Nimeacha kusikiliza mziki wa wazibapua na chawa. Zilipendwa ndo habari

Nimeacha kusikiliza mziki wa wazibapua na chawa. Zilipendwa ndo habari

Joined
Nov 5, 2025
Posts
89
Reaction score
165
Nikiri wazi: tangu nimeacha kusikiliza muziki wa hawa wasanii chawa, moyo wangu una amani sana.
Nimengundua muziki wa zilipendwa umejaa madini na hekima nyingi sana, usiochosha kusikiliza.

Muziki wa Bongo umeharibika kabisa; wengi umejaa ngono tu. Umejaa kelele, uchi, na maudhui yanayochafua akili na kuharibu maadili ya jamii. Muziki wa kina Nasibu na wenzake umegeuka kuwa kichocheo cha ngono na upotoshaji wa vijana.

Kila ninapofungua nyimbo zao nikiwa nyumbani na binti zangu, najikuta katika wakati mgumu sana. Macho yangu hayaondoki kwenye skrini kwa hofu—kwa sababu kinachooneshwa si sanaa bali ni utupu mtupu. Muziki unaohamasisha ngono waziwazi, mavazi ya aibu, na ujumbe usio na maana.

Gez Kongole, hawa jamaa wawajibishwe. Wafundisheni hawa chawa. Wakirudi tena, waheshimu wananchi, warudi na muziki wenye staha, maadili, na ujumbe. Kwa sasa, muziki wa Bongo Tanzania umekwama—hauna maudhui ya maana zaidi ya ngono na upuuzi.

Akili inayotawaliwa na ngono hupoteza uwezo wa kufikiri kwa kina. Vivyo hivyo, jamii inayoruhusu mawazo ya ngono kutawala fikra zake hupunguza uwezo wake wa ubunifu, maamuzi ya busara, na maendeleo ya kweli.
 
Back
Top Bottom