Nimeacha kuishabikia Arsenal

Nimeacha kuishabikia Arsenal

Nawakumbusha msimamo wangu bado upo pale pale.Nadhani juzi wote mtakubaliana na uamuzi wangu ulikuwa sahihi.

Magoli ya Man unaweza kuyaombea mkopo mkubwa bank na ukapewa bila wasiwasi.
 
Suala la mtu kuhama kushabikia from timu moja hadi nyingine kwa kweli mi haliniingii akilini and I get puzzed how can one dare to do that...!
Si kwamba sisi mashabiki wa Simba tunapenda mwenendo wa timu yetu, lakini tulianza kushabikia tukiwa na sababu tofautitofauti ambazo leo hii mtu akwambie hamia Yanga eti kwa sababu inamwenendo mzuri kwenye VPL sijui kama utaweza.
Vilevile, siamini kama inawezekana mtu uliyependa kushabikia say Arsenal, leo hii unaweza kwa urahisi kabisa Man U, au Totenham...! Siamini, labda kama ungesajiliwa kuchezea from one team to another lakini siyo kushabikia.
Ninachokiamini mimi ni kuwa: Ni rahisi kuacha upenzi wa chama cha Siasa ukahamia kingine (kwa sababu nyingi tu), au kuacha kumpenda demu uliye naye ukampenda mwingine lakini si rahisi kuhama kushabikia club yeyote ukahamia nyingine eti kisa inashinda sana...!

Tulia dawa iwaingie taratibu.
 
Kwa hii Arsenal ya Arteta siondoki.

Pale anatakiwa awepo kiungo mkabaji wa maana maisha yaendelee.
 
1662488211509.jpeg

Huyu Mwamba kaleta balaa kubwa
 
Wakuu nimeamua kwa hiyari yangu na pasipo kulazimishwa na mtu yoyote kuitosa club ya Arsenal.Nina sababu nyingi za kuitosa The Gunners.

[1] Kukwepa magonjwa ya moyo.

[2] Imeshindwa kutwaa kikombe chochote kwa muda mrefu sana.

[3] Arsenal imekuwa gulio la kuuza wachezaji wake mahiri kwa Club nyingine

Baada ya kutafakari kwa kinaa na bila kushawishiwa au kulazimishwa na mtu au kikundi chochote nimeamua kujiunga na Club ya Manchester United yenye kutumia uwanja Old Trafold.Zipo sababu kibao lakini nitazitaja chache.

[1] Manchester United inaongozwa na manager mwenye mafanikio makubwa kuliko makocha wote wa UK.

[2] Manchester United imechukua ubingwa wa ligi kuu ya UK mara 19,timu inayoikaribia ni Liverpool pekee yake imechukua ubingwa mar 18 tu.

[3] Manchester United inakaribia kuweka rekodi mpya kwa kuchukua ubingwa mara 20, mpaka leo hii inaongoza ligi kwa tofauti ya point 12.

[4] Ukiishabikia Mancheter United uwezekano wa kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari ni mdogo sana.Kila wakati una kuwa ni mtu wa kucheka na kufurahia maisha duniani.

[5] Mwaka 1999 iliweka historia kwa kuchukua vikombe vitatu.Ubingwa wa ulaya.ubingwa wa Uk na Kombe la ligi.

[6] Mashabiki wa Manchester United ni wakarimu, wapole na wenye kujua kuchambua soka. Sifa hizo zinanihakikishia kwamba nitapokelewa vizuri.

Wapenzi wa Arsenal mtanisamehe sana kuhama club ni jambo la kawaida kwa mashabiki kama ilivyo kawaida kwa wachezaji. Siwezi kuendelea kusononeka hapa duniania kisa kupenda Club mbovu.

Nakala: Wacha1 Idimi Belo Steve Dii Mphamvu Dark City gfsonwin The Boss BAK Rejao Viper mfarisayo MwafrikaHalisi Kibunango Maxence Melo EMT Balantanda Mwita Maranya
Uliruka mkojo ukakanyaga inya!
Ulichokimbia Arsenal ndo hicho unachopambana nacho Man U huku wenzio uliowaacha wanakula maini sasahivi.
 
Back
Top Bottom