Lior
JF-Expert Member
- Jul 30, 2018
- 1,617
- 3,697
Sio muoga, hukuwa interested na jeshiSawa Mkuu nimekubali mimi ni muoga.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio muoga, hukuwa interested na jeshiSawa Mkuu nimekubali mimi ni muoga.
Yeah ugumu wake ni kwamba pale lazima uive ili uwe soja kamili maana ndio mwanzo wa maisha ya kijeshi. Na ili uive lazima upitie kila session/ kipindi kikamilifu bila kudodge kama JKT madogo wanavyododge nakujiona wao ni cocup😄😄Nimemaanisha kwake hiyo RTS ni noma poti.
Ndio maana ya OrderNakumbuka tulipewa order ya kuleta passport size photo ndani ya masaa ma 3 na Wakati huo ni saa 12 na nusu jioni. Anaefanikiwa ajira Usalama.
Form six gani Hiace anaita Hiance? Halafu wewe huu uandishi wako ushaharibiwa. Hakuna kitu umebaki nacho. Ndo maana mzee wako alitaka uende jeshini ukakaze misuli ya matako. Umeshalegea sana. Mwanaume hawezi omba saidiwa na mwanamke na hawezi lia eti anamwita mama yake. Wewe ni takataka. Ondoka hapa na uzi wako.Habari!
Nilipomaliza form 6 zikatoka nafasi za kwenda jeshi wanaita "kwa mujibu" basi nikaangaza macho yangu kwenye orodha nikaona "Ephen - Rukwa"
Basi nikafurahi sana, furaha haikua kwasababu naenda jeshi hapana! Hata mpango nayo nilikua sina ila tu niliona ni bahati jina langu kua kwenye list sababu sio wote uchaguliwa.
Nikawasiliana na marafiki zangu kuna baadhi walichaguliwa pia lkn hakuna niliyechaguliwaa nae kambi moja, nikaanza kusikia story plus video za status, instagram watu wanaeka makuruta wanavyogaragara kwenye matope, mazoezi magumu hadi wanalia, nikapata uoga hapo ikawa mzozo nikasema mimi jeshi siendi kwanza kunyoa kipara hapana.
Mzee akaniambia lazima uende, huko Rukwa mkuu wa kambi ni rafiki yangu hivyo wewe mateso hutoyapata nikafikiria nikaona huyu mzee ananipiga fix ili nijae mimi jeshi siendi.
Ila nikawa nataka sitaki na kilichokua kinanitatiza kwenda ni yale mateso tu niliyokua naona kwenye video.
Kuna siku rafiki yangu akanipigia simu kunishawishi twende ila akaniambia "Ephen twende kambi ya mkoa X achana na Rukwa huko wana mazoezi makali sana" nikamwambia kama hivyo fresh acha nijiandae tutaenda next week sababu deadline ilikua bado. Rafiki yangu nampa jina Anna.
Anna ana kaka ake ni mjeda sasa akawa anatupa tips muhimu za kuzingatia mojawapo alisema tranka tutakalobeba tusijaze vitu vingi tuweke vitu vyepesi ikiwezekana vitu tukanunue kambini hukohuko.
Mimi niliona usumbufu yaani nitoke na tranka tupu vitu nikanunulie kambini? nikanunua vitu vyote nikajaza kwenye tranka. Kumbe yule mjeda alikua na maana yake Aisee bora ningemsikiliza.😂
SIKU YA SAFARI
Tukatoka zetu na Anna tukapanda gari tunaenda kambi ya mkoa X japokua tumepangiwa kambi tofauti kila mtu.
Tupo kwenye gari nina furaha naenda kupata experience mpya pia nilifurahi kwenda mkoa mwingine sababu nimezoea dar tu, safari ilichukua almost masaa 7 tukafika huo mkoa X mjini, gari ndo mwisho.
Sasa wote hatujui nini kinafata hapo Anna yeye tranka lake niseme lipo tupu kabeba vitu muhimu tu, mimi nimejaza hadi kubeba linanishinda.
Tukamfata konda kumuuliza, "Sisi tunaenda kambi X tunaomba utupe muongozo" akatuambia pandeni bajaji hadi kituo flani mkifika kuna hiance zinaenda huko jina la kambi ndo jina la kituo cha kushuka.
Tukafanya kama alivyotuambia, tumeingia kwenye hiance asilimia kubwa wana vipara hivyo nikajua wote tunaenda kambini.
Kule tuliposhuka na gari nilipapenda sana ni kuzuri panavutia hamna pilikapilika nyingi nakumbuka nilimpigia simu mama, akaniuliza umepaonaje nikamjibu kwa furaha ni pazuri nimepapenda akaniambia "ukifika kambini nijulishe lkn ukiona huko mateso yamezidi nipe taarifa nikufate urudi nyumbani"
Basi tulivyokua kwenye Hiance tunaenda huko wilaya yenye kambi mwanzoni nasmile na Anna wangu ghafla akili yangu ikavurugika tuliingia barabara ya vumbi sijawahi ona, gari zima hatuonani, kila mtu kwenye gari katapakaa vumbi hadi kope zote nyeupe ndani ya pua nywele vumbi hapo nikapata sign ninapoenda sio pazuri.
