SEHEMU YA 7
Nashangaa muda unaenda mbona haturuhusiwi kwenda kulala?
Yule bakabaka akastopisha kwata akasema hivi sasa ni saa 2 usiku muda bado kabisaa!
Kuruta tunaulizana muda bado kivipi akati tumetumia muda mwingi kombania.
kuruta wakisinzia wanapewa kazi ya kushindana kukimbia
Mimi sikua nasinzia nilikua najipa moyo muda simrefu tunaenda kulala ila wapiiiii.... kila muda bakabaka anasema ndo kwanza saa 2 kamili usiku.
Tunaimba chenja, mazoezi ya viungo kwenye mazoezi nilikua napenda viroba (squats) hata 100 nashuka tu nasihisi kuchoka. then bakabaka anasema hapohapo ulipo jilaze ulale! Basi watu fasta tunajilaza kwenye vumbi
Dakika 5 nyingi anasema inuka rukaruka kichura
Kuruta tulipata hasira hadi wengine wakaanza kusonya.
Hapa nilishangaa kitu! Kuruta anamsonya bakabaka halafu hafanywi kitu zaidi tu anasmile halafu anasema "kuruta fungua moyo huo"
Ila walikua wanaudhi fikiria mtu anakuambia lala ghafla ruka kichura anarudia mara nyingi zile hasira plus usingizi watoto wengine hawana adabu wanamsonya na yeye anablush tu.
Hamuwezi amini alfajiri ilifika tukishuhudia kwa macho! Sasa tunaulizana "mbona leo hatujaenda kulala?" Tutafanya nini ndo ishapita hiyoo
Tukapanga foleni mabio yakaanza, kama nilivyosema muda wa mabio niliupenda sana zile chenja ndo ugonjwa wangu nikawa nakimbia bila kutegea nafurahia kukimbia.
Tumerudi jogging uelekeo shambani, tukitoka shambani chai kuipata hadi ukimbie 2km, tukitoka chai uelekeo kwata
Sikupenda kwata nilikua nanga nimekula mabao mengi tu mpaka bakabaka akanichoka! Akaniambia labda utaweza vitu vingine kama ngoma coy, karate au kazi mchanganyiko.
Ratiba iliendelea mpaka wiki ikakata hatukurudi angani hatukulala wiki nzima!
Baada ya wiki sasa bila kulala! vituko vilianza mtu anachuma machungwa huku kafumba macho anaota kabisa
Mimi ile mabio nikawa nakimbia huku nasinzia, chenja naitikia miguu inaenda mbele lakini nimelala ila naota nakimbia.
Unaweza usiamini lakini hali ndio hiyo.
Bakabaka wakawa wanasema hawa itabidi leo wakalale wasije kutufia bure hapa!
Kitengo cha kuvuna machungwa tulikua tunapiga story sana na bakabaka.
Wiki ilipita bila kuoga.
Usiku ukafika mimi najua kabisa leo tunaenda kulala, nikawa na furaha , sasa muda unaenda ila haturuhusiwi, njaa ikawa inaniuma nikasema subiri nitoroke niende kunywa chai jikoni halafu nirudi fasta kombania nilihisi tulidanganywa leo tena tunakesha.
Lahaula nilijuta kwanini nilitoroka........
Itaendelea.
Muendelezo soma
Niliyoyashuhudia Jeshini