Nimchokoze Mohamed Said juu ya historia ya Denis Phombeah; ni vipi alishiriki katika uhuru wa Tanganyika?

Kwenye kitabu chake nimesoma kuna habari nyingi zaidi za huyu Phombeah

Kasome kwanza ndio uje u criticize
 
Mzee Hekima nyingi sana watumia, Wallahi tunaenjoy sisi vijana wanaharakati kuishi katik zama za pumzi zako. Allah akuhifadhi tuyajue mengi kutoka kwako. Allahumma Amiyn
 
Mzee una nongwa bayaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].humpi hata pumzii
 
Mzee una nongwa bayaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].humpi hata pumzii
Mwana...
Muhimu tufanye mjadala wa kistaarabu.

Pumzi kubwa nampa yenye manufaa.

Anaingia kwangu akiwa hajui na anatoka na elimu na maarifa.

Denis Phombeah akiwa Meneja wa Ukumbi wa Arnautoglo aliweka mazingira mazuri ya TAA kufanya mikutano yake pale.

Phombeah katika Uchaguzi wa TAA wa 1953 alitumia pikipiki yake kwenda huko na huko kumfanyia kampeni Julius Nyerere amshinde Abdul Sykes.

Halikadhalika Phombeah na Ally Sykes mwaka huo huo Nyerere sasa akiwa President wa TAA waliwakilisha Tanganyika kwenye mkutano ulioitishwa na Kenneth Kaunda kukutanishwa vyama vya Waafrika chini ya Sahara.

Ally Sykes akiwakilisha Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) na Denis Phombeah akiwakilisha TAA.

Wajumbe hawa wakakamatwa Salisbury, Southern Rhodesia kama wahamiaji wasiotakiwa wakarudishwa Dar-es-Salaam.
 

Hapo unamuonea Mzee wetu, hii habari ni kweli ameombwa aiandike hapa lakini tayari ameshasema yeye ndio aliiandika Kwa kirefu kwenye mojawapo ya vitabu vyake.
 
Hapo unamuonea Mzee wetu, hii habari ni kweli ameombwa aiandike hapa lakini tayari ameshasema yeye ndio aliiandika Kwa kirefu kwenye mojawapo ya vitabu vyake.
The Monk,
Naogopa kuonekana najisifu lakini si rahisi mtu kunipuuza.

Yeye hajaweza kufanya hilo.
Yuko hapa ananisoma.
 
The Monk,
Naogopa kuonekana najisifu lakini si rahisi mtu kunipuuza.

Yeye hajawezq kufanya hilo.
Yuko hapa ananisoma.

Hekima ya Hali ya juu sana na ustaarabu mwingi unauonyesha.

Achilia mbali habari za huyo Phombeah, watu wanaopata darsa kuhusu ukumbi maarufu na wa Arnautoglo na mengine mengi ya kujifunza.

Endelea kutupa elimu Mzee wetu.
Pia nikutakie Heri ya mwaka mpya 2023, Mwenyezi Mungu akutunze, akuzidishie baraka na Rehema zake, Akujalie afya njema na azidi kujalia hekima na busara.
 
Monk,
Ahsante na Amin.

Mimi nimesomeshwa elimu ya mjadala kwenye madrasa na Sheikh Haruna.

Alisisitiza sana kusoma vizuri somo unalotaka kujadili au kufundisha.

Akanifunza na adabu.

Akisema ukitaka kupoteza heshima yako basi kuwa na lugha mbaya isiyochunga murua.

Tutoe elimu bila khiyana.
 

Ahsante Kwa hili Somo la adabu na staha pia Mzee wangu.
 
Nzee tupe elimu udini na ukabila sisi wa africa isiwe hajenda kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…