Nimeacha hii biashara bora nifuge kuku wa kienyeji

Nimeacha hii biashara bora nifuge kuku wa kienyeji

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Heshima kwenu wakuu.
Nimejaribu kuwekeza kwenye sekta ya usafirishaji kwa mda sasa yaani daladala . Ni shida kubwa sana kufanya hii kazi , ziko sababu kazaa kwa uzoefu wangu.

(1) Trafiki wana mtazamo hasi kuhusu magari haya ya daladala, kwa hiyo wawapo barabarani huwa wanajiandaa kupambana utadhani ni vita. Nimejionea hili mwenyewe , kwani wakati fulani hupata mda wa kuendesha mwenyewe. Unatozwa faini mpaka unakoma. Kwa wale ambao mnataka kuingia kwenye hii sekta jiandaeni na hili.

(2) Uhuni wa madereva na makondakta. Ni ngumu sana kupata dereva mwaminifu atakayeweza kukupa pesa na kuitunza gari yako. Wanaweza ukapewa pesa siku kadhaa lakini gari ikawa imehalibiwa vibaya mno kiasi kwamba ukipeleka gereji pesa zote zinatumika , na zingine zitakutoka kwenye mshahara wako.

Sina nia ya kutisha watu bali ninachoeleza ni uzoefu wangu katika hii biashara. Nadhani iko kasoro mahali fulani lazima ilekebishwe.
 
Me nishaachaga toka mwaka jana maana ilikua biashara ya kichaa nikauza icho kigari nikaimalisha shamba langu na mabanda asaiv nina kuku wakienyeji wakutosha to na wanyama maisha burudan sina presha tena
 
  • Thanks
Reactions: MC7

heri yako ulingundua mapema mkuu.
 
heri yako ulingundua mapema mkuu.
its about time mkuu inabidi usome alama za nyakati....Mwendokasi imeua daladala share labda uwekeze barabara za nje ya mji plus serikali nayo kama haioni umuhimu wa hawa watu
 
biashara yoyote ya chombo cha usafiri ni kichaaa

kuanzia daladala, bodaboda, bajaj, na malori... zote ni biashara ngumu sana...
 
kazi ya daladala kwa dar ngumu bt mi nasimamia gari 4 hivi huku mkoani kiukwel gari zina miaka 5 na nyingne 3 ila ziko kwenye hali ya kulidhisha na kwa sasa nimemwachia mwenye gari kwa kuwa Niko bize
 
  • Thanks
Reactions: MC7
its about time mkuu inabidi usome alama za nyakati....Mwendokasi imeua daladala share labda uwekeze barabara za nje ya mji plus serikali nayo kama haioni umuhimu wa hawa watu
Hii hali inatisha sana , yaani unaamua kuwekeza pesa yako kidogo angalau upunguze umaskini, lakini watu anakubana mpaka unakalibia kufilisika.
 
Back
Top Bottom