Safari ilichukua kama masaa 3 tukaambiwa wale wa kambini mmefika.
Katika maisha yangu bad moment niliyowahi kuexperience ni hii siku, Tumeshuka tu nikaona njia ya vumbi imekata kulia ni ndefu kama 2km nikasikia sauti "Hapohapo wote chuchumaa tranka kichwani ruka kichurachura uelekeo huu hapa kwenda kambini"
Kudadeq ndo nikajua kwanini niliambiwa niende na tranka tupu
Anna yeye chap kachuchumaa tranka kichwani, mimi machozi yashaanza kunitoka nikamwambia Anna mimi nimeghairi siendi narudi nyumbani, hata sijamaliza sentensi nishakula bao la mgongo kutoka kwa mjeda akaanza kufoka wewe bila shaka umetoka Dar naongea tii Amri kwanini umesimama ? Aya tranka kichwani kuruka uelekeo huu.
Akaja mjeda mwingine akanitwika tranka kichwani hapo nishachuchumaa sikuweza kuimili kuruka na tranka.
Anna akaniambia lete nikusaidie chukua langu, yule mjeda aliona tu hata akinipiga ule mzigo siuwezi na Anna pia hauwezi akamwita mjeda anayejitolea chukua hili tranka wasaidie, basi nikapona hivyo.
Kimbembe kikawa hiyo kichurachura nikiangalia mbele sioni geti, ni mbali almost 2km ndo niruke kichurachura? Hapo machozi yananitoka nalia nkamwambia Anna "mimi namwambia mama anifate siwezi hizi mambo" Anna nae analia Ephen usiondoke ukaniacha mwenyewe bora hivi tupo wote Afadhali.
Nilihisi miguu inawaka moto inataka kupasuka, msafara tupo wengi hadi wanaume wanalia, sasa tulivyoloa vumbi hadi kope mtu ukimuangalia mwenzako unatamani kucheka ukisikilizia maumivu ya miguu unatamani kulia.
Itaendelea......
Hasira sio nzuri!Form six gani Hiace anaita Hiance? Halafu wewe huu uandishi wako ushaharibiwa. Hakuna kitu umebaki nacho. Ndo maana mzee wako alitaka uende jeshini ukakaze misuli ya matako. Umeshalegea sana. Mwanaume hawezi omba saidiwa na mwanamke na hawezi lia eti anamwita mama yake. Wewe ni takataka. Ondoka hapa na uzi wako.
Wewe ndo basi tena. Huu uandishi wako mbona wa kimchekea sana. Una deka kinyama.Mkuu unaongea tu! Mimi sikuzoea mambo hayo ndomaana ikawa mtihani
Kuna baadhi ya taasisi au wizara nyeti za serikali hawakupi ajira mpaka uwe umepita huko. Inakuongezea sifa na ulaji wake ni mnono bali si wa kitoto.Hivi kupita jeshi kuna umuhimu gani haswa?
Hasira lazima niwe nazo. Una jina la kiume unaandika kwa sauti ya kike.Hasira sio nzuri!
Nimekusamehe kwa kuniita takataka.
Sio muoga bali haukuwa interested kabisa na Jeshi na sumu walizokuwa wameshakujaza kitaa ukaona ohoo, na uliyoyakuta huko ndio kabisa ukawa unamuwaza mama tu muda gani atakuja kukuchukua. Inaonekana ilibaki kidogo ujikojolee simu zilipokusanywa, ukajua mawasiliano na bi mkubwa ndio bhasi tena 🤣🤣Sawa Mkuu nimekubali mimi ni muoga.
Don't mind.Hasira sio nzuri!
Nimekusamehe kwa kuniita takataka.
Umeotea episode nayoiandika ni ya hiyo simu kukusanywa😂Sio muoga bali haukuwa interested kabisa na Jeshi na sumu walizokuwa wameshakujaza kitaa ukaona ohoo, na uliyoyakuta huko ndio kabisa ukawa unamuwaza mama tu muda gani atakuja kukuchukua. Inaonekana ilibaki kidogo ujikojolee simu zilipokusanywa, ukajua mawasiliano na bi mkubwa ndio bhasi tena 🤣🤣
Sic Tanga sehemu hizo tatu.Ni Mafinga au Dom?
Si haukutaka nikufundishe?😜Hizi ndo story nataka sasa,usisahau kuandika style ya kabali la kutoa roho ya mtu chap kwa haraka...tafadhali