalia tu kama mwanamke[emoji706]..Watoto wa Mama ndio hawa wakikutana na Mitiani ya maisha kidogo tu wanajinyonga,Au kutoa ndogo...Sasa apo poti angesema amuombe TIGO dogo ili apunguziw mazoezi unafkiri huyu Mtoto wa Mama asingetoa??
Watoto wa Mama inabidi mjue Dunia ni katili sana hii lazima uwe MGUMU sio Kuonesha huruma na kulia ovyo Haisaidii.Kuna siku utaishi bila mama ndo utajua dunia ni Katili
Ni mdada hata sisi kambini wadada wengi walikua wanadeka, we wakiune ulie lie jeshini ase sipati picha utachakazwa wanaume unalia ndani kwa ndani imeisha.
 
Yani natamani kuingia kwenye Uzi nilipige mbata..Matoto ya Mama kila kitu linalia tu kama mwanamke[emoji706]..Watoto wa Mama ndio hawa wakikutana na Mitiani ya maisha kidogo tu wanajinyonga,Au kutoa ndogo...Sasa apo poti angesema amuombe TIGO dogo ili apunguziw mazoezi unafkiri huyu Mtoto wa Mama asingetoa??
Watoto wa Mama inabidi mjue Dunia ni katili sana hii lazima uwe MGUMU sio Kuonesha huruma na kulia ovyo Haisaidii.Kuna siku utaishi bila mama ndo utajua dunia ni Katili
Mbona kasema yeye ni mwanamke? Huu ujinga unamuandikia nani?
 
Sasa dogo hiyo ni kozi ya mujibu tena mnafundishwa uzalendo tu kwa miezi yenu mitatu then mnarudi kitaa huku mkirashia rashia MK, UP, Shabaha na Pori then Gwaride wengi mkiangukia vitengo vya ngoma coy, KO na Singe wengine Gwaride na kuondoka zenu. Sasa ungeenda kozi ya kujitolea au RTS ungesemaje?😄😄
Kiufupi tu mwambie hapo walichofanyiwa ni kurashia rashia tu na sio mziki kamili 😆😆😆😂😂😂🤣🤣🤣🚬🚬🚬🏃🏾‍♂️🏃🏾‍♂️🏃🏾‍♂️
 
Back
Top Bottom