Nimeacha Kushabikia Taifa Stars rasmi

Nimeacha Kushabikia Taifa Stars rasmi

Kwani ulivyoanza kushabikia ulitupa taarifa?
 
Nikiwa na akili zangu timamu kabisa wala sijashawishiwa na mtu yoyote yule, kwa aibu hii tuliyoipata leo toka kwa Algeria, naacha kushabikia timu ya taifa, kutiana presha sipendi tena, japo nitaonekana sio Mzalendo ila potelea mbali.
Inawezekana matokeo yamechakachuliwa, kumbuka Tanzania kwanza lawama baadae , hata Brazil walipigwa idadi hiyo ila kuitamka ndipo naanza kukuelewa inafedhehesha poleni sote.
 
Maguflka had kwenye magofulika ha ha ha ha Algeria na nyie hamtaniwi au ndio mpo kwenye HAPA KAZI TU!
 
Nani alisema mpira sio lelemama? Mbona hawa Taifa Stars wanacheza lelemama. Wamekatikiwa Mara Saba Kama vigoli.
 
Mumefanywaje...?
Wew ukiacha kushabikia Taifa Stars, wa Brazil watafanyaje...?
Nikiwa na akili zangu timamu kabisa wala sijashawishiwa na mtu yoyote yule, kwa aibu hii tuliyoipata leo toka kwa Algeria, naacha kushabikia timu ya taifa, kutiana presha sipendi tena, japo nitaonekana sio Mzalendo ila potelea mbali.
 
We sio mshabiki ni bendera fuata upepo, brazil alipigwa wiki kama stars, mashabiki wake walilia na kuomboleza, baada ya muda wakasahau maisha yanasonga, na mpaka muda huu anaongoza goli moja dhidi ya peru, tumecheza na timu bora na wachezaji wa ligi mbalimbali duniani we unafikiri ni nini kitatokea:what: sisi tuna Samatta na Ulimwengu ndio wachezaji tunaowatupia macho, nafasi yetu ilikuwa hapa nyumbani, wachezaji wetu wangetulia tungewafunga mengi na sisi, tusife moyo, nchi ni yetu, timu ni yetu. tuiunge mkono.
 
kwanini wasingefanya kama kile kilichofanyika zenji! warushe mech hadi mwezi ujao
 
Jecha yupo wapi? Tafadhali futa matokeo ya mechi hii. CCM yetu ndiyo imeshinda . La sivyo, mechi irudiwe.
 
Inawezekana matokeo yamechakachuliwa, kumbuka Tanzania kwanza lawama baadae , hata Brazil walipigwa idadi hiyo ila kuitamka ndipo naanza kukuelewa inafedhehesha poleni sote.

Ina maana wametuzidi sisi kwa uchakachuaji?basi nimeamini kila mjanja ana mjanja wake
 
Mechi ilikuwa na kasoro nyingi ikiwemo wa Algeria kuvaa jezi mpya na kufanya warm up kabla ya mechi kuanza. Taifaccm tulikuwa fair kwa kuvaa jezi za zamani maana fedha tulilipia deni la kutengeneza MRI na T-Scan Muhimbili. Jecha tafadhali futa mechi hii. La sivyo, shirikiana na NEC kuleta kapu la magoli feki.
 
Niliwaambia mapema,safiiii timu ya ccm imegogwaje?Haya futeni matokeo na jecha wenu.nimefurahije!
 
Back
Top Bottom