Nimeacha rasmi kushabikia Manchester United

Nimeacha rasmi kushabikia Manchester United

Mme wenu

New Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
2
Reaction score
566
Ngudu wanajamiiforum wenzangu kuanzia Leo nimeacha kushabia team ya Manchester united sababu haina mikakati madhubuti ya kutawala EPL na kutetea wanyonge ili kuondoa ile Spain domination kwenye champions League.

Na natangaza kuhamia Manchester city sababu wana mikakati na kikosi kipana cha kuweza kuichallange hata real Madrid sio man united inayofungwa hadi na Huddersfield itakuwaje tukikutana na Madrid si utapigwa kama ambavu huwa zinapigwa team zenye kiwango kama chetu ambazo huko Spain zimeshashuka daraja ambazo ni Valladolid na Osasuna.

Sababu nyingne iliyonisukuma kuhama ni ubovu wa kikosi chetu kuanzia kocha hadi wachezaji wote tukianza na goal keeper sio mbaya sana lakini beki za Manchester united hasa Bailly na Lendof ni wabovu na wamezidiwa viwango na Endru Vincent a.k.a Dante

Eneo la kiungo tatzo ni kubwa mno likichangiwa na pogba ambae kiwango chake hakimfikii hata Shaban nditi wa mtibwa

Katika eneo la ushambuliaji napo hovyo kabisa wenzetu wana Hazad sisi tuna Martial na Lingard ambao viwango vyao wote hawamfikii Geoffrey mwashuya wa yanga na katika umaliziaji ni bora angefanya scouting ya kumchukua samatta kuliko kuwa na mzigo Lukake ambaye hana tofauti sana na tambwe Hamisi

Sababu nyingne ni Manchester united kujaza rundo la mashabiki walio na viherehere kwa Madrid na wasiojua mpira

Kuanzia Leo nipo Manchester city team iliyokamilika kila idara na inayocheza sexy football
 
Nani anaongoza kubeba mataji ya EPL mkuu,,, tuanzie hapo!!!
Any way kila la kheri uendako,,, ila sidhani kama uzi upo serious huu.... I guess n mamluki wa kuichafua timu,,,
 
Nani anaongoza kubeba mataji ya EPL mkuu,,, tuanzie hapo!!!
Any way kila la kheri uendako,,, ila sidhani kama uzi upo serious huu.... I guess n mamluki wa kuichafua timu,,,
Team imezeeka mkuu.
 
U cant be seriois mkuu,,, huezi mfananisha Dante na Baily,, !Mwashiuya na Martial??
Manchester City wana safari ya more than 15+ years kimafanikio huku Manchester United wakiwa championship ndio some how walinganishwe

Ufahamu upi mkubwq upo nao wewe?? Comparison hizo hata std Vii atashtuka,,
 
Acha kuifananisha Manchester United na vitu vya kipumbavu wewe!! Kwa nn usitumia Yanga na watu wangekuelewa tu!!!
 
Makombe ya thamani ya mapinduzi cup hayo ten million
sasa we unaona bora vipi, ukose makombe kabisa uwe coke zero au uchukue angalau ya mapinduzi?

na kama makombe ni hela basi Man u ndio timu bora ulimwenguni kwa sasa, sababu wana hela kushinda timu zote.
 
Safi sana umefanya uamuzi wa busara sana

Kuna timu ambazo ukizishabikia hata jehanamu kuna kuita siku ya kiama haijalishi hata kama ni askofu lazima uende jehanamu.

Wewe timu inajiita mashetani, hama kabisa
 
Back
Top Bottom